Wednesday, February 8, 2017

YESU ALIKUWA 100% MUNGU NA 100% MWANADAMU

Image may contain: text
Ndugu msomaji,
Tunaendelea kujifunza kuhusu Uungu wa Yesu. Quran, Allah, Muhammad na Jibril kwa mara nyingine tena wanakiri kuwa Yesu ni Mungu.
Hii ni sifa nyingine ya Mungu pekee na wala si ya mwanadamu.
Quran 40:2-3 Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye kujua. Anaye SAMEHE DHAMBI na anaye pokea toba, Mkali wa kuadhibu, Mwenye ukarimu, hakuna mungu ila Yeye; marejeo ni kwake.
Je, Bwana Yesu alikuwa na sifa hii ya kusamehe dhambi?
Katika tukio moja ambalo Yesu alionesha mamlaka yake ya Uungu kwa kusamehe dhambi na wakuu wa dini walioina hiyo kama kufuru kwani mwenye uwezo wa kusamehe dhambi ni Mungu pekee kwa vile hata wao hawakufahamu mamlaka ya Yesu ni Mungu
Marko.2:5-11 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, UMESAMEHEWA DHAMBI ZAKO.Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu? Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.
Hili ni mojawapo ya matendo ya Yesu ***kusamehe dhambi*** aliyotenda kuonesha Uungu wake na mamlaka yake.
Sura ya 4
Ubinadamu wa Yesu na sababu ya kuitwa Mwana wa Mungu toka mamlaka ya Uungu.
Ndugu mpendwa msomaji tutakubaliana kuwa hilo ni moja kati ya maswali nyeti yanayoulizwa na watu wengi wanao hoji na kutafiti mamlaka haswa ya Bwana Yesu.

“Ubinadamu wake”
Chanzo cha maswali yote yanayo ulizwa juu ya Bwana Yesu kinaanzia mara tu Yesu alipovaa mwili wa kibinadamu tendo hilo kwa fikra za haraka tu linaweza kudhaniwa kuwa ndilo linaloshusha mamlaka yake ya asili kama Mungu. Pamoja na hayo mimi binafsi nichoelewa ni kuwa tendo hilo kamwe halishushi mamlaka bali linafunika mamlaka aliyokuwa nayo kwa kadri ya sababu…………
Ifuatayo:-
Mungu aliwahi kujifunua wazi katika nyakati za nyuma na wanadamu wakaangamia
Fuatilia:- kutoka 19:20-21 Bwana akaushukia mlima, juu ya kilele cha mlima; Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda juu. Ndipo Bwana akamwambia Musa, Shuka chini, uwaonye watu wasije wakapasua njia waje kwa Bwana kutazama, kisha wengi miongoni mwao wakaangamia.
“swali la kujiuliza”
Je! Mungu aje katika hali gani ili mwanadamu aweze kuikabili?
“Jibu”
Ni lazima aje katika hali inayofunika uwazi wa mamlaka yake iliyo ya utisho kwa mwanadamu mdhambi.
Na anapokuwa katika hali ya ubinadamu ndipo anapoona njaa, kulia, kutembea, kusinzia na hali zote za ubinadamu anakuwa nazo na ndo maana Yesu ni Mungu 100% na mwanadamu 100%
Fuatilia kutoka 33:18,20 (Musa) Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako…. Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi
Sababu hiyo ya kimsingi ndiyo inayofanya Bwana Yesu kuchukua mwili wa kibinadamu kupitia Mariam kama tulivyo kwishaona. Hivyo mwili ya Bwana Yesu ulisitiri mamlaka kuu ya Uungu wake ambayo hainge kuwa busara kuufunua na kufanya binadamu kuangamia badala ya kuokolewa naye. Kwa kauli nyingine ni kuwa Mungu (Yesu) alitumia mwili huo ili kuwafikia waja wake kama tulivyoona hapo nyuma jinsi Mungu alivyojifunua hata kwa kichaka kwa kadri ya Qur-an tukufu. “Ubinadamu ni njia ya Mungu kusema na waja wake:”
Qur-an 42:51 ……….. Mungu husema na wajawake kwa njia ya:-
Ilhamu – sauti ya ndani ya moyo ya Mungu
Nyuma ya pazia – ishara ya kufunika mamlaka.
Kwa kadri ya Aya hiyo tunaona Qur-an ikitaja “Pazia” kama chombo cha mawasiliano ya Mungu kwa wanadamu, pazia hii umaanisha ni kitu kinachofunika ili kuzuia kuonekana kwa uhalisi wa jambo kwa lugha nyingine Mungu wakati Fulani huamua kufunika uhalisi wake kwa kujifunua nyuma ya “Pazia”.
“Pazia ni nini Kibiblia?”
Waebrania 10:20 ……….. ipitayo katika “Pazia” yaani mwili wake.
Katika Biblia Pazia huashiria mwili wa Bwana Yesu, hivyo hiyo ni njia ya kimawasiliano kati yake na binadamu inayofunika mamlaka yake ya Asili ya Uungu ili binadamu kumudu kukutana naye.
1Timotheo 3:16 Mungu alidhihirishwa katika mwili
Ebrania 10:5 Mwili uliniwekea tayari
Filipi 2:7 alijifanya hana utukufu …….. akawa na mfano wa mwanadamu.
Kwanini aitwe Mwana naye ni Mungu?
Tendo la Bwana Yesu kuitwa Mwana wa Mungu linaanzia kwenye chanzo cha kutwaa mwili.
Yohana 1:14 naye neno akafanyika mwili akakaa kwetu nasi tukaona utukufu wake utukufu
kama wa Mwana pekee atokae kwa baba …………..
Andiko hii linaonyesha hatua kuu mbili yaani:-
Kufanyika mwili
Kuitwa mwana atokae Mbinguni.
Sababu kuu
Tendo la Yesu kuamua kuchukua jukumu la kutuokoa lilimladhimu siyo kufunika Utukufu wake (Uungu ) tu kwa mwili bali pia kubadili kitambulisho chake cha mamlaka
“Fatilia mfano huu”
Maji yanaweza kugeuka katika hali mbalimbali katika kile ninachojua maji hayo mara yanapo badiri hali tu pia tendo hilo huambatana na kubadilli jina, yaani mfano maji yanapoganda hayaitwi tena maji bali huitwa barafu
Swali:- Je barafu si maji?
Jibu:- la barafu ni maji ila yamebadili asili kwa muda na baadae hurejea.
Sababu ya Bwana Yesu kuitwa mwana inatokana na kusudi lake tu la kuja Duniani Kutukomboa hivyo alifanyika barafu toka asili ya maji (alifaninyika mwana toka asili ya Uungu kama njia ya Ukombozi) lakini asili yake ya Uungu inabaki palepale.
Fuatilia ushauri mwingine juu ya Uungu wa bwana Yesu katika mafungu yafuatayo:-
Yohana 14:7-10……… aliyeniona mimi amemwona Baba
Tito 2:13 ……. Yesu Mungu mkuu na mwokozi wetu.
Yohana 20:28 Bwana wangu (Yesu) na Mungu wangu.
Ndugu mpendwa ninaamini hofu na mashaka ya moyo wako juu ya mada hii yamepingwa na uondolewa kupitia uchambuzi huu, fanya maamuzi yako leo kwa kujenga upya imani yako juu ya mamlaka ya Bwana Yesu kama tulivyo jifunza.
Hitimisho
Yesu ni Mungu na hivyo yeyote anayehitaji kwenda mbinguni, njia pekee na pekee tu ni Kristo Yesu-‘Matendo 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW