Saturday, July 2, 2016

KUMBE QURAN IMEJAA SHAKA NA HAIPO WAZIWAZI

Je, madai ya kuwa Quran imekalika na ipo waziwazi ni ya kweli?
Allah ateremsha aya na kudai kuwa, Quran haijakamilika na haipo waziwazi.
Allah asema kuwa aya zingine ndani ya Quran hakuna ajua maana yake isipokuwa Allah.
Ndugu wasomaji;
Leo tutaangalia utata ulio jaa ndani ya Quran ambayo wanadhuoni wengi hudai kuwa imenyooka, huku Allah akiwapinga na kuteremsha aya ambayo inasema kuwa Quran haijanyooka na haipo waziwazi.
Kwanza tuanze kwa kuangalia aya ambayo inasema kuwa Quran ipo wazi na aya zake zimepambanuliwa ni uongofu kwa walio ongoka.
Surat HUD (11:1). Alif Lam Ra. Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimewekwa wazi, kisha zikapambanuliwa, kilicho toka kwa Mwenye Hikima na Mwenye Khabari
Surat Al Anaam (6:114). Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa na Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi usiwe katika wanao tia shaka.
Surat An nah’k (16:89). Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu
Surah tulizo ziweka hapo juu, zinasema na kudai kuwa Quran imepambanuliwa na ni kitabu kilizo elezwa waziwazi. Ikimaanisha kuwa, unapoisoma Quran, hautapata maswali au kusoma utata katika aya zilizo teremshwa na Allah.
LAKINI HAYO MADAI, YANAPINGANA NA UTATA KATIKA AYA IFUATAYO INAYO DAI KUWA, NDANI YA KURAN KUNA AYA AMBAZO ALLAH PEKE YAKE NDIE ANAZO ZIFAHAMU
Hebu tuisome hiyo aya:
Surat Al Imra (3:7) Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.
Ndugu zanguni, huu ni msiba mwingine katika Uislam, Allah katika Surat Al Imra iliyoteremka Madina anasema kuwa:
i. Ndani ya Quran kuna Aya mukham, zenye maana wazi,
ii. Zipo aya zenye mifano ambazo wanao zifuata hutafuta fitna na kutafuta maana yake,
iii. Zipo aya ambao hapana ajuaye maana yake ila Allah.
Ndugu zanguni, hii Surat 3 aya 7 inapingana na Surat HUD 11:1, Surat Al Anaam (6:114), na Surat An nah’k (16:89) zinazo dai kuwa aya za kuran zipo waziwazi na zimepambanuliwa.
Sasa, Waislam wafuate kipi?
Je, Waislam wanaamini kipi katika hii Quran inayo jipinga yenyewe na ambayo haipo waziwazi?
Mbona Allah anajipinga mwenyewe katika hizo aya hapo juu?
Au tatizo lilikuwa ni Muhammad ambaye alikuwa hajui kusoma wala kuandika na alishindwa kukariri maelekezo ya Jibril?
ZAIDI YA HAPO, kwanini Allah aliteremsha aya ambazo hakuna azijuaye ila yeye Allah?
Hizo aya zinamsaidia vipi Mwislamu?
Waislam wanapata faida gain wanapo zisoma hizo aya huku ikifahamika kuwa ajuaye maana zake ni Allah peke yake?
MWSIHO, ningependa kufahamu, hawa Waislam wanaelewaje kuwa aya walizo zisoma ndivyo walitakiwa walelewa huku ikifahamika Allah ameweka mtego kwa kusema kuwa, kuna aya ndani ya Quran ambazo ni Allah pekee anaye zifahamu.
Kumbe ndio maana Waislam wana pigana wenyewe kwa wenyewe kama ISIS, Sunni vs Shia, nakadhalika.
Kumbe ndio maana Quran inausaidizi wa Sahih Hadith na Suna za Muhammad.
Huu ni msiba mwingine katika dini ya Allah.
Kwanini Allah aliteremsha aya ambazo anazifahamu yeye mwenye?
Karibuni kwa Yesu aliye hai ambaye ametuletea Roho Mtakatifu kama Kiongozi wetu.
Yohana 16: 3 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. 15 Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari.
YOHANA 16: 26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
1 YOHANA 2: 27 Nanyi, mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, wala hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama mafuta yake yanavyowafundisha habari za mambo yote, tena ni kweli wala si uongo, na kama yalivyowafundisha, kaeni ndani yake.
Ndugu wasomaji, Yesu amesha weka kwa uwazi kuwa, ukimfuate yeye, basi utapokwa kipawa cha Roho Mtakatifu na yeye huyo Roho Mtakatifu ataishi ndani yetu na atatufundisha yote.
Karibuni kwa Yesu.
Mungu awabariki sana
Max Shimba Ministries Org

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW