Sunday, September 9, 2018

HONGERA MAREHEMU MUHAMMAD KWA KUKUBALI WEWE NI KAFIRI PAMOJA NA ALLAH

Image result for KAFIRI


Na Ustadhi Abel Sulaiman Shiliwa:

WAISLAMU MNAKUBALI KUWA ALLAH NA MALAIKA WAKE JIBRIL NI MAKAFIRI?
Hili siyo swali la kashifa, dhihaka ama tukano, bali ni swali tu la ufahamu, kutokana na itikadi, na imani ya Waislamu kuamini kuwa MUNGU aliyemtuma YESU, wanaemwitakidi kuwa ni Isa, ndiye Mungu aliyemtuma MUHAMMAD, pia Waislamu wanaamini kuwa, Malaika Gabriel aliyetumwa na MUNGU kwenda kwa Mariamu kumpa habari za kumzaa YESU KRISTO, ndiye huyo huyo JIBRIL aliyetumwa kwenda kumpa Muhammad utume na ndiye aliyekuwa anamteremshia MUHAMMAD Wahyi (Ufunuo) kutoka kwa ALLAH.
Sasa kama hivyo ndivyo, Je! mnakubaliana nami kuwa, ALLAH NA JIBRIL ni makafiri kwa mujibu wa QURAN, Kama inavyojinadi Quran.
( وَقَالَتِ الْيَهُودُ عُزَيْرٌ ابْنُ اللَّهِ وَقَالَتِ النَّصَارَى الْمَسِيحُ ابْنُ اللَّهِ ۖ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَاهِهِمْ ۖ يُضَاهِئُونَ قَوْلَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ ۚ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ ۚ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ )
التوبة (30) At-Tawba
Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!
Hapo Muhammad anapewa ufunuo (Wahyi) na Jibril kutoka kwa ALLAH kuwa, Wakristo kusema YESU KRISTO ni Mwana wa Mungu, ni maneno wanayoiga (yaani wao siyo Waanzilishi wa tamko hilo) bali ni waigaji tu wakiyaiga maneno ya waliokufuru kabla yao, yaani kuna MAKAFIRI waliotangulia kusema hayo ya Masihi kuwa Mwana wa MUNGU, na Masihi huyo ni Yesu.
Yohana 4:25 Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.
26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye.
Ni ukweli usiopingika kuwa, Wakristo kusema YESU ni MWANA WA MUNGU, hawakuanzisha wao, isipokuwa kuna sehemu wametoa, na aliyeanza kusema ni GABRIEL, ambaye WAISLAMU wanamwitakidi kuwa ndiye JIBRIL, GABRIEL anasema.
Luka 1:35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.
Malaika ndiye wa Kwanza kusema kuwa, Yesu ataitwa Mwana wa Mungu, atakapozaliwa, na MUNGU akaja kuthibitisha kuwa YESU ni MWANAE.
Mathayo 3:17 na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Sauti hiyo ikajirudia tena MLIMANI YESU alipokuwa na WANAFUNZI wake.
Mathayo 17:5 Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
6 Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.
Petro akathibitisha kuwa SAUTI ILE wao wenyewe waliisikia.
2 PETRO 1:16 Maana hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.
17 Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
18 Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu.
NA YESU KRISTO kwa upande wake, amethibitisha kuwa, Yeye kuwa Mwana wa Mungu siyo Ufunuo wa Kibinadamu, Bali ni UFUNUO wa Mungu Mwenyewe.
Mathayo 16:13 Basi Yesu akaenda pande za Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake akasema, Watu hunena Mwana wa Adamu kuwa ni nani?
14 Wakasema, Wengine hunena u Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.
15 Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16 Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
17 Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
Sasa ikiwa ni kweli, Malaika GABRIEL ndiye JIBRIL, na huyo Mungu Baba, ndiye ALLAH, JE! waislamu mnakubali kwamba, Allah ni kafiri na Jibril ni kafiri kwa sababu wao ndiyo waanzilishi wa kusema Yesu ni Mwana wa Mungu???
Kama mtakataa kuwa siyo MAKAFIRI, mtakubaliana nami kuwa, Mungu aliyemtuma MALAIKA GABRIEL, siye Mungu aliyemtuma Jibril kwenda kwa Muhammad?? maana Allah kamleta Muhammad na Quran ili kuja kumuonya Mungu wa kweli, ambaye Yesu Kristo ni Mwanae.
1 Yohana 5:20 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele.
Mungu wa kweli anapatikana kupitia Mwanae Yesu Kristo, na Quran imekuja kumuonya huyo Mungu wa kweli kama inavyojinadi.
( وَيُنذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا )
الكهف (4) Al-Kahf
Na kiwaonye wanao nena: Mwenyezi Mungu ana mwana.
Sasa inawezekanaje Mungu huyo aseme Yesu Kristo ni Mwanae katika NCHI YA ISRAEL, halafu aje kuibuka tena katika NCHI YA HIJAZ (SAUDIA ARABIA) na Malaika wake yule yule aje kujionya yeye na huyo Malaika wake???
TAFAKARI KWA KINA NAFASI BADO IPO WOKOVU BADO UPO.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW