SEHEMU YA KWANZA
Tunazidi kuchambua HOJA ZA MIHADHARA ya Kiislamu
LEO TUANGALIE SINAGOGI!!
Kwa miaka mingi afrika mashariki na kati kunakosemwa kiswahili kumetokea mafundisho ambayo ni mapotofu sana ya kukejeli, na lengo lao hasa ni kuangusha mwili wa Yesu kristo (kanisa) na mafundisho yake. Na kupitia mafundisho hayo wengi wameacha imani iliyo ya kweli nakufuata imani zingine ambazo mwisho wao ni mauti. Na hawa siyo wengine bali ni wahadhiri wakiislamu. Wao hudai kuwa wanafuata mafundisho ya Bwana Yesu. Unukuu aya hii mathayo 11:29-30 pale Yesu alisema jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo nanyi mtapa raha nafsini mwenu; kwa maana nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.
Pia wanasema Yesu aliingia kwenye sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake siku ya Sabato luka 4:16.kupitia kwa tendo hili la Yesu kwingia kwenye sinagogi , wahadhiri hawa wanadhai jambo ili linamfanya Yesu kuitwa muislamu. Tafadhali ndugu yangu ukitaka kujua ukweli fuatilia somo hili hadi tamati.. hii ni sehemu ya kwanza. Biblia ya Kiswahili katika maneno magumu imetaja kuwa Sinagogi ni msikiti wa Kiyahudu. hapa majamaa wanakesha!!
Historia ya sinagogi:
Ukitaka kujua mtu Fulani ni lazima uangazie mambo kadha wakadha ikiwemo historia yake, pasina historia ni vigumu watu kufahamu mambo yaliyofichika. Hivyo nimeonelea kuwa ni bora sana kuangazia historia ya sinagogi na chanzo chake. Jambo la msingi kwanza ni kujua maana ya sinagogi. Neno hili Sinagogi maana yake ni mahali pa watu kukutania. Sinagogi lilianzia pale wana wa Israeli walipokuwa utumwani kule Babeli kwa miaka sabini kulinga na unabii wa nabii Jeremia,jeremia 25:11-13.

baadaye nitaeleza tofauti ya Sinagogi na Hekalu.
Sababu ya wayahudi kuanzisha sinagogi ni hizi.
• kule utumwani hawengeweza kurudi kule Yerusalemu ambapo palikuwa na hekalu kwa minajili ya mambo ya ibaada. Kwa hivyo Wayahudi walitafuta jinzi ya kuendelesha ibaada na miandamo ya sikukuu zao.
• Kuendelesha utamaduni wao kama vile kutahiri mtoto wa kiume akiwa na siku nane kulingana na amri ya Mungu mwanzo 17:9-12
• Ili kuzingatia sheria za Mungu kufundishana habari za torati na manabii.
Uongozi
Sinagogi lilikuwa likianzishwa na wazee wapatao saba au kumu wa kiyahudi, kila sinagogi lilikuwa na viongozi wapatao wawili au zaidi. Na vyongozi hao huchaguliwa na wazee wa sinagogi. Katika karne ya agano jipya kulikuwepo masinagogi mengi sana yapatao 480 ambazo zilikuwa zikiingiwa na watu wa wamataifa mbalimbali ambao walikubali kufuata taratibu zote za dini ya kiyahudi.

Kazi ya sinagogi:
Malengo makubwa ya sinagogi yalikuwa kujikumbusha sheria na pia kuangalia utamaduni wao. Tusomapo Biblia na kuichunguza tunaona mambo yafuatayo;
Malaki 4:4
Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliomwamuru huko Horebu kwa ajili ya watu wangu Israeli wote naam, amri ya hukumu.
Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliomwamuru huko Horebu kwa ajili ya watu wangu Israeli wote naam, amri ya hukumu.
Mathayo 5:17
Yesu alifundisha hivi:- Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii la sikuja kutangua, bali kutimiliza
Yesu alifundisha hivi:- Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii la sikuja kutangua, bali kutimiliza
Hivyo basi kwa habari za torati na manabii wayahudi walikuwa wakifundisha watoto wao kwenye sinagogi. Matendo 15:21. kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.
.jpg)