Sunday, September 9, 2018

UTUME WA PAULO KWA MUJIBU WA QURANI TUKUFU

Image result for Apostle Paul
Mwanzo wa Utume wa Paulo;
Katika Hesabu 12:6
Mwenyezi Mungu anaeleza namna mitume na Manabii wanavyopata Wahyi kutoka kwa Mungu:
Je sifa hii ya kuletewa Wahyi Paulo alikuwa nayo?
Tunasoma katika Matendo. 16:9
“Wakati wa usiku Paulo akaona maono…”
Je Mungu alieleza kuwa Paulo alitumwa kwa watu gani?
Matendo. 9:15
“Lakini Bwana akamwambia Anania…Mtu huyu ni chombo changu kiteule nilichokichagua apate kulichukua jina langu kwa watu Mataifa na wafalme wao na mbele ya watu wa Israeli.”
Matendo 13:2
“Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalumu niliyowaitia”
Je Paulo Mwenyewe anajishuhudia vipi kuhusu utume wake?
Wagalatia 1:1
“Paulo, mtume, si mtume wa wanadamu aliyetumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu”
Wakolsosai 1:1
“Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na ya Kristo Yesu tumaini letu.”
Hapa Paulo anatusaidia kujibu swali la Mada yetu, anasema ni “Mtume wa Mungu”
UTUME WA PAULO KWA MUJIBU WA QUR’AN NA HADITH ZA MTUME.
Kwanza Kabisa nikumbushe sifa za imani ya Mwislam. (Swifat ul I’iman mufaswalu)
Kwanza ni Kumwamini Mwenyezi Mungu
Pili ni Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu
Tatu ni kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu
Nne ni Kuamini Mitume wake
Tano ni kuamini Kheri na Shari zake
Sita ni kuamini Siku ya Mwisho (Siku ya malipo)
Kwa mujibu wa Mada hii nitajikita katika sifa ya nne yaani Kuamini juu ya Mitume wa mwenyezi Mungu.
Katika imani ya Kiisalamu kuna jumla ya mitume wapatao 124,000 laki moja na Ishirinina tano, kati ya hao, ni mitume 25 tu, Mtume Muhammad (S.A. W) ndiyo aliweza kufunuliwa na kuelezewa habari zake. Kama inavyosema Qur’an katika Sura ya 4:164
“Na mitume tuliokwisha kukuhadithia kabla yake, na mitume wengine hatukukuhadithia. Na Mwenyezi Mungu alinana na Musa kwa Maneno”
“Semini nyinyi: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa sisi, na yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyopewa Musa na Isa, na pia waliyopewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutofautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.”
Aya hii inawataka Waislamu kuwa amini mitume wote wa zamani, aya inasema wanatakiwa waamini walioteremshiwa wajukuu wa Yakobo, na Manabii wengine wote ambao hawakutajwa ndani ya Qurani.
Paulo Mwenyewe amesema kuwa ni Mjukuu wa Yakobo.
“…mimi ni Mwisraeli wa kabila la Benyamini, Mwebrania wa Waebrania..” (Wafilipi 3:5)
Benjamini alikuwa mtoto wa Yakobo. Hivyo twaona kuwa Qurani Sura ya 2:136 inakusudia kuaminiwa kwa mitume wote waliotangulia akiwemo na Paulo na manabii wote waliotajwa ndani ya Taurat, Zaburi na Injili.
Hivi yaonekana kuwa umati mkubwa wa mitume bwana Muhammad hakuweza kuelezwa habari zake. Sehemu kubwa ya Mitume na Manabii waliotajwa ndani ya Qur’an ni wale waliotajwa pia ndani ya Biblia. Hivyo basi Mwislam anapotaka kufahamu zaidi juu ya habari za Mitume na manabii yampasa kuzingatia agizo la Mwenyezi Mungu kwa Mtume katika Sura 10:94 kwamba;
“Na ukiwa na shaka juu haya tuliyokufunulia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako (Mayahudi na Wakristo)…”
Inashangaza kuona kuwa baadhi ya Waislam wameibuka siku hizi kupinga mitume waliofunuliwa katika Biblia hasa Mtume Paulo. Kwa sehemu kubwa upinzani huu unafanywa bila kuzingatia Qur’an Yenyewe pamoja na mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W). Yaonekana wale wanaopinga hawana elimu ya kutosha juu ya Qur’an na Imani yenyewe ya Uislam.
Hebu tuangalie mada hii kwa kutumia Qur’an na Hadith pamoja na Sherehe za Wanazuoni mbalimbali ndani ya Uislam.
Tunasoma Katika Qur’an 36:13-14 kwamaba
Mwenyezi Mungu hapa anamkumbusha mtume juu ya wakazi wa mji Fulani, ambapo yeye Mwenyewe Mwenyezi Mungu anasema—alituma “wajumbe wake”.
Wafasili wengi wa Qur’an wakiwemo Shekhe Balwani, pamoja na Yusufu Ali katika tafsiri zao wanautaja mji huo kuwa ni ANTIOKIA.
Ibn Kathir yeye anatueleza zaidi juu ya mitumehao kuwa majina yao yalikuwa, Yohana, Simoni pamoja na Paulo.
Ni dhahiri basi kwamba hoja hii ya upizani juu ya Paulo ndani ya Uislam ni ya hivi karibuni sana. Ushahidi wa hadithi za mtume Muhammad waonyesha kuwa Waislamu wa mwanzo hawakuwa na tatizo juu ya utume wa Paulo.
Katika kitabu kilichoandikwa na Ibn Hisham kiitwacho Sirat Nabawiyat, juzuu ya 4 uk. 140 (Tazama sehemu ya tatu ya somo hili) kuna section nzima Mtume Muhammad anawaelezea Masahaba wake orodha ya mitume wa Bwana Yesu na Sehemu walizotumwa, Miongoni mwa mitume hao, ametajwa pia Mtume Paulo, na kwamba Yeye Paulo alitumwa kwa watu wa Rumi.
Ndugu zangu Waislamu kama nilivyotangulia kusema, ikumbukwe kwamba kupinga utume wa Paulo ni kupinga Imani, kupinga Dini yenyewe na kupinga Qur’an, kuwapinga wanazuoni waliotutangulia, na mwisho wa yote, KUMPINGA MWENYEZI MUNGU. Hivyo basi twaona kuwa, kupinga utume wa Paulo ni Ukafiri uliokithiri ambao Mwenyezi Mungu hawezi kuuvumilia.
Shetani ni mjanja sana, anahila nyingi za kuwapotosha wanadamu, wengi wanadhani kuwa wanatetea dini wanapopinga utume wa Paulo kumbe kwa yakini wanapinga dini kwa kufanya hivyo. JIEPUSHE USINASWE KATIKA MTEGO HUU.
Bada ya kuangalia uthibitisho juu ya utume wa Paulo ndani ya Biblia Takatifu, hebu tuigeukie Quran tukufu ili kupata uthibitisho mwingine.
UTUME WA PAULO KWA MUJIBU WA QURANI TUKUFU
Kwa kuanza naomba niwakumbushe Waislam kwambu uislamu una sifa zifuatazo. (swifat ul I’iman mufaswalu)
1. Imani juu ya Mungu.
2. Imani Juu ya Malaika wa Mwenyezi Mungu.
3. Imani juu ya Vitabu vya Mwenyezi Mungu
4. Imani juu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu
5. Imani juu ya Kheri na Shari za Mwenyezi Mungu.
6. Imani juu ya Siku ya Mwisho.
Kwa mujibu wa Mada ya leo. Nitajikita juu ya Imani juu ya Mitume.
Waislamu wanaamini kwamba, wapo Mitume wapatao 124,000. Kati ya hao. ni 25 tu ndiyo ambao mtume Muhammad (S. A. W) aliweza kupewa habari zake. kama tunavyosoma.
[ AN-NISAAI – 164 ]
Na Mitume tulio kwisha kukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine hatukukuhadithia. Na Mwenyezi Mungu alinena na Musa kwa maneno.
Hii inamaana kwamba Muhamad alifahamu kidogo sana kuhusu habari za mitume. yaani kama ni asilimia ni 0.0002 ya uelewa wake juu ya mitume. na huo ndio uelewa wa waislamu wote linapokuja swala la mitume. Hata hivyo. Allah s.w alikwisha kumwelekeza mtume mahala pa kupata nuru zaidi aliposema.
(YUNUS – 94)
Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka.
Hivyo kwa habari za mitume, karibia mitume wote aliosimuliwa muhammad wamo kwenye Biblia. Basi kama tulivyoona sehemu ya kwanza ya mada yetu leo twawagabarisha waislamu juu ya utume wa Paulo.
Hata hivyo ukisoma Quran kwa uangalifu utagundua kuwa Habari za Paulo zimeelezwa vizuri humo.
Chunguza aya hii.
(YA-SIN – 13-14)
Na wapigie mfano wa wakaazi wa mji walipo wafikia walio tumwa.
Tulipo watumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwenu.
Aya hii inaeleza kisa cha WAJUMBE WA MWENYEZI MUNGU.
Wafasiri na wanazuoni mfano Shekhe Balwani, Yusufu Ali wamefasiri aya hii na kusema mji huo walikotumwa wajumbe ni ANTIOKIA.
Ibin Kathir katika tafsir yake anasema wajumbe hao ni Yohana, Simoni na Paulo.
Na hapa namnukuru ibn Kathir.
Imesimuliwa na Ibn Jurayj kutoka kwa Wahb bin Sulayman, imepokelewa na Shu`ayb Al-Jaba’i, “Majina wajumbe wawili wa waliotumwa mwanzo ni Simoni na Yohana na jina la wa tatu ni Paulo. Na mji huo ulikuwa Antiokia” , and the city was Antioch. Na wakasema (kwa watu wa mji huo) “hakika sisi tumetumwa kwenu kama wajumbe”, hii ina maanisha “Wajumbe kutoka kwa Allah aliyewaumba nyinyi na anayewaamrisha mumwabudu yeye peke yake na msimfanyie washirika.” Qatada amesema walikuwa ni wajumbe wa Masihi Isa bin Maryam (a.s) waliotumwa kwa watu wa Antiokia. Wakasema “Ninyi ni wanadamu kama sisi…ni kwa vipi munaweza kupokea ufunuo wakati nyie ni wanadamu na sisi tu wanadamu kama nyie, kwanini sisi hatupokei ufunuo kama nyie?” hivi ndivyo ilivyokuwa kwa watu wa mataifa mengine walivyosema ‘hatuamini’, kama vile Allah anavyotuambia katika sura ya 64:6 , as Allah has told us in the Ayah: That was because there came to them their Messengers with clear proofs, but they said: “Shall mere men guide us!” (64: 6) “Hayo ni kwa kuwa walikuwa wakiwajia mitume wao kwa hoja zilizo wazi, nao wakasema: Hivyo binadamu ndiyo atuongoe? Basi wakakufuru na wakageuka upande. Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao…”
Hivyo twaona kuwa hoja ya kumkataa Paulo ni uzushi wa hivi karibuni. Waislamu, wasomi na Maulamaa wa kale hawakuwa na hoja hii ya kumkataa Paulo.
Shalom,

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW