Friday, November 4, 2016

YESU NI ALFA NA OMEGA, MWANZO NA MWISHO


Bwana Yesu Asifiwe,
Yesu Kristo alipokuwa akijitambulisha kwa Yohana katika kisiwa cha Patmo alisema: "Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja,Mwenyezi"(Ufunuo wa Yohana 1:8)
Yesu alitaka tujue ya kuwa ndani ya jina lake kuna nguvu za( au upako wa) Afla na tena kuna nguvu za (au upako wa) Omega. Yaani ni mwanzilishi wa jambo na pia ni mkamilishaji wa jambo. Yeye ni mwaminifu kiasi cha kwamba akianzisha kazi njema ndani yako uwe na uhakika ataikamilisha.
Je una wazo ndani yako unalojua ni la Mungu na unapata shida kuanza kulitekeleza?...itia jina la Yesu likusaidie. Je una wazo uliloanza kulitekeleza na una uhakika ni Mungu alikupa lakini linakupa kusuasua katika kulitekeleza?....itia jina la Yesu likusaidie.
Kesho (LEO) tutakuelekeza kwa nini Yesu alijiitia ya kuwa Yeye anatambulikana kama "aliyeko, na aliyekuwako na atakayekuja"!
Ubarikiwe.

No comments:

THE SEVEN PROPOSALS OF MUHAMMAD THAT WERE REJECTED

  1. Why did some women reject Muhammad's proposals? 2. Why did Muhammad continue to propose despite the rejections? Dear reader, Today ...

TRENDING NOW