Friday, July 14, 2017

YESU KRISTO ALIKUJA KWA MATAIFA YOTE

Image may contain: one or more people and crowd


Bwana Yesu Asifiwe!!
Leo ningependa tujikumbushe kidogo kazi ambayo tulipewa na Yesu kristo ya kuhubiri Injili kwa mataifa yote.
Injili ikiwa na maana ya Habari Njema kama ilivyo fundishwa na Yesu Kristo, ndio Neno tulilopewa sisi Wafuasi wa Yesu kulitanganza kwa Mataifa yote.
Hebu tuendelee kusoma yale ambayo Yesu aliwaagiza wafuasi Wake wa kweli, ambao waliamini kwamba Yeye ni Mwana wa Mungu, ni Masiya.
Kueneza injili ni kazi ya wakristo wote ulimwenguni. Imeandikwa Mathayo 28:19-20 "basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho mtakatifu na kuwafundisha kuyashika yote niliyo waamuru ninyi na tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote hata ukamilifu wa dahari."
Habari njema nilazima ihubiriwe kote kabla ya kurudi kwa Yesu. Imeandikwa Mathayo 24:14 "Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote hapo ndipo ule mwisho utakapokuja."
Tumeitwa tuwe mabalozi wa Yesu imeandikwa 2Wakorintho 5:20 "Basi tuwajumbe kwa ajili ya Kristo kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu."
Kueneza injili nikuzungumza kwaniaba yake Mungu na kuutangaza ukweli wake imeandikwa Marko 16:15 na Yohana 13:35 "Akawaambia enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe... hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mikiwa na upendo ninyi kwa ninyi."
Injili ni zaidi ya kuhubiri na ushuhuda imeandikwa Isaya 60:1 "Ondoka ukaangaze kwakuwa nuru yako imekujia na utukufu wa Bwana umekuzunguka. Imeandikwa Isaya 61:1 " Roho ya Bwana Mungu I juu yangu kwa sababu Bwana amenitia mafuta ni wahubiri wanyenyekevu habari njema amenituma ili kuwanganga waliovunjika moyo kuwatangazia mateka uhuru wao na hao walio fungwa habari ya kufunguliwa kwao."
Yesu anamalizia mahubiri Yake yote kwa mfano. Bila shaka ni mfano wenye kuonyesha mahusiano kati ya wokovu na utii.
“Basi, kila asikiaye hayo maneno yangu na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba. Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa” (Mathayo 7:24-27).
Mfano wa mwisho wa Yesu si “njia ya kufanikiwa maishani” kama wengine wanavyotumia. Mada siyo jinsi ya kufanikiwa kifedha wakati mambo ni magumu, kwa kuziamini ahadi za Yesu. Hili ni hitimisho la yote ambayo Bwana Yesu alisema katika Mahubiri Yake pale Mlimani. Wale wanaotenda aliyosema ni wenye hekima nao watadumu; hawana haja ya kuogopa ghadhabu au hasira ya Mungu. Wale wasiomtii Yeye ni wapumbavu na watateseka kweli, na kupata “adhabu ya kuangamia milele” (2Wathes. 1:9).
Yesu aliwaambia wanafunzi Wake hivi: “Basi, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi … na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi …” (Mathayo 28:19-20 – Maneno mepesi kutilia mkazo).
Jina la Yesu Libarikiwe Sana
Katika Huduma yake
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.
Copyright © Max Shimba Ministries 2013

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW