Friday, September 21, 2018

MUHAMMAD (S.A.W) ALIKUWA ANAMPENDA SANA MTUME PAULO

Image may contain: 2 people
MUHAMMAD (S.A.W) ALIKUWA ANAMPENDA SANA MTUME PAULO
SOMA UTHIBITISHO HAPA
Uislam unaamini na kufundisha juu ya kuwepo kwa wajumbe Manabii, Mitume zaidi ya 124,000 (laki moja na ishirini na nne elfu). Lakini hoja ya msingi ni kuwa pamoja na imani ya kuwepo kwa kiwango cha idadi
hiyo ya wajumbe hao bado maandiko ya Qur an yanataja jumla ya wajumbe 25 tu katika aya kadhaa za kitabu hicho ambao ni:
Adam, Saleh, Lut, Hud, Yaakub, Ibrahim, Yunus, Musa, Daud, Al yaasa(Elisha), Zakara, Dhul Kifli(Ezekiel), Isa, Nuh, Shuaib, Ismail, Yusuf, Is haq, Harun, Suleiman, Yahya, Ayyub, Iliyas, Idrees, Muhammad.
Hao ndiyo mitume pekee wanaonekana kutajwa kwa majina katika mafunuo hayo huku imani ya kiislam ikiamini juu ya kuwepo kwa zaidi ya mitume 124,000.
Katika kitabu kiitwacho SIRAT NABAWIYA. Kilichoandikwa na Ibn Hisham, aliyekuwa mwanafunzi wa ibn Ishak. Katika juzu ya 4 ya kitabu hicho uk 140 tunakuta Muhammad anaorodhesha majina ya Wanafunzi wa Yesu. na anawagawa katika mafungu 2. la kwanza ni wale waliomfuata wakati wa uhai wake na wale waliomfuata baada yakuwa amepaa juu. Muhammad anaeleza kila mmoja wa wanafunzi hao na mahala walikotumwa, kuhusu Paulo anaeleza kuwa Yeye alitumwa Rumi.
Na hapa namnukuru ibn Hisham.
*أسماء رسل عيسى عليه السلام*
أسماء رسل عيسى عليه السلام
قال ابن إسحاق ‏:‏ وكان من بعث عيسى بن مريم عليه السلام من الحواريين والأتباع ، الذين كانوا بعدهم في الأرض ‏:‏ بطرس الحواري ، ومعه بولس ، وكان بولس من الأتباع ، ولم يكن من الحواريين ، إلى رومية ، وأندرائس ومنتا إلى الأرض التي يأكل أهلها الناس ، وتوماس ، إلى أرض بايل من أرض المشرق ، وفيلبس إلى أرض قرطاجنة ، وهي أفريقية ؛ ويحنس إلى أفسوس ، قرية الفتية أصحاب الكهف ؛ ويعقوبس إلى أوراشلم ، وهي إيلياء قرية بيت المقدس ، وابن ثلماء إلى الأعرابية ، وهي أرض الحجاز ؛ وسيمن إلى أرض البربر ، ويهوذا ، ولم يكن من الحواريين ، جعل مكان يودس ‏.‏
Majina ya Mitume wa Yesu Masihi:
“Amesema ibh Is-hak: walikuwa mionguni mwa wanafunzi wa Yesu (amani iwe juu yake) wale waliomfuata wale waliokuwa baada yake duniani: Petro Mwanafunzi wa Yesu, na pamoja naye alikuwepo Paulo miongoni mwa wafuasi, Paulo hakuwa miongoni mwa wale wanafunzi wa kwanza wa Yesu. Naye (Paulo) alitumwa Rumi kuhubiri Injiri. Na Andrea naye alitumwa katika nchi ambayo wakazi wake wanakula watu. Na Tomaso alitumwa katika nchi ya Babeli katika nchi za mashariki. Na Philipo alitumwa katika nchi pande za Afrika, na Yohana alitumwa Efeso na Yakobo alitumwa Yerusalemu na Batholomeo alitumwa Uarabuni katika nchi ya Hijaz. Na Simoni alitumwa Baribari.”
Yashangaza kuona kuwa licha ya ushahidi mkubwa namna hii waislamu wa leo (hasa wanaharakati) wameamua kufumbia macho ukweli huu na kuanza kudanganya watu. ama kwa maksudi ama kwakutokujua. SWALI NI HILI. wanafanya hivyo kwa faida ya nani?
Rafiki yangu mwislamu, napenda kukutahadharisha kwamba, shetani ni mjanja, siku zote atakuja kwa hila akiwatukia waalimu wa uongo, wengine watakuja kana kwamba ni watetezi wa dini kumbe ndiyo waharibifu wakubwa wa dini.
Pamoja na maelezo hayo ya uchambuzi nimeona pia iko haja ya kumuuliza mtume Paulo mwenyewe aweze kujieleza tabia yake katika mwenendo wake kwa Kristo itakayo tuwezesha kujua ujumla wa maana ya kauli yake hiyo. Hebu fuatilia aya hizi:-
2 Wakoritho 11:7 “Je nilifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, Kwasababu niliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira?”
2 Wakoritho 10:1 “Basi mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu………”
2 Wakoritho 12:11 “Nimekuwa mpumbavu, ninyi mmenilazimisha. Maana ilinipasa nisifiwe na ninyi, kwasababu sikuwa duni ya mitume ya mitume walio wakuu kwa lolote, nijapokuwa si kitu.”
“Utume wa Paulo ni hakika kama unavyothibitishwa na maandiko ya Biblia”
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu. Tito 2:13

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW