Friday, April 1, 2016

URITHI WA UISLAM KUTOKA KWENYE DINI ZA KIPAGANI





(SEHEMU YA KWANZA)
Allah alitokea wapi?
Uislamu unajinadi kwamba Allah ndiye Mungu yuleyule aliyejishughulisha ya Wayahudi tokea nyakati za Ibrahimu katika Agano la Kale. Je, jambo hilo ni kweli?
Uislamu ulianza na Muhammad kwenye miaka 600 baada Kristo. Je, kabla yake imani za Waarabu zilikuwaje? Je, yako mambo yoyote kutoka kwenye imani hizo ambayo yaliingia kwenye Uislamu? Kwa maneno mengine, je, Uislamu hauna upagani ndani yake?
Fuatana nami kwenye makala haya marefu yanayochambua chimbuko la Uislamu ili tuweze kuona iwapo upo uhusiano wowote kati ya Uislamu na upagani uliokuwa ukitawala miongoni mwa jamii za Waarabu kabla ya kutokea kwa Muhammad?

Asili Ya Allah
Jamii za wanadamu KOTE duniani zimekuwa na kawaida ya kujiuliza ni wapi ulimwengu huu umetokea, nini maana ya maisha na wapi watu huenda baada ya kufa. Matokeo yake, kila jamii ilifikia kuamini kuwa kuna aliye na nguvu (au walio na nguvu) kuliko wanadamu wote ambao ndio wanapaswa kuabudiwa na kuombwa msaada pale matatizo yanapotokea.
Hawa wenye nguvu wakajulikana kwa majina mbalimbali kwenye jamii tofauti. Vilevile, kila jamii ilianzisha utaratibu maalum wa kuwasiliana na hawa wenye nguvu, yaani miungu.
Lakini jambo moja ni dhahiri, kwamba UKIACHA JAMII YA WAYAHUDI PEKE YAO, jamii zote za wanadamu zilizobakia duniani – iwe ni Afrika, Ulaya, Asia, n.k. - zimeanzia kwenye ibada za kipagani. Jamii hizi ziliabudu miungu mbalimbali. Na miungu hii iliwakilishwa na vitu kama vile milima, miti mikubwa, jua, mwezi, majoka makubwa, sanamu, wafalme, n.k. Kwa mfano, Warumi walikuwa na miungu kama vile artemi, jupiter, minerva, atlas, n.k. Tazama hapa. Wagiriki walikuwa na miungu kama vile chronos, dionysus, eros, ares, appolo, hermes, poseidon, n.k. Tazama hapa. Wahindi wana miungu kama vile durga, ganesha, garusha, brahma, n.k. Tazama hapa. Imani hizi za kipagani ziliweza hata kukua sana na kuenea maeneo mengi. Kwa mfano, imani ya ubudha ni imani ya kipagani lakini iliweza kuenea sehemu kubwa sana ya Asia – India, Japan, Sri Lanka, Uchina, n.k.
Kwa hiyo, jamii za Kiarabu, kama ilivyo kwa wanadamu wengine, vilevile hazikuwa tofauti. Jamii hizi nazo zilikuwa zina ibada zao za kipagani.
Waarabu walikuwa wakiabudu kile ambacho kinajulikana leo kama “star family”, au “familia ya nyota.” Tazama hapa. Inaitwa ‘familia ya nyota’ kwa sababu walichukulia miungu yao kwa tabia za kibinadamu. Mwezi ulichukuliwa kuwa ni mungu mwanamume na jua kama mke wa mwezi. Kisha hawa walizaa watoto. Kwa mfano, waliaminika kuwa walikuwa na mabinti watatu waliojulikana kwa majina ya al-lat, al-uzza na manat.
Ndiyo maana hata quran ikasema: Have you considered Al-Lat and Al- Uzzah, and another, the third (goddess) Manat? (Sura 53:19-20).
Yaani: Mmemwona Al-Lat na Al – Uzza, na mwingine, wa tatu (mungu mke) Manat?
Na hata Muhammad alikuwa akiabudu miungu hii kabla ya kuanzisha Uislamu. Tunasoma kutoka Hisham al-Kalbi, Kitab al-Asnam (Book of Idols), uk.17 kwamba:

'We have been told that the Apostle of Allah once mentioned al-Uzza saying, "I have offered a white sheep to al-'Uzza, while I was a follower of the religion of my people."
Yaani:
Tulishaambiwa kwamba Mtume wa Allah aliwahi kumtaja al-Uzza akisema, “Nilitoa kondoo mweupe kwa al-Uzza, wakati nilipokuwa nikifuata dini ya watu wangu.” Watu wake ni Waquresh.
Jina Allah linatokana na al-llah. Al ni kama neno la Kiingereza, yaani article ‘a’; na ilah ni mungu. Kwa hiyo,al-ilah maana yake ‘a god’ au tu mungu kwa Kiswahili – maana Kiswahili hakina neno linalofanana na ‘a’.
Kwa sababu lugha huenda ikibadilika, ndipo jina hili likafupishwa na akuwa ‘allah’. Ni kama unavyoona kwenye Kiswahili utasikia mtu akisema ‘mambo ndo ivo bwana.’ Kumbe ‘ndo ivo’ ni kifupi cha ‘ndiyo hivyo’. Huenda miaka hamsini au mia ijayo watu hawatajua kuwa kumbe asili ya ‘ndo ivo’ ni maneno ‘ndiyo hivyo.’
Sasa, allah alikuwa ni nani? Allah alikuwa ni mungu mwezi, ambaye tumesema mke wake alikuwa ni jua na watoto (mabinti zao) walikuwa ni al-lat, al-uzza na manat. Hawa ndio walikuwa wakichukuliwa kuwa ni miungu wakuu miongoni mwa mamia ya miungu iliyokuwa ikiabudiwa na Waarabu kabla ya Uislamu – kipindi ambacho Waislamu hukiita ‘Jahiliyah’.
Na jina hili ‘Allah’ ni jina la kiume (masculine); na ndiyo maana binti yake mmoja akaitwa ‘al-lat’, ambalo ni jina la kike (feminine). Ni kama unavyoona Francis na Fortunatus ni wanaume lakini Francisca na Fortunata ni wanawake – japo majina haya asili yake ni ileile. Ndivyo ilivyo kwaAllah na al- Lat. Yote ni jina lilelile, tofauti tu kwamba moja ni la kiume na jingine la kike.
Mojawapo ya jamii iliyokuwa ikimwabudu sana Allah ilikuwa ni jamii ya Waquresh, ambayo ndiyo jamii alikotokea Muhammad.
Watu wasioelewa wanadhani kuwa Allah alijulikana baada ya Muhammad kutokea. Na wengine nao watasema kuwa Allah alijulikana tangu wakati wa Ibrahimu kama anavyojulikana leo. Kama hilo lingekuwa ni kweli, inabidi wajiulize ilikuwaje Allah wa Ibrahimu akapotea hadi ikawa kwamba kuna Allah wa kipagani?
Mathalani, inafahamika wazi kwamba baba yake Muhammad hakuwa mwislamu bali alikuwa mpagani.
Sitashaangaa endapo baadhi ya Waislamu watasema kuwa baba wa Muhammad alikuwa mwislamu. Hata hivyo, huyu mtu alikufa kabla hata ya Muhammad kuzaliwa. Na je, Muhammad mwenyewe anasema nini kuhusiana na baba yake?
Tunasoma hivi:
Anas reported: Verily, a person said: Messenger of Allah, where is my father? He said: (He) is in the Fire. When he turned away, he (the Holy Prophet) called him and said:Verily my father and your father are in the Fire. (Sahih Muslim, Book 001, Number 0398).
Yaani:
Imeripotiwa na Anas: Hakika, mtu mmoja alisema: Mjumbe wa Allah, baba yangu yuko wapi? Akasema: Yuko motoni. Alipogeka kuondoka, (Mtume mtakatifu) akamwita na kusema: Hakika baba yangu na baba yako wako Motoni.
Na swali ambalo tungependa wajiulize ni kuwa, kwa nini baba yake Muhammad, ambaye alikuwa mpagani aliitwa ‘Abdullah’?
Na kwa kuwa ‘Abdullah’ maana yake ni ‘mtumwa wa Allah’, hii ni ishara ya wazi kwamba wapagani wa kipindi cha jahiliyah walikuwa wakimwabudu Allah hadi kufikia kuwapa watoto wao majina kwa heshima ya Allah – kama ambavyo Wayahudi nao walikuwa wakiwapa watoto wao majina kwa heshima ya Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo.
Kwa mfano:
Yoshua – Yahwe ni wokovu;
Yothamu – Yahwe ni mkamilifu;
Yehoahazi – Yahwe ameshikilia;
Hezekia – Yahwe ametia nguvu;
Elisha – Mungu ni wokovu, n.k.
Jibu liko wazi. Allah alikuwa ni mungu wa kipagani aliyeabudiwa kabla ya Uislamu kuja. Na mungu huyu alikuwa ni ‘mungu mwezi’, yaani ‘al-ilah’. Jina lake jingine aliitwa ‘hubal.’ Mungu huyu wa kipagani aliabudiwa kote mashariki ya kati; wala si kwa Waarabu peke yake.
Hili ni jambo ambalo limeshathibitishwa tena na tena na wanaakiolojia – ambao hufukua masalia ya vitu vya kale – hawa wameshafukua vitu vingi sana ambavyo vinaonyesha jinsi kuabudu mwezi na jua na nyota kulivyokuwa kumeshamiri sana katika eneo la mashariki ya kati.
Na ndiyo maana baba yake Muhammad, yaani Abdullah, alikoswakoswa kuchinjwa na babu wa Muhammad, yaani Abdul Muttalib. Abdul Muttalib alitaka kumchinja mwanawe huyo kama sadaka kwa Allah. Lakini mjomba wake Abdullah akamwokoa na hatimaye walichinjwa ngamia 100 badala yake. Na ifahamike kwamba machinjo hayo yalifanyikia kwenye kaaba (hili tutaliangalia huko mbeleni).
Tunaambiwa kwamba:
An arrow showed that it was 'Abdullah to be sacrificed. 'Abdul-Muttalib then took the boy to Al-Ka'bah with a razor to slaughter the boy. Quraish, his uncles from Makhzum tribe and his brother Abu Talib, however, tried to dissuade him. They suggested that he summon a she-diviner. She ordered that the divination arrows should be drawn with respect to 'Abdullah as well as ten camels. … the number of the camels (finally) amounted to one hundred. (Ibn Hisham 1/151-155; Rahmat-ul-lil'alameen 2/89, 90).
Maana yake:
Mshale ulionyesha kwamba Abdullah ndiye aliyetakiwa kutolewa kafara. Kwa hiyo, Abdul Muttalib alimchukua yule kijana hadi kwenye Al-Kaaba pamoja na wembe kwa ajili ya kumchinja. Quraish, mjomba wake kutoka kabila la Makhzum na kaka yake Abu Talib, hata hivyo, walijaribu kugeuza mawazo yake. Walipendekeza kwamba amwite mwaguzi wa kike. Huyo aliagiza mishale ya uaguzi ichorwe baina ya Abdullah na ngamia kumi … hatimaye idadi ya ngamia ikafikia mia moja.
Ndiyo maana Mungu wa Biblia alikuwa akiwaonya sana wana wa Israeli juu ya tabia za kipagani za jamii zilizowazunguka kuhusiana na masuala ya kuabudu familia ya nyota au jeshi la mbinguni. Kwa mfano, anasema:
….. tena usije ukainua macho yako hata mbinguni, na ulionapo jua, na mwezi, na nyota, jeshi la mbinguni lote pia, ukashawishiwa na kuviabudu, na kuvitumikia, ambavyo Bwana, Mungu wako amewagawanyia watu wote chini ya mbingu zote. (Kumbukumbu la Torati 4:19).

Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na Bwana, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa Bwana, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake, ….. naye amekwenda kutumikia miungu mingine na kuiabudu, au jua, au mwezi, au vilivyo katika jeshi la mbinguni vyo vyote, nisivyoagiza mimi (Kumbukumbu la Torati 17:2-3).

Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. (2 Wafalme 21:3).

Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. (2 Wafalme 21:5).

Akawaondosha wale makuhuni walioabudu sanamu, ambao wafalme wa Yuda waliwaweka ili kufukiza uvumba katika mahali pa juu, ndani ya miji ya Yuda, na katika kila mahali, pande zote za Yerusalemu; na hao pia waliomfukizia uvumba Baali, na jua, na mwezi, na sayari, na jeshi lote la mbinguni. (2 Wafalme 23:5).
… nao wataitawanya mbele ya jua, na mwezi, na jeshi lote la mbinguni, walivyovipenda, na kuvitumikia, na kuandamana navyo, na kuvitafuta, na kuviabudu haitakusanywa pamoja tena, wala kuzikwa; itakuwa ni samadi juu ya uso wa nchi. (Yeremia 8:2).
…. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa. (Yeremia 19:13).

…. na wale walisujudiao jeshi la mbinguni juu ya dari za nyumba; na hao waabuduo, waapao kwa Bwana na kuapa pia kwa Malkamu (Zefania 1:5).
...............................................
Katika mwaka 570 BK, mwaka uleule ambao Muhammad alizaliwa, alikuwapo mtawala mmoja wa dola ya Aksum ya Ethiopia ambaye alikaa Yemen. Huyu aliitwa Abrahah al- Ashram. Inaelezwa kwamba alikuwa na wivu na mji wa Makka kwa jinsi ambavyo watu wengi walikuwa wakienda kuhiji (yaani hija ya kipagani), hivyo na yeye naye akajenga kanisa kubwa kule Sanaa, Yemen akitarajia kuvuta watu wengi, jambo ambalo halikutokea.
Matokeo yake, aliamua kwenda kuvamia Makka kwa lengo la kuiharibu kaaba. Alisafiri na watu wake wengi juu ya kundi kubwa la tembo - ndiyo maana hata mwaka ule ukajulikana kama mwaka wa tembo.
Koo za Kiquresh ziliungana ili kujaribu kuikoa kaaba. Abdul Mutaleb (babu yake Muhammad) aliwaambia watu wakimbilie kujificha milimani wakati yeye na baadhi ya watu walibakia karibu na kaaba.
Lakini kwa sababu ya ukubwa na nguvu ya jeshi la yule Abrahah, Abdul Mutaleb alisema:

"The Owner of this House is its Defender, and I am sure He will save it from the attack of the adversaries and will not dishonor the servants of His House."
Yaani:
Mmiliki wa nyumba hii ndiye atakayekuwa Mlinzi wake, na nina uhakika ataiponya dhidi ya kushambuliwa na maadui na hawatawafedhehesha watumishi wa nyumba yake."
Mapokeo yanasema kwamba wakati Abrahah anasonga mbele kuiendea kaaba, lilitokea kundi kubwa la ndege ambao walianza kumdondoshea mawe kama mvua hadi wakamjeruhi. Hivyo, azma yake ya kuiharibu kaaba haikufanikiwa, badala yake akarudi kwake akiwa ameumizwa.
Sasa, swali ni kuwa, kama wakati ule Muhammad alikuwa bado kichanga, na hivyo Uislamu ulikuwa haujaanza; na pale kwenye kaaba inajulikana kwamba kulikuwa na mamia ya miungu ya kipagani; je, Mmiliki wa Nyumba anayetajwa na Abdul Mutaleb ni nani?
Ni wazi kwamba huyu ni mungu wa kipagani, yaani allah aliyekuwa akiabudiwa na kutumikiwa na Abdul Mutaleb, yaani mungu mwezi.
Na swali kubwa zaidi ni kuwa, Quran inasema katika sura Al-Fil (au Tembo) 105:1-5:

"Have you not seen how your Lord dealt with the owners of the Elephant? Did He not make their treacherous plan go astray? And He sent against them birds in flocks, striking them with stones of baked clay, so He rendered them like straw eaten up."

Yaani:

Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo? Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi, Wakiwatupia mawe ya udongo wa Motoni, Akawafanya kama majani yaliyo liwa!
Swali ni kuwa:
Mambo haya yalitokea wakati Uislamu haupo, bali ulikuwa ni wakati wa upagani. Mtumishi wa mungu wa kipagani Abdul Mutaleb alisema kwamba Mmiliki wa Nyumba ile (kaaba) angeitetea.
Je, Mmiliki wa nyumba aliyetajwa na Abdul Mutaleb alikuwa yupi na Mola wako anayetajwa na Quran kwenye sura hii ni yupi? Au tuseme kulikuwa na miungu miwili iliyoshirikiana kumpiga mawe Abrahah na tembo wake?
Abdul Mutaleb hakumjua Allah wa Muhammad, kwa hiyo kwa namna yoyote ile hangeweza kumtaja huyo (kama kweli Allah wa Muhammad ni tofauti na wa Abdul Mutaleb).
Mazingira yote yanaonyesha kwamba mungu mwezi, aliyeabudiwa na Abdul Mutaleb ndiye aliyeilinda kaaba dhidi ya tembo wa Abrahah. Kwa hiyo, aya hii ya Quran haina uwezo wa kujinadi kwamba inamtaja mungu tofauti na huyo!!

Hitimisho

Kama wewe ni Mwislamu, je, haujiulizi inakuwaje kwamba mwezi ndio wenye usemi juu ya mambo mengi ya muhimu kwenu Waislamu?
Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uanze?
Kwa nini ni lazima mwezi uonekane ndipo mfungo uishe?
Kwa nini alama kuu juu ya kila msikiti ni nusu mwezi na nyota?
Ni nini asili ya vitu hivyo?
Mungu awabariki sana.
By permission
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 1, 2016

IMAM WA MSIKITI AOKOLEWA NA YESU




Zak Gariba ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia yao. Kwa sababu ya kulitaja jina la Yesu msikitini, Zak Gariba, ambaye alikuwa ni imam alitupwa si tu nje ya msikiti, bali pia nje ya familia yake. Alikataliwa na kujikuta hana tena ndugu; na akapoteza kila kitu. Matokeo yake alifika mahali ambapo aliamua kujiua. Lakini Yesu Kristo mwenyewe alienda kugonga mlango wa nyumba yake na akayabadili kabisa maisha yake kutoka mautini na kumwingiza uzimani.

Kwa maneno yake mwenyewe, Zak anasema:

“Nilizaliwa katika familia ya Kiislamu na kulelewa katika Uislamu na wazazi wangu walinichagua niweze kupata mafunzo ili nije kuwa imam. Nilienda kwenye shule na nikajifunza pia lugha na utamaduni wa Kiarabu.

Nilisomea masomo ya kuwa imam. Baadaye nilienda Nigeria na nikawa imam wa msikiti mmoja. Nilipenda kile nilichokuwa nakifanya.

Kuna wakati nilikutana na Wakristo fulani marafiki zangu ambao walikuja na Biblia zao na tukaanza kubishana, huku nikiwaambia kuwa Quran ina nguvu kuliko Biblia. Tuliendelea kubishana na ikafika mahali nikawapiga. Nikafikia pia wakati ambao nikawa nimewachoka; nikawa nataka waende zao, maana wao walikuwa ni  watu wakimya. Nikawa natafuta namna ya kuwaondoa.

Baadaye waliniomba kama naweza kuwabeba kwa gari hadi mahali fulani ambako kulikuwa na mkutano wa injili. Nikasema, kama hilo ndilo mnalotaka, nitawapeleka – maana niliona hiyo ni njia itakayonisaidia kuachana nao.

Mama mwenye nyumba yangu alikuwa na msichana mdogo ambaye, tangu kuzaliwa,  alikuwa amepooza kuanzia kiunoni kuja chini. Waliniomba nimbebe ili kumpeleka kwenye mkutano. Nilimbeba hadi kwenye huo mkutano uliokuwa unafanyika kwenye uwanja mkubwa.

Niliegesha gari nyuma ya uwanja na kulikuwa na spika kubwa imeelekea kulekule; na kuna mtu akawa anasema Yesu, Yesu!

Baada ya kuegesha gari, watu wengine wenye magari nao walikuja. Nikajikuta nimezingirwa na magari mengine kiasi kwamba haikuwezekana kutoka tena.

Msichana yule akataka kutoka kwenye gari. Ikabidi nimbeba mikononi ili nimpeleke kwenye benchi mojawapo. Na yule mtu wa kwenye spika naye aliendelea tu kusema Yesu, Yesu. Na mimi nikawa ninatamani kufunga masikio yangu ili nisisikie lakini siwezi, maana nimembeba huyu msichana.

Lakini wakati kuo kitu cha ajabu kilitokea. Mguu wa huyu msichana ulisogea kwa namna isiyo ya kawaida. Nikawaza, ‘Ha! Nini hiki tena? Bila shaka hii ni voodoo! Huu utakuwa ni uchawi tu!’

Na kadiri yule msemaji alivyoendelea kusema Yesu, Yesu, miguu ya msichana huyu iliendelea kusogea zaidi na zaidi. Nikawa kama nimechanganyikiwa. Kisha huyu msichana akasema, ‘Nataka kutembea.’

Nikamwambia, ‘Hutaweza.’

Matokeo yake, aliniuma. Ninalo kovu hapa(kwenye mkono). Ikabidi nimwachie hadi chini. Na mbele ya macho yangu, nilimwona msichana huyu akitembea!

Nami nikawa najiuliza, ‘Inawezekanaje mtu mmoja ataje jina la Yesu na mtu mwingine apone kabisa? Nikaanza kuwaza kuwa, ni lazima kuna kitu hapa kwenye kitendo tu cha kutaja jina hili la Yesu.

Baadaye nilirudi nyumbani na jioni ile, kama kawaida, nilienda msikitini. Nilipokuwa msikitini nikiongoza swala, sijui ni kwa vipi, lakini kwa namna nisiyoelewa, ghafla maneno yalinitoka mdomoni ambayo hata sijui yalitoka wapi. Badala ya kusema,  Muhammad-sallal-laahu-alaihi-wasallam, nilijikuta tu nasema kwenye spika za msikitini pale, ‘Yesu Kristo wa Nazareti!’ Katikati ya msikiti! Katikati ya waumini wengi! Nilichanganyikiwa. Matokeo yake waumini wakanitoa nje. Walitaka hata kuniua!

Na huo ukawa ni mwanzo wa matatizo yangu.

Baada ya hapo, kaka yangu mkubwa alinisaidia kuja Kanada kusoma. Nilipokuja huku, niliazimia kuwa nitaishi maisha ya kipagani kabisa. Sikutaka kuwa Mkristo wala kuwa Mwislamu!

Lakini nakumbuka tarehe 3 Januari 1997 nilikuwa chumbani kwangu na nilikuwa nimepanga kujiua. Nilikuwa nimefika mwisho wa maisha yangu kabisa. Wazazi wangu walishanikataa; na hata walishafanya msiba kwa ajili yangu. Kila kitu kilikuwa hovyo kwangu. Nilikuwa nimeshaandaa vidonge na kila kitu.

Ilipofika saa 3:00 asubuhi nilisikia mlango ukigongwa. Nilipandwa na hasira sana. Nikaenda kuangalia, lakini hakukuwa na mtu. Nikawaza, hii ni ajabu! Yaani Kanada? Mbona hapa watu wana simu wanaweza kukupigia kabla ya kuja kwako!

Nikarudi ndani. Lakini nikasikia mtu anagonga tena. Nilipofungua, sikuona mtu tena. Nikafunga mlango na kuwaza, ‘Labda atagonga tena mara ya tatu.’ Kwa hiyo, nikanyagakanyaga sakafu kama vile natembea – ili kwamba huyo mtu afikiri kuwa nimeenda ndani. Lakini nikawa nimesimama palepale karibu na mlango.

Mara kweli nikasikia amegonga tena. Nilipofungua, hakukuwa na mtu; lakini nikasikia sauti ambayo sijawahi kuisikia maishani mwangu. Ilisema, “Mama na baba yako wamekuacha,  lakini mimi nitakuwa pamoja nawe.”

Nikatazama huku na huku na kuwaza, ‘Yaani sasa nimeanza hata kusikia sauti!’

‘Wewe ni nani? Wewe ni nani?’ niliuliza.

Sauti ile ikasema, ‘Mimi ni Yesu. Sasa nakuita kufanya jambo jingine.’

Nikasema, ‘Hebu ngoja kidogo. Nilitaja jina la Yesu wa Nazareti msikitini matokeo yake nikaingia kwenye matatizo makubwa kiasi hiki ...! Sitaki kujihusisha na chochote kinachohusiana na wewe!’

Akasema, “Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Niko tayari kukusaidia.’

Na huo ndio ukawa mwanzo wa maisha yangu.

****************

Zak Gariba, kwa neema ya Mungu, pamoja na kukataliwa na ndugu na kila mtu, alimpata Mungu wa kweli. Hivi sasa yeye ni mchungaji. Unaweza kusoma zaidi habari za kanisa lake kwenye www.orilliajubileecc.org.

Yesu yuko tayari kukuokoa na wewe sasa. Usichelewe kumwita na kumkaribisha moyoni mwako. Kanuni ya msingi ya wokovu ni kwa mtu kuamua moyoni mwake na kuchukua hatua ya kusema, ‘Bwana Yesu karibu moyoni mwangu ili unipe uzima wako wa milele.’ Kuna watu wachache tu ambao Bwana Yesu, kwa kuamua mwenyewe, huwaendea uso kwa uso na kuwatoa kwenye upotevu na kuwaingiza uzimani. Kwa hiyo, usije ukasema, nitangoja hadi Yesu atakapokuja kugonga mlango wa nyumba yangu kama alivyofanya kwa Zak Gariba ndipo nitaokoka. Anaweza asije kabisa hadi mwisho kwa namna hiyo; maana hiyo si kanuni ya msingi ya wokovu. Lakini usiku na mchana anagonga kwenye moyo wako kwa njia ya Roho Mtakatifu ambaye husema na dhamiri zetu muda wote.

Uzima wa milele haupatikani kwenye dini yoyote – iwe ya Kikristo au isiyo ya Kikristo. Uzima wa milele unapatikana kwa Yesu Kristo pekee. Yesu hakuja kuokoa Wakristo – maana wakati alipokuja duniani hadi anaondoka, wala hakukuwa na Ukristo. Yesu alikuja kwa ajili ya dhambi za wanadamu wote. Yeye ni Mwokozi wa ulimwengu wote – si Mwokozi wa Wakristo.

Tatizo la dhambi ni tatizo la wanadamu wote. Na hilo ndilo tatizo pekee linalomfanya mwanadamu yeyote aikose mbingu na kuingia jehanamu ya milele. Lakini tumepewa njia rahisi na ya uhakika ya kupona na kuokoka; nayo ni kumwamini Yesu ambaye alikufa ili awe sadaka kwa ajili ya dhambi zetu. Hii ni kwa sababu sisi hatuna kabisa uwezo wa kuishi maisha matakatifu kwa nguvu zetu wenyewe kiasi cha kufikia utakatifu wa Mungu mwenyewe. Maana bila utakatifu, HAKUNA yeyote atakayeingia mbinguni. Na ni mwanadamu gani basi anayeweza kusema kuwa yeye ana maisha matakatifu? Bila shaka hakuna hata mmoja.

Ndiyo maana Yesu aliye Mungu, alikuja kuishi maisha ya kibinadamu, lakini kwa ukamilifu wa kiungu ili kwamba, kwa kule tu kumwamini, sisi si tu tunahesabiwa haki ya kuwa wana wa Mungu, lakini pia tunapewa neema ya kuishi maisha matakatifu.

Amua leo!

ALIYEKUFA SIKU YA BIRTHDAY YAKE NA KUFUFUKA ASHUHUDIA KANISANI

Waumini waliofika katika ibada ya shukrani iliyoandaliwa na kanisa la Glory of christ ministries international maeneo ya Tottenham jijini London jumapili iliyopita wameweza kusikia ushuhuda kutoka kwa mchungaji Catherine Mganga ambaye aliwahi kufariki kwa muda wa masaa mawili na kuchukuliwa mbinguni nakuonyeshwa maeneo mbalimbali na kurudishwa tena duniani

akishuhudia mbele ya waumini kanisani hapo mchungaji Catherine amesema mnamo mwaka 1975 wakati anaadhimisha siku ya kuzaliwa kwake(Birthday) akiwa na dada yake pamoja na ndugu jamaa na marafiki walikuwa wanasifu na kuabudu mara alijikuta akiangalia angani na kuona malaika akishuka kwenye kaa la moto,akiwa anapaa aliona mwili wake mwingine ukiwa bado sakafuni, anasema alipofika mbinguni alichukuliwa na malaika hadi sehemu ambayo watu duniani wakiomba maombi yao yanazuiwa na ibilisi, anasema kuna giza kuu
Mchungaji Grace Gwajima akifafanua maana ya ibada ya shukrani kanisani hapo

Waumini wakimsikiliza mchungaji Grace Gwajima

amesema mara baada ya kutoka hapo malaika akawa anamchukua kumpeleka jehanamu,amesema akawa anakataa kwenda akijua malaika anakwenda kumuacha huko pia kwasababu ya giza lilivyokuwa akazidi kuogopa lakini malaika akamwambia twende ukaone ili upate kuwashuhudia watu duniani,amesema alianza kulia na kumuomba malaika kurudi sehemu ambayo iliwafanya waumini waliokuwepo kanisani hapo kutaka kusikia kilichoendelea kutokana na kilio chake.
Mchungaji Grace akimkaribisha mchungaji Catherine kwa ushuhuda

Mchungaji Catherine Mganga akishuhudia

pia waumini waliweza kusikia shuhuda kutoka kwa watu wengine akiwemo mama Melisa ambaye alishuhudia juu ya binti yake huyo mwenye miaka saba kwamba mwaka jana alikuwa anafanya maombi kwamba mama anunue nyumba mpya,hata akiwa anajiandaa kwenda shule asubuhi maombi ni hayohayo Mungu amwezeshe mama yake anunue nyumba mpya na kweli Mungu akafanya miujiza  mama yake akanunua nyumba mpya,lakini mambo yakabidilika gafla kwa Melisa amesema akaanza kupata malalamiko kutoka shuleni kwamba Melisa kamchapa kibao mwalimu wake,ni mbishi pia kuna wakati anabadilika kabisa muonekano wake ukimwangalia,kwa mujibu wa mama yake anasema hakuwa akiamini maneno yote kwakuwa binti yake hana tabia hizo,ndipo uongozi wa shule walipomshauri kumpeleka hospitalini kwa uchunguzi zaidi, jibu alilopewa ni kwamba inawezekana ni uchovu kwahiyo anahitaji muda wa kutosha kupumzika kitu ambacho mama huyo alikipinga


Mama Melisa akiwa na Melisa akitoa ushuhuda ambapo pia walimaliza kwa kuimba wimbo

amesema alimhamisha shule lakini kilichotokea huko pia hakuamini baada ya kusikia mwanae amemkwangua mwalimu pia ameangusha kabati la vitabu kitu ambacho hata walimu wa shule hiyo hawakuamini kwamba ni Melisa aliyefanya yote hayo,lakini siku moja akiwa darasani peke yake alipiga kelele akipinga jambo "no noooooooooooo" mwalimu wake alipomtazama alimuona kakaa peke yake alipomuuliza kulikoni hakujibu, ndipo mama yake akajua kuna kitu kinaendelea kwakuwa hata binti yake hakuwa akipenda kuingia chumbani kwake kama ilivyokuwa zamani kisa kikiwa ni maombi ambayo alikuwa akiyafanya ndipo rafiki yake na mama melisa alipomchukua kumpeleka kwa mchungaji Grace Gwajima lakini kabla ya kuondoka nyumbani Melisa alikuwa hawezi kumtazama mama yake machoni alikuwa kama anayeona aibu, baada ya maombi Melisa akabadilika na kuwa kama awali

Ndipo mama yake alipomuuliza visa vyote vilivyotokea Melisa akamwambia mama yake kuwa kuna sauti ilikuwa ikimwamuru kufanya hivyo hata kuwapiga wenzake ikiwa pamoja na mwalimu,hata siku alipopiga kelele darasani ilikuwa inamlazimisha kufanya tukio ambalo yeye anasema alikuwa analipinga kukawa na mtu ambaye anamtisha ila watu wengine walikuwa hawawezi kumuona, baada ya maombi anasema huyo mtu pamoja na sauti haijarudi tena na amesharudi katika hali yake ya maombi
Watoto nao walisimama na kuzungumza mistali mbalimbali ya Biblia
Baadhi ya wasumini waliokuwepo ibadani

jumapili hiyo kulikuwa na wengi ambao walishuhudia shuhuda zilizowagusa wengi,Gospel kitaa inaahidi kukuletea shuhuda zote ikiwa pamoja kumalizia shuhuda ya Mchungaji Catherine Mganga ambaye kwasasa amejiunga rasmi na kanisa hilo ambapo jumapili ijayo atakuwa kanisani hapo kumalizia ushuhuda wake ikiwa ni pamoja na kuhubiri wakiwa pamoja na mchungaji Grace Gwajima
waumini wamekuwa wakiongezeka katika kanisa hilo kutokana navile Mungu anatenda miujiza na kuwafungua watu wenye matatizo mbalimbali ikiwa ni miezi mitano tangu kuanza kwa huduma hiyo. ambapo ibada wanafanyia katika ukumbi wa shule ya sekondari Peak view huko Tottenham,Langham Road, N15 3RB
moja ya jengo la shule hiyo ambapo ibada zinafanyika

Thursday, March 31, 2016

SHEIKH ALHAJI RASHID TATASHAJARA ABUBAKAR WA MSIKITI WA MTAA WA MWANZA ILALA DAR ES SALAAM AOKOKA






1. AKIRI KULA NYAMA ZA WATU
2. AKIRI KUNYWA DAMU ZA WATU
3. AKIRI KUMEZA MAJINI 360
4. ASEMA UISLAM NI DINI YA WACHAWI
Ndugu msomaji,
Soma huu ushuhuda wa kusisimua kutoka kwa Sheikh Alhaji Rashid Tatashajara Abubakar aliye kunywa damu za watu, kuhamisha nyota za watu, na kumeza majini 360.
Mwenyekiti wa waislamu waliookoka, Afrika Mashariki na Kati!
Alitokea kwenye familia ya kichawi, mama yake alijiita ni Mungu na kufanya miujiza mbalimbali ikiwemo ya kunyesha mvua. Sheikh Alhaji Rashid Tatashajara Abubakar, aliwahi kufanya shughuli za kisheikh katika msikiti wa Ilala mtaa wa Mwanza ambapo pia alikua mwanafunzi wa sheikh Yahaya Hussein ambaye ni marehemu kwa sasa.
Alianza kujifunza madrasa, akapanda vyeo na kusomea vyuo vya kichawi baada ya kuhitimu majaribio mbalimbali ikiwemo kufukua makaburi, kunywa damu za watu, kuhamisha nyota za watu, na kumeza majini 360 na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mkuu wa wachawi Afrika mashariki na kati!
Anasema katika mambo hayo yote, alikua akitumwa kushambulia watumishi wa Mungu mbalimbali, aliwahi kujaribu kwa Moses Kulola, Emmanuel Lazaro na Askofu Mwanisongole. Lakini alishindwa na kupata mieleka iliyompelekea kuumwa sana.
Akielezea ushuhuda wake kwa ufupi, Jinsi alivyompokea Bwana Yesu, ilikuwa sababu ya mke wake wa pili kupita kwenye mkutano wa Injili na kuponywa tumbo lililomsumbua kwa muda mrefu bila mafanikio ya kupona “mke wangu alikuwa akirudi nyumbani na kuimba nyimbo za makafiri, baadaye anaenda kanisani, sasa adhabu ya mtu anayekiuka sheria ni viboko 40, nilipotaka kumchapa mkono ukaganda, ndio mke wangu akasema piga magoti chini, akaniombea na mkono ukarudi mahala pake, baada ya hapo mengi yalitokea kukatisha story Mungu alianza kunifundisha na kunitumia”
“Siku Moja mtaa wa Salender Bridge kama mliwahi kusikia kisa cha dada aliyeota manyoya, alifikishwa kwangu nikamuombea kwa Jina la Yesu naye akapokea uponyaji. Kwa sasa yuko Marekani! nimemuona Mungu kwa jinsi ya tofauti kule nilikotoka nilikua namtumikia shetani, kwa sasa namtumikia Bwana Yesu, na kila ulimi utakiri kwamba Yesu ndiye Mungu”
Alhaji Rashid Abubakary kwa sasa ni mwenyekiti wa waislamu waliookoka Afrika mashariki na kati. Mungu amekua akimtumia kwa jinsi ya tofauti na amealikwa makanisa mbalimbali na kueleza shuhuda nyingi ambazo Bwana Yesu amefanya na kufanya kwenye maisha ya watu wengine. Ameonekana kwenye Televisheni ya kikristo ATN, ushuhuda huu kwa ufupi ameutoa tarehe 26 Agosti 2011, Kanisa la City Christian Centre.
By permission
Max Shimba Ministries Org

ABUU MTOTO WA SHEKHE "MUARABU" AKATA SHAURI NA KUMPOKEA YESU

Abuu kwenye ubatizo wa maji mengi chini ya kanisa la EAGT Mito ya Baraka, Dar es Salaam



























1. ABATIZWA NA SASA ANAITWA BOAZ
2. BABA YAKE ANAYEISHI OMAN AKIRI KUWA MUNGU WA "ABUU" HAKIKA NDIE MUNGU MKUU
3. ABUU SASA ANAMTUMIKIA YESU
Ndugu msomaji,
Bwana Yesu apewe sifa,
Haya msomaji wetu karibu katika kipengele chetu maalumu ''USHUHUDA'' ambacho kinakujia kila siku kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutokea lakini yawezekana hauijui pia yawezekana ilitokea ukawa unaijua lakini labda umesaihau.
Abuu Levy au waweza kumuita kwa jina la Boaz kama wengi walivyomzoea, ni jina ambalo amelipata baada ya ubatizo. Historia yake inarejea kwenye Uislamu, ambako ndipo alilpotokea, asili yake akiwa Muarabu. Baba yake mzazi anaishi Oman hadi hivi sasa.
Kwa taarifa yako, licha ya kukulia kwenye famlia ya usilamu, lakini hakuwai si tu kwenda msikitini, bali pia hata mazingira ya ndani ya msikiti anayafahamu yalivyo. Neema imetokana pale alipolelewa na mama yake mkubwa ambaye ni "mlokole".
Alipotimiza umri wa miaka kumi, Abuu alikata shauri na kuokoka. Lakini pamoja na baba yake mzazi kuwa Shekhe wa imani kali ya Kiislam, hakuleta kipingamizi chochote zaidi ya kumsihi tu kuwa asimuache Mungu, yaani Yesu Kristo. Hii ni tofauti na wazazi wengine wa Kiislam ambapo huleta vita kwa mwanao na hata kutishia kifo.
Pamoja na kupewa baraka na baba yake mzazi ambaye ni Muislam mwenye siasa kali, bado hali haikuwa nyepesi kwa baadhi ya ndugu zake, kwani Abuu amepitia magumu mengi, kuotka ndugu zake ambao takribani wote ni Waislam kwa kumtishia maisha yake na kusema maneno makali yenye laana kwasabu ya kubadili dini na kuwa Mkristo. Hata hivyo Abuu alisimama ndani ya Yesu na hakukuwa na kurudi nyuma. Abuu sasa anamtumikia Yesu kwa kuimba Nyimbo za Injili. Tumeweka linkhttps://www.youtube.com/watch?v=sFu6socEVMQ ya nyimbo zake. Tafadhali nunua CD'S/DVDS zake ili kuendelea kuimarisha kazi yake kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Abuu, mwenye umri wa miaka 24 kwa sasa ni mwimbaji wa nyimbo za injili kwa muda wa miaka nane huku akiwa na album tatu hadi sasa, kati yake mbili zikiwa madukani tayari.
Mungu huandaa na kubadilisha watu wake kwa njia mbalimbali, maana ametujua tangia hatujazaliwa. Naye Abuu yuko kwenye kazi/huduma ya Mungu. Yuko katika utumishi wa Yehova.
Mungu akubariki sana msomaji wetu, tuendelee kuitangaza Injili ya Yesu Kristo kwa Mataifa Yote.
Mungu anawapenda wote na tusikate tamaa hata tunapo kuwa katika magumu, mateso, Yesu bado anatupenda na yupo pamoja nasi kila siku.
Mungu awabariki sana.
By permission
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.
April 1, 2016








Monday, March 28, 2016

Nini kitaingia PEPONI: Roho/Nafsi au Mwili au zote mbili?

UTATA MKUMBWA NDANI YA KORAN
Nini kitaingia PEPONI: Roho/Nafsi au Mwili au zote mbili?
Somo letu la leo ni la swali kwa Allah ambaye ameshindwa kujieleza, kuwa ni kipi kinaingia Peponi kati ya Roho/Nafsi au Mwili?
Koran inadai kuwa, baada ya ufufuo, ni mwili (baada ya kuungana na roho?) Ambayo inaingia peponi. Haya madai yamewekewa mkazo katika Koran. Angalia mistari ifuatayo 13:05, 17:98-99, 20:55, 34:7, 75:3-4.
Hata hivyo mistari ya 27-30 kwenye Sura 89 inapinga aya zilizo pita kwa kusema kuwa ni nafsi (Nafs) tu ambayo inaingia Peponi!
Quran 17:99. Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini madhaalimu hawataki ila ukafiri.
Quran 75:3. Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? 4. Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
Aya hizo hapo juu, zinadai kuwa Nafsi na Mwili vitaungana na kuingia Peponi, hayo ni maneno ya Allah kama alivyo yashusha kupitia Quran yake. Lakini Allah huyohuyo anabadilika na kusema kuwa Nafsi ndio itaingia Peponi. Hebu soma aya zifuatazo.
Quran 89 27. Ewe nafsi iliyo tua! 28. Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha.
Katika aya hapo juu, Allah anaiamuru Nafsi irejee kwake. Sasa ni ipi kati ya Nafsi na Mwili vitaingia Peponi? Utata huu ni Msiba Mkubwa kwa Allah ambaye hafahamu nini kati ya Nafsi na Mwili vitaingia Peponi.

UTATA NDANI YA QURAN. "AYA ZA QURAN ZAPINGANA"



Ndugu msomaji,
Leo tutaangali utata mkubwa uliopo kwenye Quran kama ifuatavyo:
Sura Al-Baqara 2:109
109. Wengi miongoni mwa watu wa Kitabu wanatamani lau wange kurudisheni nyinyi muwe makafiri baada ya kuamini kwenu, kwa ajili ya uhasidi uliomo ndani ya nafsi zao, baada ya kwisha wapambanukia Haki. Basi sameheni na wachilieni mbali mpaka Mwenyezi Mungu atapo leta amri yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
Hapa quran inaongelea watu wa kitabu (yaani Wakristo), na kusema:
Wengi wa watu wa kitabu, kutokana na wivu wao, wanatamani kuwarudisheni kwenye kutoamini baada ya kuwa mmeamini, pamoja na kwamba ukweli umeshadhihirishwa wazi mbele yao. Kwa hiyo wasameheni na kuwavumilia hadi Allah atakapowafunulia mapenzi yake. Yeye ana nguvu juu ya kila kitu.
Quran pia inawaagiza Waislamu katika sura Al Imran 3:20 kwamba:
Na pindi wakikuhoji, basi sema: Mimi nimeusalimisha uso wangu kumwelekea Mwenyezi Mungu, na kadhaalika walio nifuata. Na waambie walio pewa Kitabu na wasio na kisomo: Je! Mmesilimu? Wakisilimu basi wameongoka. Na wakikengeuka basi juu yako ni kufikisha ujumbe tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaona waja wake.
Yaani:
... kama wasipowasikiliza, basi ninyi kazi yenu pekee ni kuwaonya tu.
Kwa hiyo, kutokana na aya hizi mbili, yaani Al-Baqara 2:109 na Al Imran 3:20, tunaona mambo yafuatayo:

KWANINI ALLAH NA MUHAMMAD (S.A.W) WALIRUHUSU KUUWAWA KWA WAKONGWE NA AJUZA?


Ndugu msomaji,
Leo tutaangalia tabia mbaya ya Allah na Mtume wake Muhammad. Hivi kwanini Allah aliruhusu kuuwawa kwa Vikongwe? Hivi kwanini Muhammad alifanya hiyo kazi ya Allah na kuwauwa Vikongwe na ajuza?
Mohammad na kikosi chake kiliuwa wazee wa makamo; Umm Qirfa Fatima, Abu Afak na mzee aliyekataa kusujudia Al-Kaaba.
Baada ya kuuteka mji wa Kaaba Mohammad alimtuma mfuasi wake, Zayd Ibn Haritha kuenda kuuteka kabila ambalo liliukana Uislamu. Zayd bin Haritha alifanikiwa kuuteka huo mji pamoja na kuuwa wazee wakongwe na kuwateka wanawake na watoto walitojaribu kutoroka.
“…na tuliwashambulia kutoka pande zote hadi tukafika karibu na visima vyao ambapo tulipigana vita vikali. Tuliwauwa Aadui zetu wengine huku wengine wakichukuliwa kama mateka wa vita. Niliona kwa mbali kundi la watu lililojumuisha wanawake na watoto wakitoroka. Niliogopa, wasije wakafike mlimani kabla yangu, hivyo nikalenga mshale kati yao na ukaangukia kwa mbele kati yao na mlima. Nikawarudisha nikiwakimbiza kama mifugo walikotoka. (Sahin Muslim 4345)
Umm Qirfa ni miongoni mwa wanawake walitekwa vitani
Alikuwa ajuza (bi kizee), mke wa Malik. Binti yake (na wenzake) walitekwa pia. Zayd Ibn Haritha akaamuru Qays kuuwa Umm Qirfa na akamuuwa kinyama kwa kumfunga kwa kamba kila mguu kwa ngamia mbili na kuwaamuru hao ngamia kuenda pande tofauti. Umm Qirfa alichanika katikati, akatokwa na damu akapasuka mishipa, mifupa na kufa ghafla! (Ibn Ishaq/Hisham 980)
Binti yake ajuza, Umm Qirfa Fatima, aliletwa Makka pamoja na mateka wengine ambapo alipewa kama jizya (zawadi). (Hii ilikuwa kabla ya Mohammad kumtambua)
Niliwatembeza hadi nikawaleta kwa Abu Bakr ambaye alinitunukiza huyu binti kama zawadi. Hivyo tukafika Medina. Sikuwa nimemvua buibui wakati mtume wa Allah (s.a.w) alipokutana nami njiani na kusema; “nipe huyu binti awe mke wangu.” (Sahih Muslim 4345)
Mohammad aliamuru kuuliwa kwa mkongwe aitwaye Abu Afak. Hii ilitendeka miaka miwili baada ya Mohammad kuingia Medina. Abu Afak akikuwa na umri wa miaka 120. ‘kosa’ lake likiwa kuandika mashairi ya kukashifu vitendo vya mtume wa Uislamu-Mohammad vya kuchinja na kuteka wanawake vitani.
Mohammad akasema, “Ni nani ataniadhibia huyu mtwana?” Hivyo mfuasi wake Mohammad akainuka na kumuua Abu Afak. (Ibn Ishaq/Hisham 995).

Saturday, March 26, 2016

NZI, MIKOJO, NA MATE YA MUHAMMAD NI DAWA KATIKA UISLAM


UTATA WA KUJITIBU KATIKA UISLAM
1. Eti Nzi ni dawa?
2. Eti Mate ya Muhammad ni Dawa?
3. Eti Kunywa Mikoja ni dawa!!!!
Jamani hii sayansi ya Kiislam ilitokea wapi?
MUHAMMAD ASEMA NZI NI DAWA
"Kama nzi ataangukia kwenye kinywaji cha yoyote kati yenu, itafaa kumchovya (kwenye kinywaji), kwani moja ya mbawa zake ina ugonjwa na linguine lina tiba (kiuasumu cha ugonjwa) (1). Maelezo chini ya ukurasa (1) yanasema "Tazama Hadithi na.673 juzuu ya 7 (kwa maelezo)" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 15 na.531 kabla ya uk. 335.
"Abu Huraira alisimulia: Nabii alisema, ‘Kama nzi wa nyumbani ataangukia kwenye kinywaji cha mmoja wenu, na amchovye nzi huyo (kwenye kinywaji), kwani moja ya mbawa zake ina ugonjwa na nyingine ina tiba ya ugonjwa huo." Bukharijuzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 16 na.537 uk.338.
Kwa taarifa, nzi aliyeshiba vizuri huenda haja kubwa kila baada ya dakika tano kwa mujibu wa
http://www.thebestcontrol.com/bugstop/control_flies.htm.
Abu Hureira ana kumbukumbu halisi: "Abu Huraira alisimulia: Nilimwambia Mtume wa Allah ‘Nimesikia simulizi (Hadithi) nyingi kutoka kwako lakini nimezisahau.’ Mtume wa Allah alisema, ‘Tandaza Rida (vazi) lako’ nilifanya kama alivyosema na kisha akaitembeza mikono yake kana kwamba anaijaza na kitu fulani (na kisha akaikunjua kwenye Rida langu) na kusema, ‘Chukua na jifunike shuka hili mwilini mwako.’ Nilifanya hivyo na baada ya hapo sijawahi kusahau kitu chochote." Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 3 sura ya 43 na.119 uk.89. Pia Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 27 na.841 uk.538; Bukhari juzuu ya 9 sura ya 23 na.452 uk.332.
"Abu Huraira anasimulia: Mtume wa Allah alisema, ‘Ikiwa nzi ataangukia kwenye chombo cha yoyote kati yenu, mtu huyo na amchovye (kwenye hicho chombo) na kumtupa mbali, kwani kwenye bawa lake moja kuna ugonjwa na kwenye bawa linguine kuna uponyaji (1) (kiuasumu chake) yaani, tiba ya huo ugonjwa." Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 uk.58 na.673 uk.452-453.

Maelezo chini ya ukurasa (1) yanasema, "Kwa mujibu wa fani ya tiba sasa inafahamika sana kuwa nzi hubeba vijidudu vyenye kusababisha magonjwa (pathogens) kwenye baadhi ya sehemu zake kama ilivyosemwa na Nabii (karibu miaka 400 kabla wakati ambapo wanadamu walikuwa na ufahamu mdogo sana wa tiba ya kisasa). Kwa namna hiyo hiyo, Mungu aliumba viumbe na njia nyingine ambavyo vinaviua vijidudu hivi vinavyosababisha magonjwa k.m. kuvu la penisilini huua vijidudu kama Staphalococci na vinginevyo. Hivi karibuni majaribio yaliyofanywa chini ya usimamizi yameonyesha kuwa nzi hubeba vijidudu vyenye kusababisha magonjwa (pathogens) pamoja na viuasumu vya hivyo vijidudu. Kwa kawaida nzi anapogusa kimiminika kinachotumika kama chakula huathiri kimiminika kwa vijidudu vyake vinavyosababisha magonjwa, kwa hiyo ni lazima kumchovya ili kutoa pia kiuasumu cha vijidudu vyenye kusababisha magonjwa ili vipambane na vijidudu hivyo. Kuhusiana na somo hili, nilimwandikia pia rafiki yangu Dr. Muhammad M. El-SAMAHY mkuu wa Idara ya Hadithi ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar Kairo (Misri) ambaye aliandika makala ya Hadithi hii na kuhusiana na fani ya tiba amesema kuwa wataalamu wa viumbe vidogo (mikrobiolojia) wamethibitisha kwamba kuna chembe chembe za chachu za longitudino zinazoishi kama vimelea ndani ya tumbo la nzi na chembe chembe hizi za chachu, ili kurudia mzunguko wao wa maisha huchomoza kupitia kwenye neli za kupumulia za nzi na endapo nzi atatumbukizwa tena kwenye kimiminika, chembe hizi hupasuka kwenye kimiminika na vitu vilivyomo ndani yake ni kiuasumu cha vijidudu vyenye kusababisha magonjwa ambavyo nzi huvibeba."

ALLAH KARUHUSU KULA NYAMA YA MIJUSI, FISI, NA NGAMIA


Ndugu msomaji,
Leo tutaandali nyama zinazo liwa na Waislam ambazo ni haram na Najisi kutokana na Biblia.
Mambo ya Walawi 7: 4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; NGAMIA, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu. 6 Na SUNGURA, kwa sababu hucheua, lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
Lakini nilipo soma vitabu vya Kiislam, nikagundua kuwa, wao wana chuki kubwa na Nguruwe tu, huku wakila kwa furaha nyama ya Ngamia, mijusi, Sungura, Bata, nk.
Hebu tusome kidogo ushahid kutoka vitabu vyao:
Sayyidina Ibn Ammar (RA) alisema kuwa, siku moja alimuuliza Jabir Jbn Abdullah (RA) kuhusu uwindaji wa FISI. Alinijibu na kusema, inaruhusiwa kuwinda Fisi. Nilimuuliza, Je, tunaruhusiwa kula, na akanijibu kuwa Kula Fisi ni Halal (Inaruhusiwa kula Fisi).
Nikamuuliza tena, Je, Nabii wa Allah(SAW) aliruhusu kula Fisi? Jabir r alinijibu na kusema. NDIO, Nabii wa Allah aliruhusu kula Fisi. [Abu Dawud 3801, T 1798, Ibn e Majah 3085, Ahmedl4456]
9- Kitabu cha HAJJ
Kama tulivyo soma hapo juu, Waislam wameruhusiwa kula nyama ya Fisi. Zaidi ya hapo, Muhammad aliendelea na kuruhusu kula nyama za mijusi.
MTUME MUHAMMAD ASEMA KULA NYAMA YA MIJUSI NI HALAL
Sahih Muslim Kitabu 21, 4788 Idadi :
Ibn 'Umar taarifa kwamba kulikuwa na baadhi ya watu na Mtume wa Allah (amani iwe juu yake) miongoni mwa maswahaba wake alikuwepo Sad. Basi ililetwa nyama ya Mjusi na mwanamke miongoni mwa wake wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (amani iwe juu yake) alisema: Ni nyama ya mjusi. Hapo Nabii Muhammad alisema: Kuleni hiyo nyama ya Mjusi kwa kuwa ni halali…
Eti kula Nguruwe ni haram lakini wanakula Fisi na Mijusi. Eti kula nguruwe ni haram lakini wanakula NGAMIA. Huu ni msiba.
Swali la kujiuliza, kama kweli Yehova Mungu wa Musa ndie huyo huyo Allah wa Waislam, kwanini WAISLAM wanapinga aya ya kula NGAMIA? Mambo ya Walawi 7: 4 Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; NGAMIA, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.
Zaidi ya hapo, Waislam wanakunywa Mikojo ya Punda na maziwa ya Punda. Je, huko si kuvynja amri ambayo ilisemwa katika Mambo ya Walawa 7 aya ya 4?
Abdallah Ibn Umar anasema kuwa kula Nyama ya Ngamia, na kunywa Maziwa yake ni HARAM. Lakini waislam wao wanaendelea kula Nyama ya Ngamia na kunywa Maziwa na Mikojo ya NGAMIA. (‘Abdallah Ibn ‘Umar al-Baydawi, Tafsir al-baydawi)
MUHAMAMD AWARUHUSU WAISLAM KUNYWA MIKOJO NA MAZIWA YA NGAMIA AMBAYE NI HARAMU KATIKA [WALAWI 7: 4]
Hata hivyo Muhammad aliwaamuru baadhi ya watu kumfuata mchungaji wake na kunywa maziwa na mikojo ya ngamia.

Ancient Jewish Wedding Ceremony: “No man knows the day or hour, only the Father”

  The Ancient Jewish Marriage Rite: A Detailed Exposition of Betrothal, Preparation, and Consummation Dr. Maxwell Shimba Shimba Theological ...

TRENDING NOW