Tuesday, May 16, 2017

USIOGOPE: YESU ANATULINDA

Image may contain: text
“Kwa sababu ameweka upendo wake juu yangu, mimi nitamwokoa pia. Nitamlinda kwa sababu amelijua jina langu.”—Zaburi 91:14.
Baba mwenye upendo hawaandalii tu watoto wake mahitaji yao bali pia hujitahidi kuwalinda. Kwa kawaida, anajitahidi kuwaokoa wanapokabili hatari. Ndugu mmoja anakumbuka jambo fulani lililotukia alipokuwa mvulana mdogo. Alipokuwa akirudi nyumbani na baba yake baada ya kuhubiri, walifika mahali penye kijito. Kijito hicho kilikuwa kimefurika baada ya mvua kubwa kunyesha asubuhi. Ili kuvuka kijito hicho walihitaji kuruka kutoka jiwe moja kubwa hadi lingine. Akiwa mbele ya baba yake, mvulana huyo mdogo aliteleza na kutumbukia mara mbili ndani ya maji. Alishukuru sana wakati baba yake alipomshika kwa nguvu begani na kumwokoa asizame! Baba yetu wa mbinguni anatuokoa kutoka katika ulimwengu huu mwovu ulio kama mafuriko yenye nguvu na kutoka kwa mtawala wake, Shetani. Kwa kweli, Mungu ni Mlinzi bora zaidi unayeweza kupata.—Mathayo. 6:13; 1 Yohana 5:19.
Shalom.
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW