Sunday, July 23, 2017

UTHIBITISHO KWAMBA MUNGU YUPO (SEHEMU YA PILI)

Image may contain: one or more people and text
Je, unafahamu kuwa mabadiliko huletwa na Mbadilishaji:
Vitu vyote hubadilika: iwe mata (matter) au nguvu (energy), wakati (time) au nafasi (space). Mwenye hekima mmoja alisema vizuri, ‘hakuna kisichobadilika isipokuwa badiliko lenyewe.” Kwa kutazama kwa macho au darubini, vitu vina uwezekano wa kubadilika na si uwezo wa kubadilika. Mchanga huhamishwa na upepo na ua ukaushwa na jua. Uwezo wa kubadilika hutoka nje ya kitu husika. Kwa kuwa ulimwengu katika ujumla wake unabadilika, basi yupo Mleta-mabadiliko nyuma yake. Kama hayupo Mbadilishaji basi ulimwengu ungebakia ulivyokua daima. Mleta-Mabadiliko Mkuu wa ulimwengu yupo, yeye habadilishwi na habadiliki. Biblia inamtaja huyo kama,"Baba wa mianga; [ambaye] kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka" (Yakobo 1:17; lingasha na Malaki 3:6; Waebrania 3:18; Zaburi 102:24-27)
NANI MWENYE MAMLAKA YA UNABII?
Lakini kwanza inabidi tukubaliane juu ya swali moja la muhimu: Biblia inadai kwamba mamlaka ya unabii inatoka kwa Mungu tu na ni uthibitisho wa uweza wake?
Kwa hili lipo jibu muafaka katika unabii wa Isaya. Katika kifungu cha 41 Mungu anazitaka sanamu na wanaoziabudu wa nyakati zile kuthibitisha kama wanazo nguvu za kiungu. Hivi ndivyo anavyoziambia:
"Haya leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema Mfalme wa Yakobo. Wayatangaze na kutujulisha yatakayokuwa; watuonyeshe mambo ya zamani, ni mambo gani, tukapate kuyatia moyoni, tukajue mwisho wake; au wamdhihirishie yatakayotokea baadaye." (Isaya 41 Mstari wa 21 - 22)
Msingi wa changamoto hii ni dhahiri: Wanaoabudu kipagani wanadai kuwa sanamu zao ni Miungu. Sawa; wathibitishe basi! Na uthibitisho unaotakiwa na Mungu mwenyewe ni kwamba sanamu zitabiri mambo yajayo na pia kutangaza 'yaliyopita', yaani kueleza jinsi uumbaji ulivyokuwa hapo mwanzo.
Katika msitari unaofuata dhana hii iko wazi sana.
"Tujulisheni yatakayokuwa baadaye, nasi tutakiri ya kuwa ninyi ni miungu...." (Isaya 41 Mstari wa 23)
Hapa Mungu mwenyewe anatujulisha kwamba kuweza kutabiri mambo yajayo ingekuwa uthibitisho wa uweza wa kiungu. Kwa zaidi ya mara moja katika sehemu hii ya unabii wa Isaya, Mungu anatangaza ya kwamba Ni yeye pekee aliye na uwezo huo; kwa kuwa Ni yeye pekee aliye Mungu, hakuna mwingine.
"Kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine, mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi......" (Isaya 46:9)
Mungu wa Israeli hapa anatangaza kwamba hakuna kitu kinachostahili kuabudiwa ila yeye; na anaendelea kusemea ishara za nguvu zake kwa maneo haya.
"...nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote." (Isaya 46:10)
Lifikirie, nani awezaye kusema, "Mapenzi yangu yatasimama..." zaidi ya Mungu? Ni nani katika dunia nzima awezaye kusema kitu kama hicho? Kusemea hili inahitaji mwenye uwezo wa kujua mambo yajayo kabla hayajatokea, lakini awezaye kuhakikisha yanaenda alivyopanga. Kwa maneno mengine, kutoa unabii utakaotimia kwa vyovyote, unamhitaji Mungu. Hakuna namna nyingine ya kuelezea.
Agano jipya linadai hivyo hivyo. Wakati Yesu alipokuwa anakaribia kuwaacha wanafunzi wake, aliwaahidia msaada wa Roho Mtakatifu katika jukumu lao la kuihubiri injili duniani. Mojawapo ya matokeo ya karama hiyo ingekuwa, "na mambo yajayo atawapasha habari yake." (Yohana 16:13); kwa maneno mengine wafuasi wangepewa ufahamu wa mambo yajayo. Kwa
vyovyote inamaanisha wasingepewa karama hiyo ya kipekee wasingeweza kuyajua. Uweza wao kutambua yajayo ndio ungekuwa ushahidi wa nguvu ya kiungu waliyotunukiwa.
Tena, katika kitabu cha mwisho cha Biblia, kifungu 1, msitari 1, inaelezwa kwamba Mungu alimpa Yesu Kristo Ufunuo, "awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi..." (Ufunuo 1:1). Ufahamu wa mambo yajayo ulitoka kwa Mungu, kupitia kwa Kristo; bila ufunuo huo watumishi wake wasingelijua lolote linalouhusu.
Hitimisho ni wazi: Biblia inasema kiuhakika ya kwamba uweza wa kutabiri yajayo ni wa Mungu pekee.
==== USIKOSE SEHEMU YA TATU ====
BIBLIA INATABIRI YAJAYO?
Tunaweza tu kuchunguza historia na uzoefu wetu kutambua kwamba wanadamu kwa jinsi walivyo, hawawezi kujua hata kidogo ya mbeleni. Kwa nini?
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW