Tuesday, September 6, 2016

ALLAH SIO YEHOVA "YAHUH" ( يهوه ) MWENYEZI MUNGU (SEHEMU YA KWANZA)


Huu ni msiba mwengine kwa Waislam na kwa Muhammad.
Allah katika Surat Bani Israil anasema kuwa yeye anamajina mazuri mazuri na kasema kuwa Allah ni Jina na sio Wasifa. Nilipo chunguza kwa makini katika Majina yake 99, sikuliona jina la Allah katika hayo 99. Ingia hapa na thibitsiha mwenyewehttp://www.searchtruth.com/Allah/99Names.php
Lakini cha ajabu Allah anadai katika Surat Bani Israil 110 kuwa "ALLAH" ni jina lake angalia ushahid hapa chini.
Qr. 17 Surat Bani Israil 110 (Wana wa Israil)
Sema; muombeni (Mwenyenzi Mungu) kwa (jina la) Allah au muombeni (kwa jina la) Rahman. Kwa jina lolote mnalomwita (katika haya itafaa). Kwani ana majina mazuri mazuri………
Hivi huyu Allah anamatatizo gani? Maana ameshindwa kutupa jina lake. Sasa anasema kuwa Allah ni Jina lake, na nilipo angalia kwenye yale majina 99, ALLAH HALIPO. Na hata kama tukiliweka, basi ALLAH ATAKUWA NA MAJINA 100 na sio 99. Huu ni msiba mwengine kwa Waislam.
Allah ana majina mangapi, 99 au 100?
SASA TUMSOME MUNGU WA KWENYE BIBLIA:
Mungu anayejulikana
Kutoka 6:2-3,
Kisha Mungu akasema na Musa, akamwambia, mimi ni YEHOVA;
Nami nilimtokea Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, kama Mungu Mwenyezi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Unaona tofauti ya Allah na Yehova wa kwenye Biblia? Yehova hana kizungumkuti au longa longa kama Allah anaye sema yeye ana majina mazuri mazuri lakini ameshindwa kuthibitisha kuwa YEHOVA ni jina lake.
Mwenyezi Mungu kasema kwa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo miaka 2668 kabla ya Muhammad kuwa yeye anaitwa YEHOVA, LAKINI ALLAH hakuwai sema kwenye Quran kuwa Yehova ni Jina lake. KUMBE BASI ALLAH SIO MWENYEZI MUNGU WA IBRAHIM, ISAKA, NA YAKOBO.
Sasa, kati ya Mwenyezi Mungu aliye sema katika Taurat miaka 2668 kabla ya Muhammad kuwa Jina lake ni YEHOVA, NA Allah aliye shindwa kuthibitisha kuwa yeye ni Yehova zaidi ya kusema yeye ana majina mazurimazuri tumwanini nani?

Kumbuka kuwa, katika Agano la Kale peke yake, JINA Yehova limetajwa mara 6800, Huku katika Quran HAKUNA Jina la YEHOVA hata mara moja.
ALLAH ANADAI KUWA QURAN INATHIBITISHA TAURAT, INJIL NA ZABURI. AU SIO,
HEBU TUSOME KWANZA HIYO AYA.
Surat Al Baqara 89. Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao!http://www.quranitukufu.net/002.html
Soma ushahid zaidi:
Surat Al Maida 48. Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.
SASA, KAMA NI KWELI QURAN INATHIBITISHA TAURAT, ZABURI NA INJIL,
1. Kwanini hakuna Jina la Yehova kwenye Quran?
2. Kwanini Allah hakusema yeye ni Yehova kwa Muhammad?
3. Kwanini Muhammad hakumuuliza Allah, kuhusu hili jina la Yehova lililo tajwa kwenye Taurat, Zaburi na Injili?
Ndugu msomaji, ni rahisi sana kumkama Allah kwa uongo wake, maana yeye kadai Quran inathibitisha Taurat, Zaburi, na Injil, HUKU AKISHINDWA kuthibitisha kuwa yeye ni YEHOVA.
Kumbe basi Allah sio Yehova na Quran haithibitishi Taurat, Zaburi na Injili.
Kwa ushahidi uliopo hapo juu, naweza kusema kuwa ALLAH SIO MUNGU, ALLAH SIO YEHOVA, MUHAMMAD NI MTUME BANDIA NA QURAN NI KITABU BANDIA NA KIMEJAA SHAKA.
Kama kuna Muislam anabisha basi thibitisha yafuatayo:
1. Nionyeshe Jina Yehova kwenye Quran.
2. Nionyeshe Jina Yahuh kwenye Quran.
3. Niletee aya ambayo Allah anathibistihsa kuwa yeye ni Yehova kama alivyo dai kuwa Quran inathibitisha Taurat, Zaburi na Injil Surat Al Maida 48?
4. Thibitisha kuwa Allah ni jina kwa ushaidi wa aya. Kumbe Allah anamajina 100 na sio 99.
Ni mimi Max Shimba Mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

WHY CHRISTIANITY IS BETTER THAN ISLAM?

Has Islam Improved to Become Better Than Christianity? Does Muhammad fulfill and complete the mission and purpose of Christ? Muhammad emphat...

TRENDING NOW