Saturday, May 5, 2018

MUHAMMAD ANASEMA ISA BIN MARYAM NI ALLAH

KUMBE ISA BIN MARYAM NI ROHO YA ALLAH, NA ROHO YA ALLAH NI ALLAH.
Related image
Shalom Watumishi wa Mungu. Kwenye hili somo tutajifunza kuwa Isa bin Maryam ni Allah kwa uthibitisho wa aya za Quran.
Neno linasema Mungu ni roho kama ambavyo binadamu ni roho na ana nafsi na kushi kwenye mwili.
Nilipo anza kufanya utafiti kuhusu Isa bin Maryam nikagundua kuwa Allah mwenye roho moja na Isa bin Maryam wana share roho ileile.
Na Allah amemtoa kama mfano, Mariamu, binti wa Imran, ambaye *alitunza ubikira wake na ambaye ndani yake tulipulizia Roho Yetu;* ambaye aliyaamini maneno ya Bwana na maandiko yake na alikuwa kweli mcha Mungu. (Al-Tahrim 66:12.)
Masih, Isa mwana wa Mariam, alikuwa ni Mtume wa Allah na Neno Lake alilolirusha (au alilolituma) kwa Mariam; *roho kutoka Kwake*, na si zaidi ya hapo. (Al-Nisa 4:171)
kilichoingia tumboni mwa Mariam ni Roho ya Allah. Ikumbukwe kuwa roho ya Allah ni Allah. Na Isa ni roho ya Allah.
Katika Al-Anbiya 21:91 na Al-Tahrim 66:12, tumeona Quran ikisema wazi kabisa kuwa Allah anamwita Isa roho Yetu.
Na katika Al-Nisa 4:147, nako pia Quran inasema wazi kuwa Isa ni roho kutoka Kwake (yaani kutoka kwa Allah)... Hivyo basi Isa ni Allah kwa kufuata amrisho la roho ya Allah ni Allah.
Hakuna mwanadamu yeyote – kuanzia wanadamu wa kawaida, mitume na manabii wote - ambaye Mungu alisema, “Huyu ni roho yangu. Kwasababu Allah anajua kuwa roho ya Allah ni Allah. Lakini kwa Isa bin Maryam Allah anakiri kuwa Isa ni roho yake.
Katika Quran, ambacho ni kitabu kisicho na shaka, Allah aseme kuwa Isa ni roho Yetu. Yaani Isa sasa ana adhama ya Allah. Maana roho ya Allah na Isa ni moja.
QURAN..
Inatuambia wazi kuwa Isa bin Maryam ni roho ya Allah, maswali rahisi ya kujiuliza ni kuwa:
• Je, roho yangu na mimi tuko tofauti?
• Je, roho yangu si ndiyo mimi mwenyewe?
• Je, roho ya Mungu si ni Mungu mwenyewe?
Iweje Roho ya Allah ikawa Isa katika tumbo la Maryam na Isa asiwe Allah huku ikifahamika kuwa roho ya Allah ni Allah?
KAMA ROHO YA ALLAH NI ALLAH. Na Allah ameipuliza roho yake kwa Maryam. Na Allah anasema Isa ni roho ya Allah.
Iweje Isa asiwe Allah?
Shalom
Max Shimba mtumwa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW