Sunday, September 10, 2017

NAKALA ZA QURANI ZATUPWA KATIKA MTARO WA MAJI TAKA

Image may contain: outdoor
Nakala takribani 500 za kitabu kitukufu cha Qurani القرآن الكريم zimegunduliwa katika mtaro wa maji taka katika mji wa Taif, nchini Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa Afisa wa kamati ya kukuza na kufadhili mambo ya Qurani alisema tukio hilo liliripotiwa na mwanafunzi ambaye aliona msahafu katika mtaro wakati anaelekea nyumbani kwao maeneo ya Al-salama ambayo ni moja ya wilaya ya mkoa wa Taif.
Kampuni ya kuhudumia mifereji ya maji ilifungua na kukuta nakala zipatazo 500 za Qurani. Hii si mara ya kwanza kwa Quran Mtakatifu kukutwa imeharibiwa katika Saudi Arabia.
Mapema mwaka huu, Afisa wa gerezani la mkoa wa Al-Haer alitusi Qurani kiasi cha kupelekea maandamano katika sehemu mbalimbali za Saudi Arabia.
Kunajisiwa kwa Quran katika nchi ya Saudi Arabia ambayo ni jicho la Uislamu kumeibua hisia hasi katika ulimwengu wa Kiislamu.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW