Wednesday, August 10, 2016

JE! NI KWELI KWAMBA TORATI YA MUSA IMEHARIBIWA?


👆 Kwa yule anaependa KUJIFUNZA basi atatumia muda mzuri kufuatilia SOMO hili, japo siyo fupi wala siyo refu!
Waislamu wamekuwa wakiamini kwamba, Torati ya Musa, imeharibiwa, imefanywa kuwa ni UONGO, wakiamini kabisa kuwa kwa sasa haipo, iliyopo siyo yenyewe japo ukijaribu kuwaomba wakuonyeshe Orijino yake, hawathubutu kukuonyesha, SWALI LA KUJIULIZA! "utakijuaje kitu hiki ni feki ikiwa Orijino yake huijui"? andiko ambalo linawafanya WAJAWE na UPOFU juu ya torati, ni hili hapa. 👇👇
Yeremia 8:7 Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za BWANA.
8 Mwasemaje, Sisi tuna akili, na torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
👆 hiyo aya ya 8 ndiyo muhimili wao mkubwa kusema kwamba TORATI imekuwa uongo, imeharibiwa, na kwa sababu watu wengi ni WAVIVU wa kusoma vema maandiko, basi hata Mkristo anakuwa radhi kumwacha Yesu, kwa kudhani kuwa, ni kweli Torati haipo, MAANDIKO yanasema! imeharibiwa, imefanywa kuwa UONGO.
2 Petro 3:16 vile vile kama katika nyaraka zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo; katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.
👆 Maandiko yalishasema, kwamba, kuna watu ambao kazi kubwa! ni kuyapotosha maandiko kwa sababu ni VIGUMU kuyelewa!
nikija katika habari hiyo ya YEREMIA 8:8 mungu aliposema Kalamu! hakuwa na maana ya Penseli, au Bic, kwamba, imetumika kuifanya Torati kuwa, UONGO! Bali alikusudua Mwenendo wa watu ambao wamepewa JUKUMU la kuisimamia TORATI, na kuwafunza watu, wanaenenda ndivyo SIVYO, kile ambacho wanawafundisha watu sicho ambacho wao wenyewe wanakiishi, ndiyo maana Mungu akaanza kwa kusema!
Yeremia 8:7 Naam, koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za BWANA.
👆👆 Mungu anawashangaa watu wake kwamba wanazidiwa na ndege, ambao hutambua kile ambacho kinawahusu, lakini wao hawazijui Sheria za BWANA, yaani hawajishughulishi na kusoma wenyewe Torati ya MUNGU, kitendo cha wao kutozijua Sheria za BWANA, wanakuwa wanajidanganya kwamba wanazo akili, na Torati ya BWANA wanayo mikononi MWAO, huku Kalamu yenye UONGO inaifanya hiyo Torati ya ambayo wao wanayo ionekane kuwa ya Uongo pindi ambapo wanawaeleza watu! Unaweza KUJIULIZA, hao Waandishi wanaifanyaje kuwa UONGO! Yesu akaja kufafanua Zaidi na kutilia Mkazo kuwa, Torati ni sahihi ila Walio na JUKUMU la kuifundisha TORATI ndiyo ambao wanaifanya kuwa UONGO. YESU alisema! 👇👇
Mathayo 23:1 Kisha Yesu akawaambia makutano na wanafunzi wake, akasema,

2 Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa;
3 basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi.
4 Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.
5 Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao;
Yesu anasema kuwa, Mafarisayo na Waandishi, wapo kwenye Kiti cha Musa, yaani kwenye TORATI, basi cho chote kile ambacho watakisema, ambacho kipo kwenye Torati! Watu wakifuate, kwa nini WAKIFUATE? kwa sababu torati ipo sahihi, kama isingekuwa SAHIHI basi asingeweza kuwaambia kuwa, wafuate, kwa sababu kitu cha UONGO Yesu hawezi kuagiza kifuatwe! katika kutilia MKAZO kuwa Waandishi ndiyo ambao wanaoifanya TORATI ionekane kuwa ni UONGO! Yesu akasema. 👇👇
"Walakini kwa mfano wa Matendo yao msifanye maana wao husema lakini hawatendi"
Kitendo hicho cha kusema jambo halafu wewe ambaye unakisema, hukitendi, ni ISHARA ya wazi kuwa, kile ambacho unakisema, ni UONGO! kwa nini UONGO? kwa sababu, ingekuwa ni KWELI basi wewe ambaye unakisema ungekitenda!
Mfano:- UNAWAAMBIA WATU KUZINI NI DHAMBI TORATI IMEKATAZA! si kwamba watu hawapendi kuzini, wanapenda, Wataacha kwa sababu torati imesema, sasa Wakimuona Mwandishi, ambaye anawafundisha kuwa Uzinzi ni dhambi, yeye anazini, au kuiba, basi moja kwa moja wataitafsiri kuwa TORATI ambayo ameifundisha ni UONGO! mwandishi huyo anawazuia wao ili yeye AFAIDI!
Yesu akawasema kuwa, Watu watazame kile ambacho kimeandikwa, hata kama anaewaambia yeye hakifuati basi wao wasiwatazame hao bali Waitazame SHERIA isemavyo, ndiyo maana alitangulia kusema.
Mathayo 5:17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.
19 Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Torati kama ISINGEKUWEPO, au kuharibiwa Yesu asingesema kuwa, mbingu na Nchi zitakapoondoka Yodi moja wa Nukta moja ya Torati haitoondoka mpaka Yote yatimie! kauli hii ni UTHIBITISHO KUWA, YESU aliikuta TORATI ikiwa safi kabisa, ila akawa anawaweka WAZI wale ambao waaifanya Torati kuonekana kuwa ni UONGO! WAANDISHI na MAFARISAYO, akasema, haki yetu ni lazima iwazidi wao kwa sababu, Wao wanasema lakini hawatendi, sisi tuwe wasemaji na WATENDAJI.
Torati ilikuwepo haikuharibiwa, hata kabla ya kuja YESU, MUNGU aliagiza kwa kusema
Malaki 4:4 Ikumbukeni torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.
Torati ingekuwa imeharibiwa, MUNGU asingesema, watu waikumbuke TORATI, maana huwezi kukikumbuka kitu ambacho hakipo.
Na hata LEO baadhi ya Watumishi wanaosema kuwa Wanamtumikia Kristo wameifanya INJILI ya Yesu kuwa ni uongo, kutokana na kile ambacho wanakifanya! mtu unamwambia auze NYUMBA, ili fedha akupe kwa kupanda MBEGU, kisha umuombee ili Yesu ampe nafasi ya kwenda Kuishi MAREKANI! mtu huyo asipoenda Marekani, na nyumba ameuza, kwa sababu ya maneno yako, Je! hapo hutomfanya aamini kuwa Injili ni Uongo?
NI SWALI AMBALO NAKUACHIA UWEZE KUTAFAKARI.
BY ABEL SULEIMAN SHILIWA.
For Max Shimba Ministries Org

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW