Kwanza nakukaribisha katika somo hili kuhusu ngono na picha za ngono na au ponografia. Ni somo la muhimu sana, maana labda kwenye Kanisa lenu au Msikini wenu au Sinagogi lenu hamjawai fundishwa hili so. Basi ni vema leo tujifunze kwa kutumia misingi ya NENO LA MUNGU.
Kufika sasa, jambo ambalo limefanyiwa utafiti wa mara nyingi sana kwa maneno katika mitandao linahusiana na ponografia. Kutokana utafiti ulio fanywa na “google” unasema kuwa neno “sex” “ngono kwa kiswahili” linaangaliwa mara milioni 506 kila mwezi.
Maana ya ngono:
Ngono ni kitendo cha mtu au watu kufanya kitendo cha kujamiana (Tendo la Ndoa) na pia ni ile hali ya kuwa uchi wa mnyama.
Ngono ni kitendo cha mtu au watu kufanya kitendo cha kujamiana (Tendo la Ndoa) na pia ni ile hali ya kuwa uchi wa mnyama.
Maana ya picha:
Neno picha ni kivuli cha mtu, watu, kitu n.k. Picha si kitu halisi bali ni kivuli chake. Unaweza ukapewa picha ya mtu lakini usifahamu urefu wake au ni mfupi kiasi gani lakini sura yake ukawa umeiweka katika kumbukumbu yako ya fahamu.

Ponografia imeenea sana katika ulimwengu wa leo. Ingawa zaidi ya kitu cho chote, shetani amefaulu katika kugeuza na kupotosha jinsia. Amechukua jambo ambalo ni jema na zuri (mapenzi kati ya mume na mke) na kubadilisha na tamaa, ponografia, uzinzi, ubakaji, na ushoga.
Kwa ujumla picha za ngono ni dhambi kwa kuwa kuangalia picha za ngono ni kufanya zinaa. Hata kama ninyi ni wanandoa, bado kuangalia picha za ngono ni dhambi.
UTHIBITISHO WA AYA:
Bwana Yesu anasema katika Mathayo 5:28, “lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
Bwana Yesu anasema katika Mathayo 5:28, “lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
Hakuna anayeangalia picha za ngono aidha mwanaume au mwanamke alafu asiwake tamaa. Na tamaa hiyo haiwaki kwa sababu ya mwenzi unayeangalia naye, bali inawaka kwa sababu ya wale mnaotazama picha zao, nikiwa na maana kwamba chanzo cha tamaa yako hapo ni utupu wa yule mwanaume na mwanamke wanaofanya ngono na si mwenzi wako. Kwa hiyo, kwa kufanya hivyo, tayari ninyi wanandoa wote mnaingia kwenye mtego wa kuwa wazinzi.
Picha za ngono ni mtego wa shetani katika kukiweka kizazi cha sasa kiweze kila wakati kutafakari mambo ya ngono na sio kumtafakari Mungu. Mtu aliyeathirika na picha za ngono kwenye mitandano kamwe hawezi kuwa na mahusiano ya kweli na Mungu.
UTHIBITISHO WA AYA:
Neno la Mungu linasema katika Wafilipi 4:8, “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, YATAFAKARINI HAYO.”

Picha za ngono zinamfanya mtu awe mateka wa ngono, na ni ngumu kwa mtu aliyeathirika na picha za ngono kujinasua kwenye mtego huo. Kila wakati hujisikia nguvu fulani inamvuta kutazama picha hizo. Kila akiingia kwenye mtandao kuna kitu kinamsukuma kutazama picha hizo. Hizo ni dalili za mtu kuwa mateka na mtumwa wa ngono. Tayari mtu huyo yupo kwenye gereza la shetani la ngono.
Kwa mtoto wa Mungu ambaye hajawahi kunaswa kwenye mtego huu, tafadhari sana usishawishike kuingia, na ninajua ipo neema inayotukataza mambo mabaya katika ulimengu huu wa uovu.
Tito 2:11-12 inatupa mwanga juu ya neeema hiyo, “Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa.”
Moja ya njia ya kuiishi neema hii ni katika kutambua nguvu ya kuchagua kujihusisha na mambo yanayompendeza Mungu, kwa kulifuata Neno lake lote. Hapo ndipo tunapoweza kusafisha njia zetu. Zaburi ya 119:9, “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.”
MFANO WA MFALME DAUDI NA BATHSHEBA:
Wakati mmoja Mfalme Daudi alikuwa yuko gorofania, na akamuona mke wa Uria “Bathsheba akioga, sasa basi, matokea ya Mfalme Daudi kumwona yule mwanamke akiwa kwenye utupu kilimfanya alale naye. Hiyo ilikuwa sana ni Live Movie ya ngono. Kama Mfalme Daudi asinge muone Bathsheba akiwa uchi, basi asinge sukumwa na kitendo cha kufanya nae ngono.

UTHIBITISHO:
2 Samweli 11:2-27“ Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?”………..

Kile kitendo cha Daudi "kuona" lilikuwa kosa kubwa la kiufundi katika akili yake likamchanganya. Ndivyo ilivyo kwa picha za ngono lazima ukiangalia upate "Ukichaa" wa muda na unaweza sukumwa na kujichua sehemu zako za siri. Hiyo ni dhambi. Ni aibu sana sana mtu mwenye heshima zako kama wewe labda wewe ni meneja, mkurugenzi, mtu mwenye Elimu yako ya maana unakutwa unaangaika na kujichua sehemu zako za siri au unatumia “toys” ili kujifuraisha na kuteleza msukumo wa ngono ambao ulianzishwa na wewe kuangalia sinema au picha za watu wakifanya ngono.
NJIA ZA KUJINASUA NA VIFUNGO VYA PICHA ZA NGONO
1. Kiri dhambi yako kwa Bwana Yesu na kuomba msamaha. Baada kuomba msamaha kikamilifu basi amini kuwa umekwisha kusamehewa.
2. Baada ya hapo haribu CD, mikanda, majarida, magazeti ya ngono au vitu vyovyote vinavyopelekea wewe kupata mwanya wa kuangalia picha hizo.
AYA YA MSAADA KUHUSU KUHARIBU VYANZO VYA DHAMBI YA NGONO:
Mathayo 5:29-30, “Jicho lako la kuume likikukosesha, ling'oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum.”

3. Badilisha fikra za kingono kwa kuzikemea kwa jina la Yesu zinapokuja, huku ukikiri kwa kuzikataa na kwa kumwinua Kristo katika mawazo yako. Mawazo machafu yanapokuja ingia katika kumwabudu Mungu ukikiri ukuu na uweza wake. Au wazo chafu likija tu, anza kuimba wimbo wa kumwabudu Mungu, ghafla utaona mawazo yale yanapotea.
4. Ingia kwenye maombi na kumwambia Bwana Yesu aliondoe tatizo hilo na kukupa nguvu ya kuwa hai katika maamuzi ya kuzikataa picha hizo. Na baada ya maombi kila wakati soma Neno la Mungu. Neno linapojaa kwenye ufahamu wako linafuta taswira zote za ngono katika ufahamu wako. Zaburi ya 119:9, “Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako.”
Ukifuata hatua hizo kwa ukamilifu hakika Kristo atakuweka huru kwelikweli.
“Mwana akikuweka huru, unakuwa huru kweli kweli.” (Yohana 8:36)
Viwango vitatu pekee vya dhambi ni tama ya mwili, tama ya macho na kiburi cha maisha (1 Yohana 2:16). Ponografia haifusu kuwa kama mojawapo ya vitu tunavyostahili kuviwaza, kulingana na Wafilipi 4:8. Ponografia humvutia mtu na kuwa mazoea (1 Wakorintho 6:12; 2 Petero 2:19), na ni ya kuharibu (Methali 6:25-28; Ezekieli 20:30; Waefeso 4:19). Kutamani watu wengine katika mawazo, ambayo ni hali ya ponografia, ni dhambi kwa Mungu (Mathayo 5:28). Wakati itakuwa mazoea kwa ponografia inatambulisha maisha ya mtu, inaashiria kuwa huyo mtu hajaokoka (1 Wakorintho 6:9).
Tumefikie mwisho wa sehemu ya kwanza. Usikose sehemu ya pili KWANINI WATU WANAPENDA KUANGALIA PICHA NGONO?
Shalom,
Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo.
© Copyright 1998-2016 Max Shimba Ministries - All Rights Reserved.
No comments:
Post a Comment