Tuesday, September 6, 2016

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUKIRI KUWA WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAMU




1. ALLAH ASEMA WAISLAM WOTE WATAINGIA JEHANNAM
2. MUHAMMAD AKIRI KUWA YEYE NA BABA YAKE WATAINGIA JEHANNAM
3. ALLAH NA YEYE ATHIBITISHA KUINGIA JEHANNAM
Jamani huu ni Msiba katika taifa la Islam kwa kushindwa kusoma aya hii ambayo ipo wazi (Quran 40:60) http://www.quranitukufu.net/040.html .
Katika mada hii, nitawawekea aya kutoka Koran na simulizi za Muhammad ambazo zinatushuhudia kuwa, Waislam wote wataingia Jehanamu.
Hebu tumsome kwanza Allah katika aya aliyo iteremsha kwa Mtume wake Muhammad (Pbuh).
Quran 40: 60. Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.
http://www.quranitukufu.net/040.html
Mungu wa Waislam ajulikanaye kwa Jina la Allah amesema kiuwazi kabisa kuwa “wale wote ambao wanajivunia Uislam na kumuabudu Allah wataingia Motoni ili wadhalilike”
Ndugu zanguni, huu ni Msiba, tena msiba mkubwa sana katika dini na taifa la Kiislam. Allah amesha toa hukumu kwa wamfuatao na inafahamika fika kuwa, Wale wote waingiao Jehannam, hao walikuwa hawafanyi Mapenzi ya Mungu wa Biblia. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Huu ushaidi ndio tulio usoma katika Quran 40:60.http://www.quranitukufu.net/040.html
Sasa tuwasikilize na maswahiba wa Mtume Muhammad.
Simulizi:Pia imesimuliwa na Ibn Jarir, iliyosimuliwa na Abu Kurayb, imesimuliwa na Ibn Yaman, imesimuliwa na Ibn Malik Maghul, imesimuliwa na Ibn Ishaq ambaye alisema, "Kila mara Abu Maysarah anapo kwenda kulala na akiwa kitandani kwake yeye husema, 'Mimi nasikia Uchungu kuzaliwa na Mama yangu. 'na kisha anaanza kulia kwa Machozi. Alipoulizwa kwa nini alikuwa akilia, alijibu yafuatayo,' Tuliambiwa na Mtume wa Allah kwamba SISI WAISLAMU tutaingia Jehannamu, LAKINI HATUKUAMBIWA kwamba TUTATOLEWAJE HUKO JEHANNAMU NA HATUKUAMBIWA NI KIVIPI TUTATOKA HUKO'"

Mfuasi huyu wa Muhammad anaoneka kupatwa na mshtuko mkubwa, pale alipo ambiwa kuwa, Waislam wote wataingia Jehannam. Mshtuko huu umemfanya ailaani siku ambayo alizaliwa. Kitu cha kujiuliza, kwanini Allah ambaye ni mungu wa Waislam anatoa ahadi ya Jehannam na si Akhera kama wafundishavyo Waislam?
MUHAMMAD NA YEYE AKIRI KUINGIA JEHANNAM
"Wamegawanyika Mayahudi katika mapote 71, wakagawanyika Wakristo katika mapote 72 na Ummah wangu utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu)) [Ahmad, Abu Daawuud, atTirmidhiy na ad-Daarimiy]
Kama ushahid unavyo sema hapo juu kuwa Madhehebu yote ya Waislam yataingia Motoni, sasa, ni dhehebu lipi hilo ambalo halita ingia motoni?
JE, ALLAH NA YEYE ATAINGIA JEHANNAM? AMINI USIAMINI, ALLAH NA YEYE ANAINGIA JEHANNAM KAMA VIUMBE
Sasa tusome Sahih Hadith: Bukhari :: Kitabu 6 :: Juzuu 60 :: Hadith 371 Amehadithia Anas: Mtume wa Allah alisema, "watu watatupwa (Kuzimu) Jehannam na matokeo yake Jehannam itasema:" Je, kuna zaidi watu zaidi? (50.30) mpaka Allah atakapo weka mguu wake juu ya Kuzimu na Jehannam itasema, 'Qati! Qati! (Imetosha imetosha!) " Ushaidi zaidi: Bukhari :: Kitabu 9 :: Juzuu 93 :: Hadith 481, Bukhari :: Kitabu 6 :: Juzuu 60 :: Hadith 373
Sasa tumefahamu siri kubwa hapa. Kumbe na Allah ataingia motoni. Jamani, hivi huu si ndio Msiba mkubwa sana kwa dini ya Muhammad? Allah nayeye anaingia motoni.
Katika Biblia tunasoma kuwa Shetani na yeye ataingi Motoni, tena atakuwa wa Mwisho kama Allah alivyo kuwa wa Mwsiho pale Jehannam ilipo itisha watu zaidi. Sasa rejea kwenye Biblia: Ufunuo 20:10 Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele. HAPO TUNASOMA KUWA IBILISI anaingia Motoni na kuwakuta wenzake humo, kama ambavyo Sahih Bukhari imesema kuwa Allah anaingia Jehannam na kuwakuta Waislam huko.
ALLAH ANAINGIA JEHANNAM
Abu Huraira anasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):
“Pepo na Jahannam zilikuwa na mzozo, kila kimoja kikijaribu kuonyesha ule ubora wake juu ya kingine.” Basi Jahannam ikazungumza: “Mimi nimependelewa kwa kuwepo kwa wale watu wenye kiburi na nguvu ndani yangu.” Pepo ikajibu: “Mimi sijui ni kwa nini hakuna mtu isipokuwa wale dhaifu na wanyenyekevu ndio walioingizwa ndani yangu!”
Hivyo Mwenyezi Mungu akaiambia Pepo:
“Wewe ndiye Msamaha Wangu, na kupitia kwako ninatoa msamaha kwa yeyote kati ya waja Wangu.”
Halafu Yeye akazungumza na Jahannam:
“Wewe ndio ghadhabu Yangu, na kupitia kwako wewe ninamuadhibu yeyote nitakaye kumuadhibu. Kila mmoja wenu atajaa.”
“Bali Jahannam haitajaa, hivyo Mwenyezi Mungu ataingiza mguu Wake ndani yake.”
Kisha Jahannam itagutia:
“Tosha! Inatosha!”
Ndugu zanguni, ningependa mfahamu kuwa, utakapo ingia Jehannam, kutakuwa hakuna tena njia nyingine ya kutoka huko. Pale Jehannam ndio mwisho wa maisha ya walio tenda dhanb. Allah anasema kuwa, ukifanya mapenzi yake, basi wewe utaingia Jehannam. Je, kufanya mapenzi ya Allah ni sawa na kutenda dhanb? Je, Uislam ni dini ya haki, kama wanavyo sema wafundishaji wa dini hiyo? Jiulize tena, kwanini Allah anatoa ahadi ya Jehannam kwa wafuatayo mafundisho yake?
Lakini Yesu anasema haya:Yohana 14: 6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Ndugu zanguni, mwamini Yesu ili uwe na uzima wa milele. Yesu anakupenda. Yesu Ndie Njia Pekee. Yesu Ndie Uzima. Dini haita kupeleka kwa Baba aliye Mbingu, lakini Yesu anasema Yeye NDIE NJIA.
Mungu awabariki sana,
Katika Huduma Yake,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo
For Max Shimba Ministries Org
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW