Thursday, July 27, 2017

YESU KRISTO AMEKUPA UTAJIRI

Image may contain: one or more people


Watu wengu wanafikiri kuwa, Mungu aliwaumba ili wawe watu wa kawaida tu, la hasha, Mungu amekuumba wewe ukiwa Tajiri. Ukisoma kuhusu Adam katika Kitabu cha Mwanzo, utaona kuwa, Mungu alimuumba Adam na Eva baada ya kuumba dunia na kila kitu. Baada ya Adam na Eva kuubwa, walikabidhiwa kila kitu kilichopo hapa duniani.
Huo ni Utajiri mkubwa sana. Soma. Mwanzo 1: 28 Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.” 29 Kisha Mungu akasema, “Tazama, nawapeni kila mmea duniani uzaao mbegu, na kila mti uzaao matunda yenye mbegu; mbegu zao au matunda yao yatakuwa chakula chenu. 30 Nao wanyama wote duniani, ndege wote wa angani, viumbe vyote vitambaavyo, naam, kila kiumbe chenye uhai, chakula chao kitakuwa majani yote ya mimea.” Ikawa hivyo.
UNAONA: Mungu alimpa kila kitu Adam na Mkewe Eva. KUMBE ADAMA NA EVA WALIKUWA MATAJIRI. Je, wewe unasubiri na kungoja nini? Muamuru Shetani akurudishie mali zako zote kwa Jina la Yesu.
Mithali 3:16; (Yesu kristo Mnazareti) ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na Heshima katika mkono wake wa kushoto.
MAANA YA TAJIRI:
Tajiri ni yule mtu mwenye mali nyingi na mwenye moyo wa kusaidia wenye uhitaji na anayefaidi mali zake kwa amani kuu na sio tu kumiliki na kutawala mali nyingi. Huyo ndiye Tajiri katika Bwana anayesomeka pajini mwa uso wake hata pasipo kujua utajiri anaomiliki. Lakini ile kuwa na roho mtakatifu ni utajiri unaothihirika hadi mwilini. Kama ilivyokuwa kwa Mfalme Sulemani (2 Mambo ya Nyakati 1:15) inasema; "Mfalme Sulemani alifanya fedha na dhahabu kuwa kama mawe ule wingi wake huko Yerusalemu na mierezi akafanya kuwa kama mikuyu iliyoko shefela kwa kuwa mingi". Hii yote inatokana na kuwa na Bwana Yesu wa Nazareti ya kwamba ni utajiri utajirishao wengi na sio tu muhusika yaani ni utajiri usio binafsi na ndiyo utajiri wa kweli unaomaanishwa.
Biblia katika Waefeso 3:8-11 pia inasema kwa habari ya Mtume Paulo; “Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa UTAJIRI WAKE KRISTO USIOPIMIKA; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote, kusudi, sasa kwa njia ya kanisa, wakuu na wenye enzi wa mbinguni wapate kuitambua hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi. Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Bwana wetu."
“Na Mungu wangu atawajazeni KILA MNACHOHITAJI KWA KADIRI YA UTAJIRI WAKE KATIKA UTUKUFU, NDANI YA KRISTO YESU" (Wafilipi 4:9)
Biblia inasema Yesu wa Nazareti alifanyika maskini ili atufikie hata tulio maskini tupate kuwa matajiri na kumiliki pamoja nao. Neno kufanyika maskini haina maana alikuwa maskini, Yesu wa Nazareti ni tajiri kule kuja duniani ni kama alikuja katika umaskini kwani utajiri na ufahari wa mbinguni ukilinganisha na dunia, dunia inahesabiwa ni kama maskini, hakuna kitu huku utajiri wa kweli katika vyote u mbinguni na unapatikana tu kupitia Yesu Kristo wa Nazareti.
Biblia katika Yohana 12:6 inasema; Yuda alisema hivyo si kwa kuwa aliwajali sana maskini bali kwa kuwa alikuwa mwizi. Kama mtunza fedha, alikuwa mara kwa mara anaiba kutoka katika fedha alizokabidhiwa. – INA MAANA HUDUMA YA YESU WA NAZARETI WALIKUWA MATAJIRI KIASI AMBACHO HATA YUDA PAMOJA NA KUIBA KWAKE HAWAKUPUNGUKIWA KITU YAANI NI KAMA VILE KUCHOTA MAJI BAHARINI YATAISHAJE?.
Luka 5:29-30; Baadaye Lawi mwana wa Alfayo akafanya karamu kubwa kumkaribisha Yesu wa Nazareti nyumbani kwake. Watoza kodi wengi walikuwa miongoni mwa watu wal ioalikwa, 30 Basi baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria ambao walikuwa kundi moja wakawalalamikia wanafunzi wa Yesu wa Nazareti wakisema, “Mbona mnakula na kunywa na wenye dhambi?” – LAWI MWENYEWE ALIKUWA TAJIRI LAKINI AKATAJIRISHWA ZAIDI KATIKA KUMTUMIKIA YESU WA NAZARETI.
Matendo 28:30; Kwa muda wa miaka miwili Paulo aliishi katika nyumba ya kupangisha akiwakaribisha wote waliokuja kumwona.- MTUME PAULO ANATHIBITISHA PIA KWAMBA KUMHUBIRI YESU WA NAZARETI NI UTAJIRI KATIKA KILA IDARA.
Marko 10: 23-25; Yesu akatazama pande zote, akawaambia wanafunzi wake, “Itakuwa vigumu sana kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!”. Wanafunzi wake wakashtushwa sana na maneno hayo. Lakini Yesu akasema tena, “Wanangu, ni vigumu sana kuingia katika Ufalme wa Mungu. Ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”- KAMA WASINGEKUWA MATAJIRI WANAFUNZI WA YESU WASINGESHITUSHWA NA KAULI YAKE HIYO.
Luka 5:3-7; Akaingia katika mashua moja, akamwomba mwenye mashua, ambaye jina lake lilikuwa Simoni, aisogeze zaidi katika maji. Kisha akakaa kwenye mashua akaanza kuwafundisha, alipokwisha zungumza na watu akamwambia Simoni, “Sasa ipe leke mashua hadi mahali penye kina kirefu, kisha mshushe nyavu zenu nanyi mtapata samaki.” Simoni akamjibu, “Bwana, tumekesha usiku kucha tukivua na hatukuambulia kitu cho chote, Lakini, kwa kuwa wewe umesema, tutazishusha nyavu,” Nao walipofanya kama Yesu wa Nazareti alivyowaagiza, nyavu zao zikajaa samaki, zikaanza kuchanika! Wakawaashiria wavuvi wa ile mashua nyingine waje kuwasaidia, Mashua zote mbili zikajaa samaki hata karibu kuzama. WALIPOKUBALI KWA MALI ZAO KUTUMIKA NA YESU WA NAZARETI KWENYE HUDUMA WALIPATA FAIDA ZAIDI NA KUTAJIRIKA ZAIDI.
Mathayo 4: 18-22; Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya ziwa la Galilaya aliwaona ndugu wawili, Simoni ambaye aliitwa Petro na Andrea ndugu yake. Walikuwa katika mashua wakitupa nyavu zao baharini kwa maana wao walikuwa wavuvi. Yesu akawaambia,“Nifuateni, nami nitawafanya muwe wavuvi wa watu,” Wakaziacha nyavu zao mara moja, wakamfuata. Alipoendelea mbele kidogo, aliwakuta ndugu wengine wawili, Yakobo na Yohana, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo wakishona nyavu zao; akawaita, Wakaacha nyavu zao mara moja, wakamfuata. WALIKUWA WANAFANYA KAZI NA WAVUVI HIVYO WALIKUWA MATAJIRI LAKINI WALIONGEZWA ZAIDI WALIPOKUBALI KUMTUMIKIA YESU WA NAZARETI.
Mathayo 8:13-14; Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wake amelala akiwa ana homa. –WANAFUNZI WAKE WALIKUWA MATAJIRI WANAMILIKI NYUMBA NA MALI ZINGINE.
Mathayo 10:8-10; Waponyeni wagonjwa, wafufueni wafu, watakaseni wenye ukoma, wafukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure, Msichukue dhahabu, wala fedha wala sarafu za shaba katika mikanda yenu. Msichukue mikoba ya safari, wala koti la pili, wala viatu, wala fimbo: kwa maana mfanyakazi anastahili riziki yake. INA MAANA WANAFUNZI WA YESU WA NAZARETI WALIKUWA MATAJIRI KULE KUWA NAYE, YESU WA NAZARETI HAKUTAKA KATIKA KAZI YAKE WABEBE WALIVYONAVYO KWENDA NAVYO KAZINI BALI KATIKA HUDUMA YAKE RIZIKI ZILIPATIKANA KULE KULE WALIKOKWENDA KUHUDUMIA.
Luka 6:12; Siku moja Yesu alikwenda milimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. – USIKU KUCHA MASAA KUMI NA MBILI YESU ALIOMBA ILI MUNGU AMUCHAGULIE WANAFUNZI 12 INA MAANA KILA MMOJA ALIMUOMBEA KWA SAA MOJA, AKACHAGUA, YUDA - MHASIBU, PETRO, ANDREA, YAKOBO NA YOHANA WAFANYA BIASHARA YA SAMAKI, Mungu alijua kuna suala la uchumi katika huduma ili iwafikie wengi hivyo alimwekea msingi katika uchaguzi wa wanafunzi ili kuwe na mpango bora kiuchumi pia.
Waebrania 6:1; Basi sasa tutoke katika yale mafundisho ya msingi kuhusu Kristo, tupige hatua kufikia ukamilifu katika kuelewa kwetu. Hatupaswi tena kuwaeleza ninyi yale mafundisho ya msingi kuhusu kutubu na kuacha matendo yaletayo kifo, na kuhusu kumwamini Mungu – INA MAANA UKISHAKUMJUA NA KUFUATA MAFUNDISHO YAKE NA KUMWAMINI KUNA HATUA ZAIDI KUFIKIA UKAMILIFU ILI KUONYESHA TUNAELEWA NI PAMOJA NA KUJUA HAKI ZETU ZILETWAZO NA MAFUNDISHO NA IMANI KATIKA KRISTO AMBAPO NI PAMOJA NA MAFANIKIO NA UTAJIRI AMBAVYO HATA KWA WASIOAMINI VITASHUHUDIA KWAMBA KUNA HABARI NJEMA PIA UTAJIRI NA MAFANIKIO NDANI YA YESU WA NAZARETI.
Marko 10:29; Yesu mwenyewe anathibitisha suala la utajiri ndani yake kwa kusema, "Kweli nawaambieni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au mama, au baba, au watoto au mashamba kwa ajili yangu na kwa ajili ya Habari Njema, hata hivyo atapokea mara mia zaidi wakati huu wa sasa nyumba, ndugu, dada, mama, watoto na mashamba pamoja na mateso; na katika wakati ujao atapokea uzima wa milele - UTAJIRI, MAFANIKIO NA BARAKA ZINGINE NI GUARANTII 100% UKIWA NA YESU WA NAZARETI.
Yohana 21:3; Simoni Petro aliwaambia,"Nakwenda kuvua samaki" Nao wakamwambia, "Nasi tutafuatana nawe" Basi, wakaenda, wakapanda mashua, lakini usiku huo hawakupata chochote – BAADA YA YESU WA NAZARETI KUFUFUKA WALIPOENDA KUVUA SAMAKI HAWAKUPATA CHOCHOTE (UKAME) JAPOKUWA WALIKUWA NA YESU WA NAZARETI MIAKA MITATU YA HUDUMA, NA HII NI KWA KUWA WALIKAA PASIPO UWEPO WAKE WALA ROHO MTAKATIFU ALIKUWA HAJAACHIWA BADO KWAO MPAKA ILIPOFIKA SIKU YA PENTEKOSTE.
Yohana 21:5-6; Basi, Yesu akawauliza; "Vijana, hamjapata samaki wowote sio?" Wao wakamjibu, "La Hatujapata kitu." 6 Yesu akawaambia, "Tupeni wavu upande wa kulia wa mashua nanyi mtapata samaki" Basi, wakatupa wavu lakini sasa hawakuweza kuuvuta tena kwa wingi wa samaki. – NDIPO WAKAPATA SAMAKI WENGI, UWEPO WA YESU WA NAZARETI KUPITIA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA NI BARAKA NA SIO UHABA, HUWEZI KUWA NAYE USIFANIKIWE, USIONGEZWE NA KUTAJIRIKA.
Yohana 1:38-39; Basi, Yesu aligeuka, na alipowaona hao wanafunzi wanamfuata, akawauliza, "Mnatafuta nini?" Nao wakamjibu "Rabi (yaani Mwalimu), unakaa wapi?", Yesu akawaambia, "Njoni, nanyi mtaona" Hao wanafunzi wakamfuata, wakaona mahali alipokuwa anakaa, wakashinda naye siku hiyo.Ilikuwa yapata saa kumi jioni.-YESU WA NAZARETI ALIKUWA NA MAKAO WAKATI AKIFANYA HUDUMA, NYUMBA TENA SIO SEHEMU MOJA NA HATA WANAFUNZI WAKE WALIKUWA NA NYUMBA ZAO NA MATAJIRI.
Luka 8:2-3; Pia wanawake kadhaa ambao Yesu alikuwa amewatoa pepo wabaya na kuwaponya magonjwa, waliandamana naye. Hao ndio akina Maria (aitwaye Magdalene), ambaye alitolewa pepo wabaya saba; Yoana, mke wa Kuza, mfanyakazi mkuu wa Herode; Susana na wengine kadhaa. Hao wanawake walikuwa wakiwatumikia kwa mali zao wenyewe. – HATA WANAWAKE WALIKUWA WAKIWAHUDUMIA KWA MALI ZAO WENYEWE INA MAANA KULIKUWA KUNA UTAJIRI KATIKA KUWA NA YESU WA NAZARETI NA KUMTUMKIA.
Yohana 12:3; Basi, Maria alichukua chupa ya marashi ya nardo safi ya thamani kubwa, akampaka Yesu miguu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba yote ikajaa harufu ya marashi.- MARASHI HAYO YALIKUWA NA THAMANI YA DINARI 300 NA DINARI 300 NI KAMA MSHAHARA WA SIKU 300 KWA MTU MMOJA ENZI HIZO KATIKA SERIKALI YA KIRUMI, HIVYO MARASHI YALIKUWA YA THAMANI NA INAONYESHA JINSI YESU WA NAZARETI ALIKUWA WA THAMANI YA JUU AKIISHI KAMA TAJIRI MKUBWA HAPA DUNIANI NA NDIO MAANA HABARI ZAKE ZILIWAFIKIA HATA WAFALME.
Yohana 19:23-24; Askari walipokwisha msulubisha Yesu, walizichukua nguo zake, wakazigawa mafungu manne, fungu moja kwa kila askari. Walichukua pia na kanzu yake; kanzu hiyo ilikuwa imefumwa kwa kipande kimoja tu, bila mshono. Basi, hao askari wakashauriana: "Tusiipasue, ila tuipigie kura itakuwa ya nani." Jambo hilo lilifanyika ili yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: "Waligawana mavazi yangu, na nguo yangu wakaipigia kura." Basi,ndivyo walivyofanya hao askari. – HATA MAVAZI YA YESU WA NAZARETI YALIKUWA NA THAMANI, HAIWEZEKANI ASKARI KUIKATA NGUO KATIKA VIPISI NA KISHA KUGAWANA NA KILA MMOJA KURITHIKA NA ILIYOBORA ZAIDI WAKAIPIGIA KURA PASIPO KUIHARIBU, HII INATOKANA NATHAMANI YAKE.
Marko 6:37; Yesu akajibu akawaambia wapeni ninyi chakula (walikuwa wapata wanaume 5,000) wakamwambia, Je’twende tukanunue mikate ya dinari 200 ili tuwape kula? –HIVYO WALIKUWA TAYARI NA UWEZO ULIKUWEPO WA KUWALISHA WANAUME 5,000 KUTOKA KATIKA MFUKO WA HUDUMA, YESU WA NAZARETI NI TAJIRI NA HAKUISHI KWA SHIDA NA KATIKA UMASKINI KAMA WENGI WANAVYODHANI ILA KULE KUKAA DUNIANI UKILINGANISHA NA MBINGUNI UTAJIRI WA DUNIA NI KAMA HAKUNA KITU.
Mathayo 17:27; Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoano ukatwae samaki yule wa azukaye kwanza na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako. – KWA YESU WA NAZARETI UHITAJI WA PESA HAIKUWA KITU CHA KUFIKIRIA ALIKUWA TAJIRI KIASI AMBACHO CHOCHOTE ALICHOTAKA ALIKIPATA KWA KUCHUKUA PESA HATA MDOMONI MWA SAMAKI.
Hivyo nimeyathibitisha hayo kutoka katika Biblia ili tupate kujua ya kwamba wewe si maskini bali ni tajiri kwatika Yesu.
JE, UPO TAYARI KUWA TAJIRI?
Mwaka huu ni mwaka wa baraka kwako. Pokea sasa utajiri katika Jina la Yesu.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW