Monday, November 7, 2016

ADHABU YA KUVUNJA SABATO

Utunzaji wa sabato uliandamana na utoaji adhabu kwa yeyote ambaye alivunja sheria hiyo. Mtu ambaye aliasi sheria ya sabato, adhabu yake ilikuwa ni kuuawa. Maandiko yanasema: Kila mtu atakayefanya kazi yoyote siku ya sabato, hakika yake atauawa. Sasa tukija kwenye agizo la kushika sabato halikuwa ni siku ya kukusanayika, bali ni pumziko la kazi tu na kustarehe kama tunavyoweza kuona katika kitabu cha KUTOKA 31:14-15, “Basi mtaishika hiyo sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake. Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa Bwana, kila mtu atakayefanya kazi yoyote katika siku ya sabato, HAKIKA YAKE ATAUAWA.”
Pia KUTOKA 35:2 Biblia inasema, “Fanyeni kazi siku sita, lakini siku ya saba itakuwa siku takatifu kwenu; ni sabato ya kustarehe kabisa kwa Bwana; mtu awaye yote atakayefanya kazi yoyote katika siku hiyo ATAUAWA”.
Maswali kwa watunza Sabato:
1. Je umesha wai vunja Sabato?
2. Je, umesha wai uwa mtu kwa sababu alivunja Sabato?
3. Kwanini hamfuati hii amri ya kuuwa watu wanao vunja Sabato?
Ndio maana ninasema kuwa Yesu ndio Mwishop wa Sabato na aliitengua.
Ni mimi Max Shimba Mtumwa Yes Kristo

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW