Wednesday, November 16, 2016

JE, MUHAMMAD ALIROGWA?


Leo napenda Kumnukuu Mwalimu wangu Daniel Mwankemwa katika majawapo ya Makala ambayo anaelezea kuhusu swala zima la Utume wa Muhammad kwenye kipengele cha KUROGWA KWAKE.
"Kwa mujibu wa Qurani tunaona Muhammad alirogwa. Kurogwa ni hali ya mtu kuathirika na nguvu za giza yaani uchawi..
Je Nabii au Mtume wa Mwenyezi Mungu wa Kweli anaweza kurogwa?
Katika Qur’an Suratul Ban-Israel, 17:47 “ Tunajua sana, sababu wanayosikiliza, na wanaponong’ona, wanaposema hao madhalimu. Nyinyi hamfuati isipokuwa mtu aliyerogwa”
Tunasoma tukio hilo katika ufafanuzi wake uliyomo ndani ya Qur’an chapa ya nane uk.977 unaofafanua Sura ya 113-114 “Athari ya uchawi juu ya mtume (s.a.w).
Swali la pili lijitokezalo kuhusu sura mbili hizi ni kwamba kwa mujibu wa hadithi uchawi ulifanywa dhidi ya mtume (s.a.w) naye akawa mgonjwa, na ili kuiondoa athari hiyo ya uchawi Jibril (a.s) alikuja na kumpa maelekezo Mtume (s.a.w) ya kusoma sura mbili hizi. Watafiti wengi zamani na wa sasa wamelifanyia upinzani jambo hilo, kwamba ikiwa hadithi zitakubaliwa, basi mfumo wote wa sharia utakuwa ni wa kutiliwa shaka, kwa sababu kama mtume (s.a.w) aliweza kuathirika kwa uchawi, na kwa mujibu wa hadithi hizi kweli uchawi huo ulionesha athari yake, basi hatuwezi kukaidi au kukana hadi kiwango gani maadui waliweza kumfanya Mtume (s.a.w) aseme na atende mambo kwa nguvu ya uchawi, na katika mafundisho yake mambo mangapi yatoka kwa Allah na mangapi yatokana na athari ya uchawi juu yake. Si hiyo tu, bali pia wasema kuwa baada ya kuyatambua hayo kuwa ni kweli katu haitawezekana hata kule kukaidi kuwa (s.a.w) alishawishiwa kudai utume kwa mauzauza ya kinjozi kuwa alimjia malaika. Pia wanasema hadithi hizi zapingana na Qur’an, na kama ilivyo katika Qur’an kuwa tuhuma hiyo batili kwa makafiri ilivyotajwa kuwa mtume s.a.w amerogwa naye ameathirika na uchawi:
wanaposema hao madhalimu, ‘Ninyi hamumfuati isipokuwa mtu aliyerogwa’.” (17:47), lakini hadithi hizi zinathibitisha madai ya makafiri kuwa kwa kweli aliathirika na kuongozwa na uchawi……Kadri historia inavyohusika,ukweli kuwa kiasi fulani cha athari ya uchawi juu ya Mtume (s.a.w) ni hakika iliyothibiti; na kama kwa ustadi wa ubishi inawezekana kuthibitisha kuwa kweli.
Limesimuliwa jambo hilo na Bukhari, Muslim, Nasai, Ibn Majah, Ahmad, ‘Abdur Razzaq, Humaid, Baihaqi, Tabarani, Ibn Sa’d, Ibn Marduyah, Ibn Abi Shaibah, Hakim, Abd bin Humaid na Muhadithina wengine toka kwa Bi. ‘Aisha (r.a), Zaid bin Arqam, Ibn ‘Abbas kupitia silsila nyingi mno kiasi kwamba jambo lenyewe limefikia hali ya ufululizo kamili, isipokuwa kila Hadithi, yenyewe ni ripoti kamili.
Hii ni uthibitisho mwingine mzito unaoonesha kuwa utume wa Muhammad una utata. Ikiwa na wao Waislamu kwa mujibu wa hadithi hizi hawajui ni mambo mangapi Muhammad aliyoyasema yanatoka kwa Allah na mangapi aliyasema akiwa ameshinikizwa na wachawi , Je ufunuo na utume wake utakuwa umetoka kwa Mungu wa Kweli? Tafakari !!
Ndani ya Biblia Takatifu hakuma kurogwa kwa mtu wa Mungu. Hesabu 23:23 “ Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israel. Sasa habari za Yakobo na Israel zitasemwa , Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!”
Daniel Mwankemwa is a Tanzanian Helarder for the Persecuted Body of Christ. A teacher of World Religious Studies in Theological and Bibles Colleges. A presenter of the same at different Christian radio stations in the Great Lakes. He writes articles about the World Religions in both secular and religious newspapers in Tanzania, and author of the series of books in similar field. If you want to reach him feel free to do at +255 755 680101. Email: dmwankemwa@gmail.com. Skype: daniel . mwankemwa

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW