Saturday, July 2, 2016

SINAGOGI SIO MSIKITI (SEHEMU YA PILI)


Kama tulivyosema Neno SInagogi linatokana na Kigiriki συναγωγή Sinagoge likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya Kiebrania בית כנסת beit knesset yaani "nyumba ya mkutano".
Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kutajia Sinagogi.
Katika lugha ya Kiebrania neno “ beit ” linamaana “ nyumba” ndio maana hata ukisoma Bethsaida “ Nyumba ya mvuvi” au bethsania-Nyumba ya masikini. Bethlehemu, nyumba ya mkate. (Soma injili imetajwa sana majina haya )
Katika Israeli ya Kale (kabla ya maangamizi ya Yerusalemu mwaka 587 KK) inaonekana hakukuwa na Sinagogi: walau halitajwi kabisa katika Agano la Kale.
Inaonekana ya kwamba masinagogi yalianzishwa baada ya hekalu ya Yerusalemu kubomolewa pamoja na kuanza uhamisho wa Wayahudi kwenda nchi mbalimbali.
Tangu kuharibiwa kwa Hekalu la Pili mwaka 70 Wayahudi wana masinagogi tu kufanyia ibada.
Neno hilo limetumiwa katika maana hiyo ya mukutano kwenye Septuajinti, yaani, tafsiri ya Kigiriki ya Maandiko ya Kiebrania. Lakini, baada ya muda neno hilo lilitumiwa kurejelea jengo ambapo watu walikutana kuabudu. Kufikia karne ya kwanza W.K., karibu kila mji ambao Yesu alitembelea ulikuwa na Sinagogi; Majiji yalikuwa na Masinagogi kadhaa; Jiji la Yerusalemu lilikuwa na Masinagogi mengi.
Ukumbi wa sala huwa na sehemu zifuatazo:
• Sanduku la Torati ni kabati au sanduku ambako hati za kuviringisha zenye mwandiko wa Biblia ya Kiebrania hutunzwa;
• Taa inayoendelea kuwaka muda wote;
• Meza ya msomaji ambako hati za torati hufunguliwa na kusomwa;
• Mimbari ya mafundisho;
• Kinara cha menorah chenye mishumaa 7 au 9.
Karibu na sanduku hilo, kulikuwa na viti vya mbele vilivyopangwa kuelekea kutaniko, navyo vilikaliwa na maofisa-wasimamizi wa sinagogi pamoja na wageni wowote waheshimiwa. (Mathayo 23:5, 6)
Hii ni tofauti ni Misikiti ya kiislamu isiyokuwa na Viti
Karibu na eneo la katikati la Sinagogi palikuwa na jukwaa lililokuwa na kinara na kiti cha msemaji . Kwenye upande wa mbele, wa kushoto, na wa kulia wa jukwaa hilo, kulikuwa na viti vya washiriki wa kutaniko .
• Kwa kawaida, gharama za kuendesha shughuli za Sinagogi zililipiwa na kutaniko. Michango ya hiari iliyotolewa na wote, matajiri kwa maskini, ilitumiwa kurekebisha na kudumisha jengo hilo
Bwana Yesu alipenda sana kufundisha kwenye hekalu na katika masinagogi walimokusanyika wayahudi.
“Sikuzote nilifundisha katika sinagogi na katika hekalu, ambapo Wayahudi wote hukusanyika.”—Yohana 18:20.
Hekalu katika Jerusalemu ( hekalu katika Uyahudi )
Kulikuwa na Mahekalu mawili yaliyojengwa katika nyakati tofauti tofauti na watu tofauti tofauti ndani ya Yerusalemu.
Hekalu la kwanza lilijengwa na mtoto wa mfalme Daudi, Mfalme Suleimani. Lilijengwa mnamo mwaka 957 KK.
Hekalu hili likabomolewa na mfalme Nebukadreza II mnamo 586 KK.
Hekalu la pili,
Lilijengwa 536 KK -515KK baada ya uhamisho wa Babeli.
Uhamisho wa Babeli ni kipindi ambacho Wayahudi walilazimishwa kuishi Babuloni. ( kwa lugha nyingine ni kwamba Wayahudi walilazimishwa kuishi Babeli,ambayo kwa sasa tunaweza kusema walipelekwa Iraq, sababu magofu ya Babeli yapo katika mji wa kisasa wa Al-Hillah, kando ya mto flati kama 90km kusini mwa Baghdadi)
Hekalu hili la pili linajulikana pia kwa jina la hekalu la Herode mkuu kwa sababu herode alihusika pia katika upanuzi na kuliwekea nakshi katika Hekalu hili. Wataalamu wa mambo ya kale wanasema kwamba liliwekewa wakfu na Yuda Mmakabayo.
Hekalu hili la pili likabomolewa na Warumi mwaka wa 70. Tangu hapo halikujengwa hekalu la tatu, bali Wayahudi waliendelea kukusanyika katika mikutano yaani Sinagogi na sio katika Hekalu tena mpaka leo hii.
Tangu hapo halijajengwa tena, hivi kwamba sadaka zinazodaiwa na Torati hadi sasa haziwezi kutolewa kwa muda wa miaka 2000 hivi.
TOFAUTI KATI YA HEKALU NA SINAGOGI NI KAMA IFUATAVYO.
~ Hekalu huwa ni jengo kubwa lenye sehemu mbali mbali za ibada,wakati Sinagogi huwa ni mkutano tu wa watu katika jengo lisilokuwa na mgawanyo mkubwa.
~ Hekalu lina sehemu ya patakatifu pa patakatifu, Sinagogi halina sehemu hiyo.
~Hekalu lilikuwa kuanzia agano la kale mpaka agano jipya mfano kuanzia kitabu cha 1 Samweli 1:9, mpaka Ufunuo 21:22- Wakati Sinagogi lenyewe halitajwi katika agano la kale bali agano jipya tu.
Swali:
MBONA BIBLIA INASEMA KUWA SINAGOGI NI MSIKITI WA WAYAHUDI?
UFAHAMU
Katika tafsiri ya Biblia Union Version yapo maneno kadha wa kadha yenye asili ya lugha ya Kiarabu na Kiswahili cha kimvita hii ina tokana na mfasili (Mmisionary) wa kwanza aliye tafsiri Biblia kumshirikisha mzee (Shekhe) ili aweze kusaidiana naye katika kazi hiyo iliyo onekana kuwa ngumu kwake kutokana na kutojua vizuri Kiswahili hivyo ndiyo maana utakuta maneno mengi yenye asili ya Kiarabu ndani ya Biblia (Tazama Mifano). Mashekhe kwa maana ya wazee, Kadhi kwa maana ya hakimu, Iddi kwa maana ya Sikukuu, kutawadha kwa maana ya kunawa miguu na kadhalika
Pamoja na hayo alipo tafsiri neno hili Sinagogi kuwa ni msikiti haku tafsiri kwa kuzingatia utalaamu wa lugha bali alifananisha mambo Fulani Fulani yanayo tendeka katika majengo hayo mawili yaani Sinagogi na Msikiti na ndipo akafasiri kuwa Sinagogi ni Msikiti wa Wayahudi kwa kulinganisha baadhi ya matendo yanayo fanana baina ya majengo hayo mawili.
Ni sawasawa na leo mtu kumwambia babu yake kuwa Computer ni Runinga ya kisasa wala kamwe hana maana ya Computer ni TV ila amechukua anachokifahamu mhusika ili kumweleza kitu au jambo Fulani. Hivi na sawa na mjaluo wa ugenya kusilimu kisha akirudi huku nyarigunga kavaa Kanzu yake akiulizwa vipi kulikoni? Anasema “Siku hizi mimi naenda ile Kanisa ya Waislamu” .
Hieleweke pia lugha yeyote ile iliyohai uzidi kuimalika . Ndivyo ilivyo na Kiswahili pia. mathalani leo tunayo maneno mengi yamezalishwa ambayo kimsingi miaka michache hayakuwepo kwenye kiswahili
Aina ya tafsiri iliyotumika kitaaluma
Kwa kadri ya taaluma ya Kiutafsiri mtafsiri huyo wa Biblia ametumia moja kati ya aina kuu mbili za kiutafsiri ambapo aina ya kwanza ni ile ya tafsiri “Shabihifu” na ya pili ni tafsiri “Maanifu”.
Hivyo kimsingi katika kutoa maana hiyo ya Sinagogi- Msikiti wa Wayahudi, msaidizi huyu katika utafsiri wa Biblia alionekana kukosa namna ya kulieleza neno hilo sinagogi na ndipo akaadhimu kutoa tafsiri hiyo ambayo kitaaluma siyo tafsiri “Maanifu” (haiendani na asili ya neno katika lugha husika) bali alitumia tafsiri “Shabihifu” inayozingatia mambo machache yanayofanana baina ya vitu viwili ndiyo maana alisema ni Msikiti wa Wayahudi hivyo kamwe hakusema kuwa ni Msikiti wa Waislam maana alitambua kuwa katika wakati huo bado uislam haukuwa umeanzishwa.
Lakini pia nimeelezea kuwa mtu anaweza akamwelezea mzazi wake kuhusu kumputa kuwa ni Runinga ya siku hizi, hii aina maana kuwa computer ni TV ila unafananisha anachokijua mhusika ili japo kumweleza.
Hivyo basi kwa kuwa wenyeji wa pwani walikuwa wana ufahamu wa misikiti, basi mfasiri akaamua kutumia kauli hii.
Ebu fikiria kwa Kiswahili mara nyingi huwa twafasiri neno Pharmacy kwa maana ya Duka la dawa!!! Lakini je ni sawa?
HEBU SASA TUANGALIE MAANA NA MAJINA YA MAJENGO YA IBADA ILI TUONE UKWELI WA NENO HILI SINAGOGI KATIKA UTAALAMU WA WA LUGHA
Je Sinagogi laweza kuwa ni Msikiti katika uasili wa lugha?
Qur-an Surat 22:40
Andiko hili linataja majina ya majengo mbalimbali ya ibada ikiwemo na Sinagogi ingawa halikuwekwa kwenye tafsiri ya Qur-an ya Kiswahili ila tutalichunguza kwa watafsiri wengine wa Qur-an hususani tafsiri ya kingereza iliyotolewa na Mwanazuoni wa Kislam ndugu Yusufu Ally.
Qur-an ya sura ya 22 :40 katika tafsiri ya kiingereza inaeleza yafuatayo
Those who have been expelled from their homes unjustly but only because they say our Lord is Allah for had it not been that Allah checks one by means of another have been pulled down Monasteries Churches Sinagogues and Mosques …….
Tafsiri ya aya hiyo katika Kiswahili
Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nymba za wat'awa, na Makanisa, na Masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu. Al barwani Ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki ila kwasababu wanasema mola wetu ni Mwenyezi Mungu, na kama Mwenyezi Mungu asingeliwakinga watu baadhi yao kwa wengine bila shaka yangelivunjwa Mahekalu, Makanisa, Masinagogi na Misikiti…………. Al farsy
Katika sehemu hii tafsiri hiyo ya Qur-an iliyotolewa kwa lugha ya kingereza inataja wazi kuwepo kwa majengo mawili kati ya manne ambayo kwahakika ndiyo yanayosumbua watu wengi hata hivyo Qur-an inaonekana tena kwa uwazi ikiyatofautisha majengo hayo ambayo ni Masinagogi na Misikiti. Hilo linaonekana siyo tu katika tafsiri bali hata katika maandishi ya lugha ya Kiarabu.
Fuatilia majina ya majengo hayo katika matamshi ya kiarabu na maana zake hapo chini.
BILASHAKA YANGELIVUNJWA
KISWAHILI KIARABU
1) Mahekalu Swawamiyu
1. Hekalu Swawaamiu
2. Kanisa Biyaun
3. Msikiti Masjid
4. Sinagogi Swalawaatun
Katika ushahidi huu yametajwa majengo manne lakini mwishoni tunakuta majengo mawili na jengo la kwanza linaitwa “Swalawatuni” yaani Sinagogi na la pili “Masjid” yaani “Msikiti” hivyo haya ni majengo yaliyotofauti kabisa maana Sinagogi ingekuwa ni msikiti lisinge itwa Swalawatuni kwa kiarabu bali lingeitwa Masjid hivyo hii inadhihilisha kuwa katika maana halisi ya lugha sinagogi kamwe haliwezi kuwa ni msikiti hivyo ni kama nilivyoeleza mwanzo kuwa neno Sinagogi lilimaanisha kikutanisho au kukutanika.
ENDELEA SEHEMU YA TATU
Edited by Max Shimba
Narrated by Mwalimu Chaka wa Musa

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW