Monday, September 10, 2018

UTHIBITISHO WA KIHISTORIA WA YESU KRISTO MUNGU MKUU


Image result for EVIDENCE OF JESUS

Kwenye injili, kuna vianzo gani vya habari kuhusu Yesu mbali ya Biblia vilivyoandikwa kabla ya mwaka 200 BK?

Inawezekana mtu kufikiri kuwa maisha ya Yesu na Ukristo havikuelezwa, hata nje ya Biblia. Moja ya malengo ya kutoa nukuu hizi ni kusitisha madai ambayo watu wenye kushuku wanayatoa kuwa Yesu hakuwahi kuishi hapa duniani.

Cornelius Tacitus (aliyeishi karibu mwwaka 55 hadi karibu mwaka 117 BK) alikuwa mwanahistoria wa Kiroma aliyeandika kuhusu matukio ya Roma na Uingereza kuanzia mwaka 15-70 BK. Dharau aliyoionyesha inadhihirisha kuwa hakuwa rafiki wa Ukristo. Kwenye Annals 15:44 aliandika: “. . . Lakini juhudi zote za kibinadamu, zawadi zote za kifahari za Mfalme, na kuiridhisha miungu, havikuondoa imani mbaya kuwa moto mkubwa [wa Roma] ulitokana na amri [ya Mfalme]. Kwa ajili hiyo, ili kujiepusha na taarifa hiyo, Nero alikazia hatia yake na kutoa mateso makubwa zaidi kwa kundi la watu lililochukiwa kwa ajili ya mambo yake yasiyopendeza, ambalo watu wengi waliliita Wakristo. ‘Christus’, ambaye jina hili lilitokana naye, alipewa adhabu kubwa zaidi na mmoja wa maliwali wetu, Pontio Pilato, wakati wa utawala wa Tiberius, na ushirikina wenye kusumbua sana, ambao ulidhibitiwa kwa muda, uliibuka tena Uyahudi, mahali ulikoanzia, na hata Roma, ambako mambo yote yenye kuchukiza na kuaibisha kutoka sehemu zote za dunia hufanya makao na kupata ummarufu. Kwa ajili hiyo, kwanza kabisa watu waliobainika kuwa na hatia walikamatwa; kisha, baada ya taarifa zao, umati mkubwa ulionekana kuwa na hatia, si kwa ajili ya kuuunguza mji bali kuwachukia binadamu wengine. Vifo vyao viliandamana na dharau za kila namna. Wakiwa wamefunikwa na ngozi za wanyama, walishambuliwa na mbwa na wakaangamia, au walisublubiwa msalabani, au walihukumiwa kutupwa kwenye moto na kuunguzwa, kutumika kama mwanga wakati wa usiku, wakati mwangaza wa mchana unapokuwa umeondoka . . .”

Tacitus kwenye Histories kitabu cha 5 pia anaongelea undani wa vikosi mbalimbali vya Kiroma, cha 5, 10, 15, 12, na watu wengine kutoka vikosi vya 18 na 3 walivyozimisha maasi Uyahudi na kuuteketza mji wa Yerusalem.

   Nukuu za Tacitus zimechukuliwa kutoka kwenye kitabu kiitwacho The Annals and The Histories kilichoandikwa na P. Cornelius Tacitus, Encyclopedia Britannica, Inc. 1952.

Mara Bar-Serapion alikuwa Mshamu wa kawaida aliyemwandikia mwanae, Serapion, barua baada ya mwaka 73 BK. Anamsihi kuiga mwenendo wa watu wenye hekima katika historia ambao walkufa kwa ajili ya mambo waliyoyaamini, kama vile Socrates, Pythagoras, na mfalme mwenye hekima aliyeuawa na Wayahudi. Kazi hii imo kwenye jumba la Makumbusho la Uingereza (British Museum).

Josephus alikuwa mwanazuoni wa Kiyahudi aliyezaliwa mwaka 37/38 BK, aliyeandika mambo mazuri kuhusu Kristo. Kuna vifungu viwili ambavyo anamwongelea Yesu. Kwenye kifungu cha kwanza, Josephus anaongelea maisha na huduma ya Yesu (Antiquities of the Jews 18.3.3, au 18 §§63-64), na kwenye kifungu cha pili anamtaja Yesu kama kaka yake Yakobo (Antiquities of the Jews 20.9.1, or 20 §§200-203). Kuna matoleo mbalimbali ya kifungu cha kwanza, lakini tutaongelea kwa ufupi matoleo ya Kiarabu na Kilatini. Toleo la Kilatini, ambalo limeonyeshwa hapa, na toleo la Kiarabu, ambalo liliandikwa karne ya 10, yanafanana sana isipokuwa toleo la Kiarabu halina sehemu zilizopigiwa mstari.

“Karibu na kipindi hiki, Yesu, mtu mwenye hekima, kama ni sahihi kumuita mtu, kwani alikuwa mtendaji wa mambo ya ajabu, - mwalimu wa watu kama hawa waliopokea kweli kwa furaha. Aliwavuta kwake wengi wa Wayahudi, na wengi wa mataifa. Alikuwa Kristo; na wakati Pilato, kwa mapendekezo ya wakuu wa watu miongoni mwetu, alipomhukumu asulubiwe, watu wale waliompenda tokea mwanzo hawakumuacha, kwani alitokea kwao tena akiwa hai siku ya tatu, kama ambavyo manabii wa Mungu walivyokuwa wametabiri mambo haya na kisha mambo mengine ya maajabu elfu kumi kuhusu yeye; na kabila la Wakristo, walioitwa hivyo kwa jina lake, hawajatoweka leo.” (Antiquities of the Jews 18.3.3, iliyoandikwa karibu mwaka 93-94 BK). Kifungu hiki kimetolewa kutoka Josephus: Complete Works. Kregel Publications 1960. Maneno haya ni muunganiko wa tafsiri ya William Whiston (1867) na toleo la lenye kutumika sana lililotolewa na Porter na Coates, Philadelphia, Pennsylvania).

   Toleo la Kiarabu ambalo ni fupi kuliko la Kilatini huchukuliwa kuwa sahihi zaidi. Toleo lolote lililo sahihi, huu ni ushuhuda wa kuwa Yesu alikuwepo hapa duniani na kuwa alisulubiwa.

Lucian wa Samosata, (pia alifahamika kama Lucian Mgiriki) mwandishi tashtiti wa karne ya pili, aliyeandika kuhusu Kristo, “. . . mtu aliyesulubiwa Palestina kwa sababu ya kuanzisha mfumo wa kidini ulimwenguni . . . Pia, mto sheria wao wa kwanza aliwashawishi kuwa wote ni ndugu wa kila mmoja wao baada ya kukiuka kwa kukataa miungu ya Kigiriki na kwa kumwabudu mwalimu wa filisofia mwenyewe aliyesulubiwa na kuishi kwa kufuata sheria zake.” (The Passing Peregrinus -pia inaitwa The Death of Peregrine 11-13).

Clement wa Roma alikuwa askofu wa Kikristo aliyeliandikia kanisa lililoko Korinto, kimsingi aliwauliza kwa nini hawakuwa wanatii mambo ambayo Paulo aliwaandikia miaka 50 iliyopita. Barua ya Clement iliandikwa mwaka 97/98 BK.

Pliny Mdogo alikuwa liwali wa of Bithynia aliyewaua Wakristo wengi kwa sababu ya imani yao. Alimwandikia Mfalme Trajan mwaka 112 BK na kumuuliza endapo aendelee kuwaua wanaume, wanawake, na watoto kwa ajili ya kutokuiabudu sanamu ya mfalme. Pliny anasema kuhusu Wakristo, “hata hivyo walithibitisha kuwa hatia yao yote ilikuwa kwamba walikuwa na mazoea ya kukutana kwenye siku moja iliyopangea kabla ya jua kuchomoza, baada ya kuimba mistari ya nyimbo kwa kupokezana wakimtukuza Kristo kama Mungu, na kuweka kiapo cha kutokufanya matendo yeyote maovu, bali kujiepusha na ulaghai, uizi, uzinzi, kutokusema uongo, kutokukataa jukumu wanapotakiwa kulitimiza (Epistles 10.96). Pamoja na hayo, Pliny pia anatupa habari kuhusu Waesene.

Papias ni askofu mwingine aliyekuwa mwanafunzi wa Mtume Yohana. Aliandika kazi nyingi sana karibu na miaka 110 hadi 130 BK. Kwa bahati mbaya maandiko yake yamepotea, isipokuwa maelezo mafupi yaliyotolewa na Eusebius wa Kaisaria (aliyeandika karibu mwaka 325 BK). Eusebius anasema kuwa pamoja na mambo mengine, Papias alisema kuwa Injili ya Mathayo iliandikwa kwenye Kiebrania, Marko alikuwa mkalimani wa Petro, na kwama Papias alifundisha kuhusu kuja kwa Yesu kabla ya kipindi cha kutawala kwake duniani kwa muda wa miaka elfu moja, yaani ‘premillennialism.’ (Eusebius alikuwa haamini uwepo wa kipindi hicho, hivyo anaitwa ‘millennialist’).

Ignatius alikuwa mwanafunzi wa Mtume Yohana. Aliandika barua kwa makanisa mengi, na alikufa ama mwaka 107 au 116 BK wakati wa utawala wa Mfalme Trajan.

Polycarp askofu wa Smyrna, alikuwa mfiadini Mkristo na mwanafunzi wa Ignatius aliyeongea kuhusu Kristo. Alikufa karibu mwaka c.163 BK.

Irenaeus, askofu wa yon (Ufaransa), alikuwa mwanafunzi wa Polycarp, na mfiadini aliyeishi kutoka mwaka 120/140-202 BK. Aliandika andiko kubwa dhidi ya mafundisho ya uongo ya wakati ule kutoka mwaka 182-188 BK.

Didache (au Mafundisho ya Mitume Watakatifu) kilikuwa ni kitabu cha kiada cha mafundisho ya kanisa ambacho mtunzi wake na tarehe ya kuandikwa havifahamiki, inakisiwa kuwa karibu mwaka 380 BK.

Justin Martyr alikuwa ni mwanafilosofia Mgiriki aliyezaliwa ama mwaka 110 au 114 BK. Alibadili dini na kuwa Mkristo karibu mwaka 138 na kwa mujibu wa kazi yake, First Apology ilikuwa miaka 150 baada ya Kristo kuzaliwa. Kwenye utetezi wake wa kwanza na wa pili, na kazi yake, Dialogue with Trypho the Jew, Justin anaeleza kuwa Yesu ni Mungu. Chronicon Paschale inaeleza kuwa Justin aliuawa kwa sababu ya imani yake mwaka 165 BK.

Suetonius, mwanahistoria wa Kiroma na afisa wa mahakama aliyeandika karibu mwaka 120 BK, anasema kuwa “Wakati Wayahudi walipokuwa wanafanya vurugu zilizotokana na Krestus (Chrestus, ni tahajia nyingine ya Kristus [Christus], yaani Krsto), aliwafukuza Roma (Life of Claudius 25.4).

Theophilus, askofu wa Antiokia alikuwa mwandishi wa kwanza anayefahamika sasa kutumia neno la Kigiriki lenye kumaanisha Utatu (Triad) kwenye To Autolycus kitabu cha 2 sura ya 15, uk.101. Aliandika kati ya mwaka 168 na 181/188 BK.

Clement wa Alexandria, huyu ni tofauti na Clement wa Roma aliyeongelewa hapo awali, ambaye aliishi kutoka mwaka 193-217/220 BK. Aliandika kwa kiasi kikubwa sana ikiwa ni pamoja na wimbo wa Kristo na kazi kubwa iitwayo Miscellanies.

Hippolytus aliandika kutoka mwaka 225-235/6 BK na aliandika Refutation of All Heresies. Hippolytus alikuwa mwanafunzi wa Irenaeus.

Tatian aliishi kutoka mwaka 110-172 BK na aliandika mpangilio wa injili nne unaoweka pamoja matukio yanayofanana wenye karibu 79% ya mistari yote ya kwenye injili. Kwa bahati mbaya, baadaye aliiasi imani na kujiunga na Waenkrate (dhehebu la Kinostisia la karne ya pili waliokuwa wanazuia kuoa au kuolewa, kula nyama na kunywa mvinyo), dhehebu la mafundisho ya uongo la Kinostisia (harakati kizushi ya zama za kanisa la Kikristo la karne ya pili BK iliyokazia kuwa mada ni ovu na kuwa uhuru unapatikana kwa ufahamu).

Talmudi za Kiyahudi zinamwongelea Yesu sehemu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Babylonian Talmud, Tol’doth Yeshu, Barailu, Amoa ‘Ulla’, Yeb. IV 3, na Baraita. Tazama pia Tractate Sanhedrin.

Phlegon alikuwa mwandishi wa Kigiriki kutoka Caria na mtumwa wa Mfalme Harian aliyeachwa huru. Aliandika muda mfupi baada ya mwaka 137 BK kuwa kwenye mwaka wa nne wa kipindi cha 202 cha miaka mine baina ya michezo ya Olimpiki [33 BK] kulikuwa na “kupatwa kwa jua kukubwa zaidi” na kwamba “kulitokea giza saa sita mchana [saa 6:00 kamili] hata nyota zilionekana mbinugni. Kulitokea tetemeko kubwa la ardhi huko Bithynia, na vitu vingi vilipidnuliwa huko Nikea” (Case for Christ, uk.111). Nukuu nzima kwa mujibu wa Baker Encyclopedia of Christian Apologetics, uk.384 inasomeka: “Yesu, alipokuwa hai, hakujipa msaada wowote ule, lakini alifufuka baada ya kufa na kuonyesha alama za kuteswa kwake, na kuonyesha jinsi mikono ilivyochomwa nan a misumari” na baadaye “kupatwa kwa jua wakati wa utawala wa Kaisari Tiberius, ambao unaelekea kuwa ndio muda Yesu aliposulubiwa, na tetemeko kubwa lililotokea wakati huo” kwenye Origen Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 33, uk.455 kwenye Ante-Nicene Fathers juzuu ya 4, na Julius Africanus Events in Persia sura ya 18, uk.136. Tazama pia Origen Against Celsus kitabu cha 2 sura ya 59, uk.455.

Thales (au Thallus) alikuwa mwanahistoria wa Kipalestina aliyetajwa na Julius Africanus (aliyeandika mwaka 232-245 BK) Julius anaongea kuhusu giza lililotkea wakati wa Kristo, “Giza hili Thallus, kwenye kitabu cha tatu cha historia yake, analiita, kama inavyoonekana kwangu bila sababu, kupatwa kwa jua” (The Ante-Nicene Fathers juzuu ya 6 kipande cha 18, uk.136). Muktadha ni Julius anapoongelea jinsi muda kuanzia amri ya Ahasuero hadi kusulubiwa kwa Kristo, ulivyotimiza Danieli 9.

   Mwanahistoria wa Samaria, Thallus, ambaye ni tofauti na mwanahistoria wa Kigiriki, Thales, alikuwa anafahamika sana. Kazi zifuatazo zinamtaja Thallus.

Justin Martyr’s Hortatory Address to the Greeks kitabu cha 9, uk.277 inawataja Thallus, Philo, Josephus, na wengineo.

Theophilus to Autolychus sura ya 29, uk.120 anamtaja Thallus, pia kabla ya hapo Berosus ambaye ni mwanahistoria Mkaldayo aliyeongea kwenye uk.121.

Octavius wa Minucius Felix sura ya 22, uk.186

Tertullian’s Apology sura ya 19, uk.33 inawataja Thallus na Josephus.

Julius Africanus kipande cha 18, uk.136.

The Shepherd of Hermas ni kazi ya Kikristo ambayo mwandishi wake hafahamiki iliandikwa karibu mwaka 160 BK.

Athenagoras alimwandikia mfalme wa Roma utetezi wa Ukristo karibu mwaka 177 BK.

Aristides wa Athens na Quadratus pia wanafahamika kuandika utetezi wa Ukristo, lakini tuna baadhi tu ya maandiko yao yaliyohifadhiwa.

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW