Saturday, July 15, 2017

JE, MKRISTO WA LEO ANA HAKI YA KUTUNZA SHERIA NA AMRI ZA AGANO LA KALE?

Image may contain: one or more people, mountain, outdoor and text

Ili kujibi swali hili kwa ufasaha, ni vyema kujua sababu ya kutolewa hizo sheria zilizo kuwepo kwenye Agano la kale.
Jambo muhimu la kufahamu ni kwamba agano la kale lilipatiwa taifa la Israeli wala sio Wakristo, najua umesha anza kunihoji kwa maswali mengi, tulia na ujifunze Neno tamu la Mungu.
Baadhi ya sheria hizo zilikuwa za kuwafanya Waisraeli wajue jinsi ya kumtii na kumfurahisha Mungu (amri kumi za Mungu kwa mfano), baadhi yazo zilikuwa zikiwafunza jinsi ya kumuabudu Mungu (kwa ile njia ya sadaka ya kuchinja mnyama na kumtoa sadaka, JE, WEWE LEO HII UNAFANYA HIVYO KWA KUTUMIA KABILA LA WALAWI?), nyengine zilikuwa za kuwafanya Waisraeli wawe watu maalum (kama sheria za aina za mavazi na chakula). Hakuna sheria yoyote ya agano la kale inayotumika kwetu sasa. Yesu alipokufa msalabani, alimaliza matumizi ya sheria ya agano la kale (Warumi 10:4; Wagalatia 3:23-25; Waefeso 2:15).
MAKUHANI:
Neno heireus (Gk) ambalo hutafsiriwa Kuhani humaanisha mtu ambaye hutoa dhabihu na mwenye mamlaka juu ya shughuli zote zihusianazo na mwenendo mzima wa shughuli husika. Tukiachana na kuongelea makuhani wa miungu mingine, tuangalie makuhani wa Mungu aliye hai. Ili mtu awe kuhani wa Mungu ilikuwa ni lazima atoke katika familia ya Haruni (Kutoka 29:9) nje na familia hiyo hapakuwepo kuhani katika wana wa Israeli waliowahi kuwa makuhani nje na familia ya Haruni na kabla la Lawi ni wawili tu, mfalme na kuhani Melkzedeki (Mwa 14:18, Ebrania 7:1-4, 6) ambaye hajulikani ukoo wake (hana baba, hana mama, hana wazazi, hana Mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na mwana wa Mungu), mwingine ni Yesu Kristo (Ebr. 7:25-28) ambaye hutoka katika kabila la Yuda (Mw. 49:10 Luka 3:23 – 33)
Makuhani wa Mungu aliye hai walitakiwa kufanya yafutayo kati ya wana wa Israeli, kutoa dhabihu (Lawi 1:1 -7) kutunza mahali patakatifu (hema) (Hesabu 3:38), kuhakikisha taa haizimiki daima katika hema (Kutoka 27:20-21) kutunza moto katikamadhabahu usizimike daiam (Lawi 6:12-13). Kulifunika sanduku na vitu vyote vya hema safari ilipoanza (Hesa 4:5-15), kufukiza uvumba (Kut 30:7,8), kuwabariki watu (Hesabu 6:23-27), kuwatakaza (kuwapatanisha ) wenye unajisi mbele za BWANA (Lawi 15;15-31), kubaini ukomo(Law 13:1-17), na kufundisha sheria (Law 10:11)
Makuhani walipokea ZAKA kutoka kwa Walawi. Sadaka hii iliyotolewa na Walawi kwa makuhani iliitwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA (heave sacrifice) fungu la kumi la mafungu ya kumi waliyopokea walawi kutoka kwa wana wa Israeli. (Hesabu 18:28)
Makuhani (wa nyakati zote) wanaotambuliwa katika maandiko ni kama hawa wafutao, Wamegawanyika katika makundi matatu:-
1. Makuhani kabla ya sheria:
Hapa tunamuona mmoja tu Mfalme na Kuhani mkuu Melkisedeki (Mwanzo 14:18, Ebrania 7:1)
2. Makuhani wa Mungu aliye hai wakati wa sharia:
Hawa wote wa kipindi hiki walitoka katika familia ya Haruni, nje na hiyo kama tulivyojifunza hapakuwepo kuhani, Nao ni kama wafutao, (1) Haruni (Kut 31:10), Abiathari (Samuel 23:9) , Abimeleki (1Samuel 22:11), amaria (2Nyakati 19:11), Anania (Matendo 23:2), Kayafa (Matayo. 26:3), Eliazari (Hesaabu 16:39), Eli (1Samuel 1:9), Eliashibu (Nehemia 3:`1), Ezekieli (Ezekiel 1:3), Ezra (Ezra 7:11, 12), Hilkia (2Falme 22:4), Yehoiada (2Falme 11:9), Yehozadaki (Hag 1:1), Yoshua (Zeka 3:1), Maaseya (Yeremia 37:3), Pashuri (Yeremia 20:1), Fineasi (Yos 22:30), Skewa (Mdo 19:14), Seraya (2Falme 25:18), Shelemiya (Neh 13:13), Uriya (2Falme 16:10), Zabudi 1Falme 4:5), Zakaria (Luka 1:5), Zadoki (2Samuel 15:27), Zefania (2Fal 25:18)
3. Makuhani katika kanisa la Agano Jipya
Katika wakati wa Agano jopya Kristo ndiye anayetajwa kuwa ni kuhani Mkuu tena wa milele (Ebrania 3:1) Kundi jingine linalotajwa kuwa makuhani ni wakristo wote wa kweli (Ufunuo 1:5-6, 1Petro 2:9) Hatuoni majina maalumu ya kikundi cha watu maalumu waliofanywa makuhani, hata Paulo mwenyewe hakuwahi kujiita kuhani wala mtume yeyote. Hivyo katika agano jipya Kristo pekee ndiye kuhani Mkuu na haitaji msaidizi hapa duniani. Kwa hiy kitendo cha mtu yeyote kujipa ukuhani maalum tofauti na ule wa waumini wote ni kuidharau kazi ya Kristo na kuihubiri injili nyingine, itakayomletea laana (Galatia 1;6-9)
TUPO CHINI YA SHERIA YA KRISTO:
Mahali pa sheria ya Agano la Kale, tuko chini ya sheria ya Kristo (Wagalatia 6:2) ambayo ni, “Mpende bwana Mungu wako na moyo wako wote akili zako zote na nguvu zako zote. Hii ndiyo ya kwanza na amri iliyo kuu. na ya pili ni kama ya kwanza, mpende jirani yako kama nafsi yako.
Torati yote na manabii inakamilishwa katika amri hizi mbili” (Mathayo 22:37 – 40). Tukifanya mambo haya mawili tutakuwa tunatimiza yale Kristo angetaka tuyafanye, “na huu ndio upendo wa Mungu: kutii amri zake. Na amri zake si nzito” (Waraka wa kwanza wa Yohana 5:3). Kwa mtazamo, amri kumi za Mungu hazina uhusiano na wakristo. Hata hivyo, tisa katika amri kumi za Mungu zimerudiwa katika agano jipya (zote isipokuwa ile ya kuweka sabato). Kwa kwaida kama tunampenda Mungu hatutakuwa na miungu miginemila yeye. Tukiwapenda majirani zetu hatutawaua, hatutawadanganya,hatutazini nao, wala kutamani kile walichonacho. Kwa hivyo hatuko chini ya sheria ya agano la kale. Sisi ni wakumpenda Mungu na pia majirani zetu. Tukifanya mambo haya mawili kwa uaminifu wa moyo, kila kitu kitakuwa sawa.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW