Tuesday, November 1, 2016

NENO LA MUNGU LINASEMA NINI KUHUSU SABATO? (SEHEMU YA KUMI NA MBILI)


Baada ya kujifunza sababu ya kukomeshwa kwa Sabato katika Sehemu ya Kumi na Moja, sasa tunagalie, kwanini Wakristo wanaabudu Jumapili.
Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka, Ufunuo 1:10, tunaitenga maalum kumwabudu Bwana:-
Wasabato na au Mafarisayo wa karne hii wamekuwa waliwashutumu Wakristo kuhusu siku halali ya kufanya ibada. Wakristo wanaoshika sheria ya siku ya sabato waliyo pewa wana wa Israel wamekuwa wakidai kuwa siku halali ya kufanya ibada ni Jumamosi, kadhalika, na Wakristo wanao fuata mafundisho ya Yesu na wanaofanya ibada zao siku ya Jumapili husema kuwa siku halali ya kufanya ibada ni siku ya Jumapili, na zaidi ya hapo wansema kuwa siku zote za Bwana ni halali kufanya ibada. Kama majadiliano haya yangefanywa kwa msingi wa kimaadiko, basi nina amini kabisa kwamba, kamwe kusingekuwa na mgogolo wowote, kwa kuwa Neno la Mungu liko wazi kabisa. Ni vema ifahamike kwamba, Mungu wetu anapenda sana kuona watoto wake wakimwadudu kila siku na kila saa, na wala siyo katika siku fulani au masaa fulani. Matendo 26:7 Biblia inasema, “Ambayo kabila zenu kumi na mbili wanataraji kuifikia, wakimwabudu Mungu kwa bidii mchana na usiku……”
Lakini kwa vile sisi ni wanadamu, na tunahitaji kufanya shughuli za kutupatia mkate wa kila siku, hatuwezi kufanya kusanyiko la kumwabudu Mungu kila saa, hivyo hatuna budi kuwa na siku maalumu za makusanyiko.
ANGALIZO:
Bwana Yesu, kupitia Mutme Paulo amefundisha wazi wazi kuhusu siku za kufanya makusanyiko;
UTHIBITISHO:
Warumi 14:5-6, Biblia inasema, “Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitke katika akili zake mwenyewe. Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye hula kwa Bwana…….”
Swala la siku ipi watu wafanye kusanyiko, lipo chini ya maamuzi ya watu husika, kwa kuwa siku zote ni sawa, wanaweza wakachagua siku fulani na wakawa wanafanya makusanyiko, kwa kuwa kila aadhimishaye siku huiadhimisha kwa Bwana. Kama watu wataamua kufanya makusanyiko kila siku bado ni jambo jema.
KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA
Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili, sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:9-10,13].

Wokovu wetu siku hizi uko ndani ya Kristo, siyo kwa kushika Torati ya Musa. Kuna watu wasiijua Biblia tena hawaelewi hata Agano Jipya. Hawaelewi KWA NINI Yesu alikufa. Kwa mfano wanaposema, ‘Imeandikwa katika Kutoka 20:8-11 lazima tushiike sabato!’ Je! ina maana mtume Paulo alifundisha uongo? Au alitaka kutudanganya? Au Unafikiri Biblia inajipinga yenyewe? Je! Unaamini Biblia siyo neno la Mungu? Au kwa nini watu wanapenda kujizika katika Agano la Kale?
Hivyo basi, utaratibu wa kufanya makusanyiko ya ibada siku ya Jumapili haukuanzishwa na Mfalme Constantine kama wanavyodai baadhi ya watu. Kabla ya Mfalme Constantine, Mitume katika kanisa la kwanza walikuwa wakikusanyika siku ya Jumapili; 1 Wakorintho 16:1-2 tunasoma, “Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo. Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake; kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapo kuja.” Pia Matendo 20:7-12 tunasoma, “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana kuumega mkate…..” Kwa hiyo, watoto wa Mungu wanaweza wakamwabudu Mungu katika siku zote saba, kwani Mungu hatazami siku, bali anawatafuta waabuduo halisi, ambao wanamwabudu Baba katika Roho na pia katika Kweli (Yohana 4:23-24).
SASA TUSIANGALIE SABABU ZA MSINGI ZINAZOWAPELEKEA WAKRISTO KUFANYA JUMAPILI KUWA SIKU YAO KUU YA KUSANYIKO LA IBADA

UTHIBITISHO WA KWANZA:
Mungu alikwisha iweka katika Agano la kale siku ya Jumapili kama siku ya kusanyiko ikiwa kama kiashirio cha siku ya matumaini kwa Wafuasi wa Kristo, kwani siku hii ndiyo Bwana alifufuka; Kutoka 12:16 tunasoma, “Siku ya kwanza kwenu kutakuwa na kusanyiko takatifu, na siku ya saba kutakuwa na kusanyiko takatifu…” Kwa hiyo agizo la kukusanyika siku ya Jumapili lilianza tangu Agano la kale kama kiashirio na kuthibitika katika Agano jipya.
UTHIBITISHO WA PILI:
Jumapili ni sikukuu ya malimbuko au mazao ya kwanza ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, siku ya pili baada ya sabato (on the morrow after the Sabbath) (Walawi 23:9-14), ambayo ilifanywa kama kivuli cha sikukuu ya kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye ndiye limbuko lao waliolala mauti, mzaliwa wa kwanza katika wafu (1 Wakorintho 15:20; Wakolosai 1:18).
UTHIBITISHO WA TATU:
Jumapili ni siku ya ushindi wa Bwana wetu Yesu Kristo dhidi ya kifo na mauti. Alifufuka siku hiyo na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake. Wokovu wetu unahusiana moja kwa moja na kufufuka kwa Yesu Kristo. Kufa na kufufuka ndiko kunakomtofautisha Bwana Yesu na manabii wengine. Yohana 20:1tunasoma, “Hata siku ya kwanza ya juma Mariam Magdalene alikwenda kaburini alfajili, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.” Baada ya kufufuka siku ya kwanza ya juma ambayo ndiyo Jumapili, Bwana Yesu alikuwa akiwatokea wanafunzi wake siku ya kwanza ya juma, kuashiria kuwa hiyo ni siku ya matumaini wa wanafunzi wa Yesu (Yohana 1:19, 26). Kwa wanafunzi wa Yesu, siku ya Jumamosi haikuwa siku ya matumaini kwa kuwa siku hiyo bado Bwana alikuwa kaburini, na shetani na malaika zake bado walikuwa wakitamba siku hiyo. Kwa hiyo Jumapili ina maana kubwa sana kiroho kwa wanafunzi halisi wa Yesu.
UTHIBITISHO WA NNE:
Jumapili ndiyo siku aliyokuja duniani kiongozi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika Kanisa yaani ROHO MTAKATIFU. Na huyu ndiye Bwana wa mavuno anayewapeleka watenda kazi shambani mwa Bwana. Roho Mtakatifu alikuja sawa sawa na ahadi ya Kristo, siku ya pentekoste ambayo ni Jumapili, siku inayofuata baada ya sabato (Matendo 2:1). Roho Mtakatifu alichagua kuja Jumapili ili kuanzisha siku mpya ya matumaini ya kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli (Yohana 4:23-24.
UTHIBITISHO WA TANO:
Siku ya Pentekoste yaani Jumapili, ndiyo siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza la Mitume lilianza mahubiri kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, na watu 3,000 wakaokoka na kubatizwa na kuanza kusanyiko la kwanza la ibada kanisani (Matendo 2:1-41). Torati ilipotambulishwa ilisababisha kuuawa kwa watu wengi sana, lakini neema na kweli ilipotambulishwa ilisababisha kuokolewa kwa watu wengi sana.
UTHIBITISHO WA SITA:
Wakristo wa Kanisa la kwanza la Mitume walikusanyika katika ibada siku ya kwanza ya juma yaani Jumapili (1Wakorintho 16:1-2). Mtume Paulo alifundisha katika ibada iliyofanyika siku ya kwanza ya Juma yaani Jumapili (Matendo 20:7-12). Neno linatuagiza kumfuata Paulo kama yeye anavyomfuata Kristo (1 Wakorintho 11:1), hivyo na sisi hatuna budi kufanya kusanyiko siku ya Jumapili. Pia ni muhimu kufahamu kuwa kanisa limejengwa chini ya msingi wa Mitume na Manabii na Kristo akiwa jiwe kuu la pembeni. Hivyo walichofanya Mitume na Manabii wa Yesu ndivyo nasi tunapaswa kufuata.
Lakini hata hivyo Wakristo halisi tunapaswa kujifunza Neno la Mungu na kumwomba Mungu kila siku na siyo Jumapili tu. Mitume walidumu ndani ya hekalu kila siku; (Matendo 2:46) tunasoma, “Na siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba….”
Najua kuwa narejea kwenye mambo yale yale ambayo tayari nimekwisha yaandika hapo juu. Lakini mambo hayo ni ya kimsingi. Ni lazima tuyaelewe mambo hayo pale tunapoyaangalia maisha ya watu wa Agano la Kale! Kwa kupitia Biblia nzima tunajifunza sasa juu ya Yesu Kristo na wokovu wake. Lakini kama Biblia ni neno la Mungu (na ndivyo lilivyo) kwa nini basi waopo watu wanaopinga mpango wa Mungu kupitia mwanae Yesu Kristo ili waweze kubakia katika mpango wa kale ambaop Mungu mwenyewe ameuondoa?
“Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo… Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.”
Tumefika mwisho wa Sehemu ya KUMI NA MBILI, na sasa tutaenda SEHEMU YA KUMI NA TATU
JE, UNAYAFAHAMU MAREKEBISHO YA TORATI/SHERIA KATIKA AGANO JIPYA KUPITIA CHEKECHO LA MSALABA?
********** USIKOSE SEHEMU YA KUMI NA TATU ***********
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
© Copyright 1998-2016 Max Shimba Ministries - All Rights Reserved.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW