Tunaamini unapofuata kwa makini mada hii utatii neno la Mungu wa kweli, kuliishi, na kulitenda.
Mkristo wa kweli hatorudi katika ubishi wa ki dini pamoja na wapagani ambao ni miongoni mwa Anti-Kristo waitwao waislamu.
Mkristo wa kweli hatorudi katika ubishi wa ki dini pamoja na wapagani ambao ni miongoni mwa Anti-Kristo waitwao waislamu.
Huu ni utafiti wa ki maandiko tulioufanya tukilinganisha ujumbe wa Qur’an Tukufu pamoja na Biblia Takatifu pamoja na kwamba mimi nimeishi msikitini nikajaliwa neema kuujuwa ukweli. Karibu na twakutakieni usomaji mwema.
MWANZONI KABISA
Tunakusalimu tena katika jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo,
Ni kwa mara ingine Mungu wetu ambaye jina lake ni YEHOVA ametupa neema yake ili tuweze kuchangia pamoja haya maneno ya uzima yaani ‘UKWELI WA NENO LA MUNGU, BIBLIA’
Kwanza kabisa nataka niendelee kukujulisha kama hii wavuti yetu siyo ya kidini bali ni kwa ajili ya kuipiga tarumbeta ili wana wa Mungu wa pekee na wa kweli waweze kuikimbilia kwa mbali ibada kinyume na mapenzi ya Mungu!
Hatujali wewe wa ni dini gani? taifagani? au lugha gani? sisi tunachokifanya ni kujaribu kuyachnguza maandiko matakatifu pamoja na kugundua ukweli wake!
Bwana Mungu akubariki unapokuwa sehemu ya kuitafuta kweli.
JE, SISI NA WAISLAM TWAENDA NJIA MOJA?
Amosi 3:3
‘Je, Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?’
‘Je, Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?’
Yaani hata mtoto wa miaka mitano atakuletea jibu lisemalo APANA!!!
Sababu No.1
WAO NI DINI ILA SISI NI KANISAQr. 5 au surat Al Maida 2-3,
Enyi mlioamini! Msivunje hishima ya alama ya dini ya Mwenyezi Mungu wala mwezi mtakatifu, wala wanyama wanaopelekwa Makka kuchinjwa, wala vigwe vyao, wala wanaoelekea kwendea Nyumba Takatifu, wakitafuta fadhila na radhi za Mola wao mlezi. Namkishatoka Hija yenu basi windeni. Wala kuwachukia watu kwa kuwa walikuzuilieni kufika Msikiti mtakatifu kusikupelekeeni kuwafanyia uadui. Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.
Mmeharimishiwa nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na myama aliyechinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na aliyekufa kwa kunyongeka koo, na aliyekufa kwa kupigwa, na aliyekufa kwa kuanguka, na aliyekufa kwa kupigwa pembe, aliye liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu kula nyama aliyechinjiwa sanamu. Na ni haramu kupiga ramli. Hayo yote ni upotovu.Leo waliokufuru wamekata tamaa na DINI yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni msamehevu na Mwenye kurehemu.
Qr. 4 Au surat An Nisaai 171,
Enyi watu wa kitabu! Msipite kiasi katika DINI yenu, wala msiseme Mwenyezi Mungu ila kwa lililo kweli…..
Biblia inasemaje?Mathayo 16:16, 18,
Simoni Petro akasema akajibu akasema, Wewe ndiwe KRISTO, Mwana wa Mungu aliye hai.
Nami nakwambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.Matendo ya mitume 2:41, 47,
Naowaliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.Wakimsifu Mungu, na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha KANISA kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.
1Wakorintho 3:23, Nanyi ni WAKRISTO, na Kristo ni wa Mungu
Matendo ya itume 11:26, Hata alipokwisha kumwona akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa WAKRISTO kwanza hapo Antiokia.
Sababu NO.2 MUNGU MMOJA
Ukitazama kwa haraka haraka namna wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu wanavyolinganisha aya za Qurani na Biblia unaweza ukashawishika kuamini hicho wanachokifundisha, lakini ni vyema tukajifundisha kwa undani kadiri ya Qurani na Biblia na kisha tuone kama kuna ukweli juu ya hayo mafundisho yao, ya kusema Allah Sub-hana Wataala ndiye Yehova.tukumbuke kuwa Mungu tunayeabudu alitutahadhalisha sana Wakristo kwa kusema hivi.
Kutoka 20:1-3
Mungu akanena maneno haya yote akasema Mimi ni BWANA Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa usiwe na Miungu mingine ila mimi.
Kutoka 20:1-3
Mungu akanena maneno haya yote akasema Mimi ni BWANA Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa usiwe na Miungu mingine ila mimi.
Tahadhari hii Ya Mungu wetu ya kusema usiwe na Miungu inamaanisha kuwa Miungu mingine yenye kuabundiwa na watu ipo. Kwa sababu katika Biblia neno Mungu Kiebrania“Elohim” Kiyunani "Theos" limetanjwa mara 3979 lakini pia miungu ya uongo imetanjwa mara 271. Baadhi ya miungu hiyo ya uongo ni hii:
mungu Dargoni Waamuzi16:23
mungu Baal Wafalme 18:21
mungu mke wa Waefeso aitwae Artemi Matendo 19:24-28.
Aidha tusomapo Qurani pia imetaja miungu mbalimbali iliyokuwa inaabundiwa kule Makka nayo ni hii;
Qurani 53:19-20,23 Suratul An- Najm (Nyota).
mungu mke wa Waefeso aitwae Artemi Matendo 19:24-28.
Aidha tusomapo Qurani pia imetaja miungu mbalimbali iliyokuwa inaabundiwa kule Makka nayo ni hii;
Qurani 53:19-20,23 Suratul An- Najm (Nyota).
Je, mumewaona Lata na Uzza? Na Manata (mungu wenu) mwingine wa tatu (kuwa ndio waungu hao badala ya mwenyenzi mungu)? ayakuwa haya (majina ya Lata mungu mwanamke na Uzza mungu mwanamke mwenye enzi. Na Manata mungu mwanamke anayeneemesha ila ni majina tu mliowapa nyinyi na baba zenu…..
Hivyo basi tunaona kuwa miungu yenyewe kuabudiwa ni mingi na kila mwenye kuabudu humtegemea huyo mungu wake na kusema ni mmoja. Mfano waliyemuabudu Dagoni walisema ni mungu mmoja, waliyemwabudu Baali walisema ni mungu mmoja, waliyemwabudu Artemi walisema Artemi ndiye mungu mkuu. Kadharika Manabii.walimtumikia Mungu mmoja aitwaye Yehova, naye Muhammad alimwabudu mungu mmoja aitwaye Allah. Ninachotaka kukifundisha kwa jamii ijue je, huyo Allah ndiye Yehova?,
Nabii Musa alivyosema:
Kumbukumbu la Torati 6:4Sikiza ee Israeli; BWANA Mungu wetu BWANA ndiye mmoja.
Nabii Isaya alisema hivi
Isaya 45:18, 21,
Maana BWANA, aliyeumba mbingu, asema hivi, yeye ni Mungu,ndiye aliyeumba Dunia na kuifanya ….. si mimi BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi. Mungu mwenye haki, mwokozi hapana mwingine zaidi ya mimi.
Nabii Daudi Alisema:
Zaburi 86:10, Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu, wewe ndiwe mfanya miujiza, ndiwe Mungu peke yako.
Yesu alisema hivi:
Yohana 17:3, Na uzima wa milele ndio huu wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliye mtuma
Paulo naye Alisema hivi
1 Wakorintho 8:4
Basi kwa habari ya kuvila vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika ulimwengu, na yakuwa hakuna Mungu ila mmoja tu
.
Sababu NO.3
ALLAH WAO SIYE YEHOVA MUNGU


