Wednesday, August 10, 2016

ALLAH SIO MWENYEZI MUNGU (SEHEMU YA PILI)


JE, MALAIKA MKUU WA YEHOVA NDIO YULE YULE WA ALLAH?
Ikiwa Allah ndiye Yehova, basi ni wazi kuwa Malaika Mkuu atakuwa mmoja pia. Ikiwa si mmoja hata Malaika mkuu watakuwa tofauti.
Tuanze kuangalia Allah anavyosimulia katika Qurani naye anasema hivi
Qr. 81 au surat At-Takwyr 19-21 (Kukunja/jua litakapokunjwa)
Kwa hakika hii (Qurani) ni kauli (aliyokuja nayo) mjumbe mtukufu (Jibrili) Mwenye nguvu, mwenye cheo cha hishima kwa Mwenyenzi Mungu. Anayetiiwa huko (mbinguni na malaika wenziwe) kisha muaminifu.
Ufafanuzi wa aya hizi. ulio ndani ya Qurani unaelezea aya hizi 19-21, unafundisha hivi…….
Mjumbe mtukufu na mwenye kutiiwa huko mbinguni ni Jibrili, ambaye ndiye mkubwa wa malaika wote
MALAIKA MKUU WA MUNGU YEHOVA NI HUYU
Yuda 1:9,
Lakini Mikaeli Malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthumbutu kumshitaki kwa kumlaumu bali alisema Bwana na akukemee
Hapa tunaona aya zinatufundisha waziwazi kuwa malaika mkubwa wa Allah anaitwa Jibril na Malaika mkuu wa Mwenyezi Mungu wetu Yehova anaitwa Mikaeli.
Swali; Kwa kuwa Malaika hao ni tofauti, je, Allah ndiye Yehova? Kwa kujua zaidi tofauti ya malaika, jipatie nakala ya somo la: Malaika Jibrili na Gabrieli, je ni Malaika mmoja. Somo hilo tunalo, jipatie.http://www.maxshimbaministries.org/…/malaika-gabriel-wa-bib…
Mwanzo1:26-27
Mungu akasema “Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na wanyama, na nchi yote, pia na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba. Hapa tunaona Mungu wetu Yehova ameumba mtu kwa mfano wake, lakini Allah anasema hana anayefanana naye hata mmoja……
Swali kwako mfuatiliaji:
Je, Allah ndiye Yehova?
Tafadhali usome aya hizi ili kujua zaidi (Mwanzo 5:1-2, 9:6, 1Korintho 11:7, Kolosai 1:15, 3:10, Matendo 17:28-29,Yakobo 3:9).
Pengine waweza kusema Je, Mungu amefanana na mimi kivipi? Jua kwamba Mungu ni Roho (Yohana 4:24) Naye alitupa pumzi (yaani roho ya uhai (Mwanzo 2:7) isitoshe Mungu ndiye Baba wa roho zetu (Waebrania 12:9) Mungu anasema Roho zetu ni mali yake (Ezekieli 18:4, Hesabu 16:22)
Leo tumejifunza kuwa Allah sio Mungu wa Biblia ajulikanaye kwa jina la YEHOVA.
FUATILIA SEHEMU YA TATU

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW