Thursday, May 31, 2018

MBEGU NI YA MWENYE KUPANDA


Bwana Yesu Kristo apewe sifa sana.
Mpendwa, umewahi kufikiria ni kwanini wakati mwingine unapata pesa/vitu katika hali ambayo haukutegemea kabisa kama ungepata na unaona kuwa ni muujiza tu hadi umepata?
Unatakiwa kujijengea utaratibu wa kumuuliza Mungu juu ya vitu mbali mbali ambavyo anakupa kabla haujatumia, kwasababu ni rahisi sana ukasema kwamba Mungu hajawahi kukupa mbegu kwenye maisha yako, kumbe amekuwa akikupa mara nyingi tu na wewe unakula bila kujua.
NGOJA NIKUPE MFANO HUU WA MBENGU.”Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, BWANA akambariki”. (Mwanzo 26:12).
Pia sadaka hii tunaikuta katika kitabu cha 2 Wakorintho 9: 10 Na Yeye ampaye mbegu mwenye kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa mbegu za kupanda na kuzizidisha, naye atayaongeza mazao ya haki yenu; Mungu anapokupa mbegu, maamuzi yanakuwa mikononi mwako;
Katika aya ya 10 inasema wazi juu ya mtu ampaye mtu mbegu. Hapo napata picha kuwa unaweza toa kitu kwa mtu au kwa Mungu kama mbegu. Sadaka hii imetajwa wazi kuwa ni sadaka ya KUPANDWA KAMA MBEGU.
1. Unaweza ukapanda – hilo ndilo lengo la Mungu kukupa mbegu,
2. Unaweza ukala hiyo mbegu – hiyo ni hasara kubwa kwako,
3. Unaweza ukaiutunza tu – hiyo pia ni hasara kwako (mfano wa mtu aliyepewa talanta halafu akakaa nayo tu bila kuitumia kuzalisha; Mathayo 25:14 – 28)
Iliuelewe zaidi kuhusu sadaka hii ya kupanda mbegu, Lazima ujue Mungu anavyoangalia mfumo wa kutoa. Mungu huangalia Kusudio la mtu ndani ya moyo wake. Angalia anasema. (2 Wakorintho 9:6-8). .”Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima;” Mungu haangalii sadaka iliyokuja mezani,anaangalia moyo wa mtoaji wa sadaka kwanza,anaangalia je! Mtoa sadaka huyo amekusudia nini. Unachokikusudia ndicho kitachoibeba sadaka yako. Mfano, umekusudia kuitoa hiyo sadaka kama mbengu hilo jambo ni lako. Mungu yeye hatenganishi kuwa huyu kaleta hii sadaka niiifanye shukrani, au sadaka kama mbengu au malimbuko nk. Wewe ndiye mwenye kukusudia kumpa Mungu hiyo sadaka na kujua ni ya shukrani au malimbuko au sadaka Kama mbengu.
Labda mpendwa wewe umesha kula mbegu mara nyingi sana na mambo yanakuendea vibaya. Usikate temaa, muombe Mungu atoaye mbegu. Ukisha ipata muombe akuonyeshe wapi uipande hiyo mbegu. Mbegu inazaa. Kikumi ni kulinda mali zako au kazi zako. Sadaka ni kusaidia tu na Mungu anakurudishia kiasi kile kile ulicho toa, LAKINI MBEGU UNAPATA MARA 100.
Marko 10: 30 ila atapewa MARA MIA sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.
Yesu anasema, utapewa MARA MIA sasa wakati huu, na sio baada ya kifo. Hivyobasi, Yesu anataka kukubariki sasa hivi.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW