Tuesday, August 1, 2017

KAMA MUHAMMAD ALIKUWA MTUME WA MUNGU, KWANINI HAKUWAI ONGEA NA MUNGU ALIYE MTUMA?

Image may contain: text and outdoor
Ndugu zanguni,
Hili swali limeenda shule.
Leo ningependa tujikumbushe mambo machache ambayo labda hatukuyatilia maanani. Mitume wote na manabii wote wa Biblia waliwai ongea na Mungu. Lakini, Mtume wa Allah "Muhammad" hakuwai ongea na Mungu HATA MARA MOJA. Je, utume wake tutauamini vipi maana hakuwai ongea na aliye mtuma?
Lakini Mitume wote wa Biblia waliongea na Mungu. Mifano michache hapa chini.
1. Musa anoangea na Mungu: Kutoka 3:1-21
2. Elia anaongea na Mungu: 1 Wafalme 19- Soma yote
3. Paulo anaongea na Mungu: Matendo ya Mitume 18:9 Wagalatia 1:1 Paulo, mtume, si mtume wa wanadamu aliyetumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu
Biblia ipo wazi kabisaa, kuwa Paulo alitumwa na Mungu, wakati Muhammad alitumwa na Jibril ambaye si Mungu. Koran inakiri kuwa Muhammad alikutana na Jibril na hakuwai kukutana na au ongea na Mungu hata mara moja. Lakini tunasoma katika Biblia kuwa, Paulo alipewa utume na Mungu mwenyewee.
Warumi 1:1 Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, ALIYEITWA KUWA MTUME na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu.
Hiyo ni mifano michache kutoka Biblia.
Kama Muhammad alikuwa Mtume wa Mungu, kwanini hakuongea na Mungu aliye Mtuma? Maana ya neno Mtume kwa kifupi: Ni Mtu aliye tumwa.
Mimi nataka mniletee aya ambayo inaonyesha kuwa Muhammad aliongea na Mungu.
Basi Mtume akafanya khofu, akarejea kwa mkewe, akamhadithia, na pale pale homa kubwa kabisa, ikampanda, akataka afunikwe maguo, akawa anatetemeka kwa ngerema, na kuweweseka, na kusema, "Najikhofia nafsi yangu, kuchezewa na mashetani, na kuniharibu akili yangu na kunizuga" (Kitabu cha maisha ya Nabii Muhamaad s.a, uk.17 kilichoandikwa na Sheiky A.Farsy).
KUFUATANA KITABU CHA MAISHA YA NABII MUHAMMAD, tunajifunza kuwa Muhammad kwa mara ya kwanza kabisa alipata utume wake pangoni baada ya NAFSI YAKE KUCHEZEWA NA MASHETANI.
MASWALI:
(i). Kama Jibril ndie alitumwa na Allah, na huyo Allah ni Mungu, kwanini Muhammad alisema kuwa nafsi yake imechezewa na MASHETANI baada ya kukutana na Jibril?
(ii). Kama Jibril alitoka kwa Allah, kwanini Muhammad alipo toka pangoni alisema kuwa Jibril AMEMZUGA AKILI YAKE?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW