Sunday, September 10, 2017

KWANINI ALLAH ALIUMBA UCHAWI?

Image may contain: 1 person
NINI MAANA YA UCHAWI?
"Uchawi ni makubaliano baina ya mchawi na Jinni akishurutishwa mchawi kufanya mambo ya haramu au ya shirki, na baada ya kufanya hayo, Jinni anashurutishwa kumsaidia na kumtii mchawi huyo kwa kila anachotaka."
Al Azhari ambaye ni mtungaji wa kamusi maarafu ya kiarabu iitwayo “LisanulArab” amesema:
“Neno “Uchawi”, kwa kiarabu “As Sihr”, maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na Shaytwaan na kwa msaada wake (Shaytwaan)”, na akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.”
Ama Swahaba Ibni 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema.
"Uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki."
Hayo ni katika kamusi za lugha.
Huu ni Msiba Mkubwa sana katika taifa la Muhammad. Mara nyingi Wakristo wamekuwa wanajiuliza, hivi, uchawi ulitokea wapi na mwanzo wake ni nani?
Leo Quran inakujibu kuwa Uchawi ULIUMBWA NA Kuteremshwa na Allah, HIVYO BASI wachawi nambari moja ni Waislam.
Nafahamu unafikiri kuwa Max Shimba anawasingizia Waislam au sio?
Hapa inafaa tufahamishane kuwa ushirikina ni jambo ovu linamtia mtu motoni. Kwenda kwa wachawi, wapiga ramli ni katika ukafiri na ushirikina.
Hebu soma Ushahid huu wa Quran:
SURAT TAHA: 73. Hakika sisi tumemuamini Mola wetu Mlezi ili atusamehe makosa yetu na uchawi ulio tulazimisha kuufanya. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora na Mwenye kudumu zaidi.
Kwenye Surat Taha ayat 73 kama ilivyo teremshwa Makka kwa Muhammad na kutafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani inasema kuwa ALLAH ANAWALAZIMISHA WAISLAM KUUFANYA UCHAWI. Huu ni msiba ndugu zangu. Swali la kujiuliza, hivi, tokea lini Mungu akawa mchawi? Hivi huu uchawi ulio teremshwa na Allah unafaida gani kwa Wislamu?
Hebu tuingalie tafsir ya pili ya Surat Taha aya 73 kama ilivyo tafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin inasema: 73. Kwani hakika sisi ni wenye kusimama juu ya Imani kumuamini Mola wetu Mlezi wa Haki, ili atufutie madhambi yetu yaliyo pita, na atusamehe huku kushughulikia uchawi ulio tulazimisha tujifunze na tuufanye! Na Mola wetu Mlezi ni Mbora wa malipo kuliko wewe, akit'iiwa; na ufalme wake na uwezo wake kulipa unadumu zaidi kuliko wako.
1. Inasema kuwa Waislam wanalazimishwa kujifunza Uchawi.
2. Inasema kuwa Waislam wanalazimishwa kuufanya Uchawi.
Ndugu msomaji, leo sina mengi ya kusema maana umesoma Mwenyewe kutoka Quran kuwa Allah aliteremsha uchawi na kawalazimisha Waislam wajifunze na kuufanya uchawi.
Nawashauri Wakristo wenye marafiki wa Kiislam wawe makini, maana huyo rafiki yako anaweza kuwa ndiye anaye-kuroga kwasababu kalazimishwa na Allah kufanya hivyo.
Nimenukuu quran aya ya 2:102 na maelezo/ufafanuzi wake hapo chini kutoka tafsiri mbili za quran (Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy na Tafsiri ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani). Aya hii na maelezo/ufafanuzi wake inaonesha mambo yafuatayo:
(a) Uchawi umeteremshwa na malaika wa Allah
(b) Kuna wachawi wa kiislam.
(c) Uchawi ni amali ya ukafiri
Pia, kwa mujibu wa Sahih Bukhari juzuu ya 4, Kitabu cha 54, Hadithi namba 490 na Sahih Bukhari, juzuu ya 7, kitabu cha 71, hadithi namba 658; Muhammad alirogwa na akazurika na uchawi. Kisa cha mtume kurogwa na kuzurika na uchawi pia kinasimuliwa katika quran Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy ukurasa wa 977 na 978.
MASWALI
(a) Ikiwa uchawi ni ukafiri, Kuna uhusiano gani kati ya Allah na ukafiri mpaka ateremshe uchawi?
(b)Mtume Muhammad alirogwa na wachawi wa kiislam au wachawi wengine?
(c) Mtume Muhammad alirogwa na uchawi ulioteremshwa na malaika wa Allah au uchawi mwingine?
(d) Mtume au nabii gani mwingine alirogwa na akaathirika na uchawi kama Muhammad?
Quran 2:102 inasema:
Wa Attaba`ū Mā Tatlū Ash-Shayāţīnu `Alá Mulki Sulaymāna Wa Mā Kafara Sulaymānu Wa Lakinna Ash-Shayāţīna Kafarū Yu`allimūna An-Nāsa As-Siĥra Wa Mā 'Unzila `Alá Al-Malakayni Bibābila Hārūta Wa Mārūta Wa Mā Yu`allimāni Min 'Aĥadin Ĥattá Yaqūlā 'Innamā Naĥnu Fitnatun Falā Takfur Fayata`allamūna Minhumā Mā Yufarriqūna Bihi Bayna Al-Mar'i Wa Zawjihi Wa Mā Hum Biđārrīna Bihi Min 'Aĥadin 'Illā Bi'idhni Al-Lahi Wa Yata`allamūna Mā Yađurruhum Wa Lā Yanfa`uhum Wa Laqad `Alimū Lamani Ashtarāhu Mā Lahu Fī Al-'Ākhirati Min Khalāqin Wa Labi'sa Mā Sharaw Bihi 'Anfusahum Law Kānū Ya`lamūna
Quran 2: 102(Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy) inasema: Wakafuata yale waliofuata mashetani wakadai kuwa yalikuwa katika ufalme wa (Nabii) Suleiman; na Suleiman hakukufuru, bali mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi (waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani na uchawi) ulioteremshwa kwa malaika wawili, Harut na Marut, katika (mji wa) Babil. Wala Malaika hao hawakumfundisha yoyote mpaka wamwambie: “ Hakika sisi ni mtihani (wa kutazamwa kutii kwenu); basi usikufuru.” Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waweza kumfarikisha mtu na mkewe (na mengineyo). Wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa mambo hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza ambayo yatawazuru wala hayatawafaa Na kwa yakini wanajua kwamba aliyehiari haya hatakuwa na sehemu yoyote katika akhera. Na bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia (starehe za) nafsi zao (za Akhera). Laiti wangalijua, (hakika wasingefanya hivi). (Tafsiri ya Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy ukurasa 25-26)
Nanukuu Maelezo/ Ufafanuzi wa quran 2: 102
Suleiman aliyetajwa hapa ni nabii, Mayahudi wanamwita Nabii Suleiman kuwa ni mfalme aliyepata ufalme kwa uchawi, si Mtume. Basi na hawa wachawi wa kiislam humnasibishia Nabii Suleiman hizo ilimu zao za uchawi. Basi Mwenyezi Mungu anamkanushia haya. Na aya hii yaonesha wazi kuwa
(a) uchawi ni amali ya ukafiri na
(b) kuwa mchawi hawezi kumdhuru mtu ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na
(c) kuwa mchawi mwenyewe anadhurika kwa uchawi wake. Na anataja hapa Mwenyezi Mungu kuwa nyuma huko kabisa katika zama za mfalme
Qura 2:102.(Tafsiri ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani) Inasema:
Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Su leiman. Na wala Suleiman hakukufuru, bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi, na yaliyo teremshwa kwa Malaika wawili, Haaruta na Maaruta katika Baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayo wadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walicho jiuzia nafsi zao laiti wangelijua.
Mungu awarehemu na kuwasamehe ndugu zetu wote wanao fanya Uchawi. Maana Biblia inasema kuwa WACHAWI WOTE WATAINGIA JEHANNAM. 1 Samweli 15 : 23 .......... dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.
Ndugu msomaji, mpokee Yesu aliye hai na upate uzima wa milele. Dini haita kusaidia kitu, maana sasa unaelewa kuwa, ni dini ambayo inakufanya uwe mchawi na kuachana na upendo wa Mungu.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW