Saturday, October 1, 2016

ALLAH SIO YEHOVA "YAHUH" ( يهوه ) MWENYEZI MUNGU (SEHEMU YA SITA)Je, Yehovah na Allah ni Miungu Tofauti!?

• Ukweli kuhusu Mungu anayeabudiwa na Waislam na Wakristo
• Je, Yehovah au Allah ndiye Mungu wa Wakristo?
• Je, ndiye Mungu wa Ibrahimu, Ismaili, Isaka, Yakobo, Yesu na Manabii
wote?

Yehova ni Jina la Mungu ambalo kwa Kiingereza anaitwa Jehovah na kwa Kiebrania anaitwa יהוה (YHVH) na kwa Kiarabu anaitwa (yahuh ) au ( يهوه ). ngoja niweke kwa urahisi ili wafuasi wa Muhmmad waelewe;

1. Kiebrania = יהוה (YHVH)
2. Kiingereza = Jehovah
3. Kiswahili = Yehova
4. Kiarabu = yahuh ( يهوه )

Kulingana na maelezo ya Biblia, Yehovah ni jina takatifu la Mwenyezi Mungu walilolitumia Wayahudi kwa mnasaba wa lugha yao ya Kiebrania. Aidha, Kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia, jina hilo Mungu alilifunua kwa Musa. Maandiko yafuatayo yanathibitisha ukweli huu:

"Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni Yehovah, mami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka na Yakobo kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVAH sikujulikana kwao". (Kutoka 6:2-3)
Kulingana na maandiko hayo juu, tunachojifunza hapa ni kwamba Yehovah ni Mwenyezi Mungu.


1. Mungu alivyojitambulisha kwa Nabii Musa.
Biblia inafundisha kuwa Mungu alijitambulisha kwa Musa na kwa Waisraeli wengine kwa majina ya "Yehovah" na "BWANA".

Kuhusu jina la Yehovah, andiko lifuatalo linathibitisha kama ifuatavyo:
"Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, Mimi ni Yehovah". (Kutoka 6:2).

Kuhusu BWANA, maandiko yafuatayo yanabainisha:
"Ilikuwa siku hiyo BWANA aliponena na Musa katika nchi ya Misri, BWANA akamwambia Musa, akasema, Mimi ni BWANA, mwambie Farao mfalme wa Misri maneno yote nikuambiayo". (Kutoka 6:28-29).


2. Mungu alivyojitambulisha kwa Mfalme Daudi:
Maandiko ya Biblia yanaonyesha pia kuwa Mungu alijifunua na kutambuliwa na Mfalmei Daudi kwa majina ya Yehovah, Yahu na BWANA.
Kuhusu jina Yehovah, Nabii Daudi baada ya Mungu kumfunulia, alitangaza kwa kusema:
"Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako Yehovah, ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote". (Zaburi 83:18)
Kuhusu jina Yahu, Nabii Daudi pia alifunuliwa na kusema:
"BWANA, Mungu wa majeshi, Ni nani aliye hodari kama Wewe, Ee Yahu?" (Zaburi 89:8) Ama kuhusu BWANA, Nabii Daudi vile vile alisema:
"Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, Na mfalme mkuu juu ya miungu yote". (Zaburi 95:3)


3. Mungu alivyojitambulisha kwa Nabii Isaya:
Kulingana na mafundisho ya Biblia, Mungu kupitia kinywa cha Nabii Isaya alijitambulisha kwa jina la BWANA.
Aidha, kwa upande mwingine, maandiko ya Biblia yanaonyesha kuwa Mungu pia alijifunua kwa Nabii Isaya kwa jina la BABA.
Kuhusu kujitambulisha kwa jina la BWANA, Mungu mwenyewe alisema:
"Mimi ni BWANA, ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu". (Isaya 42:8)

Ama kuhusu jina la BABA, Nabii Isaya alisema:
"Lakini sasa, Ee BWANA, Wewe U baba yetu, sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu, sisi sote tu kazi ya mikono yako". (Isaya 64:8)

Nakusihi ufanye utafiti wako mwenyewe na uone kama kuna sehemu yeyote ile Allah amejiita Yehova kwenye, Quran, kama ukikosa aya, basi elewa kuwa ALLAH SIO MUNGU WALA MWENYEZI MUNGU WALA MUNGU WA ADAM, AU IBRAHIM, AU ISAKA, AU YAKOBO AU DAUDI, NK, bali Allah ni Mpinga Mungu.

Nawakaribisha Waislamu wote kwa Mungu wa Kweli anaye itwa YEHOVA.

Mungu awabariki sana.

Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW