Monday, November 21, 2016

YESU HAKUWA MUISLAM (SEHEMU YA TATU)


YESU HAKUWAI KUOMBA HUKU AKIANGALIA MAKKAH
Yesu hakuwai kusujudu huku akiangalia Makkah, jambo ambalo ni moja ya masharti katika kumwomba na au abudu “ALLAH”. Quran 2:149. Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo ndiyo Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayo yatenda. 150. Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo ili watu wasiwe na hoja juu yenu, isipokuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Basi msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi - na ili nikutimizieni neema yangu, na ili mpate kuongoka.
Sasa tumsome Yesu katika Biblia, wapi aliangalia wakati akiomba.
Yesu aliomba huku akiangalia Mbinguni soma: Marko 6: 41 Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; na wale samaki wawili akawagawia wote.
Katika aya tuliyo isoma hapo juu, imetupa ushaidi kuwa Yesu aliangalia Juu Mbinguni ambapo Baba yake alipo na si Makkah.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW