Wednesday, May 17, 2017

ROHO MTAKATIFU NA KAZI ZAKE KWETU SOMO LA 7

Image may contain: food
MATUNDA YA ROHO MTAKATIFU NI YAPI?
Matunda ya Roho Mtakatifu ni matokeo ya kuwepo kwa Roho Mtakatifu katika maisha ya Mkristo. Biblia inaeleza wazi kwamba kila mtu hupokea Roho Mtakatifu wakati yeye anaamini katika Yesu Kristo (Warumi 8:9, 1 Wakorintho 12:13; Waefeso 1:13-14).
Wagalatia 5:22-23 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi juu ya mambo hayo hakuna sharia.” Matunda ya Roho Mtakatifu ni matokeo ya kuwepo kwa Roho Mtakatifu katika maisha ya Mkristo.
UPENDO:
Kwa nini upendo ni wa kwanza na sehemu muhimu ya tunda la Roho Mtakatifu?
Upendo wa Mungu hubadili Maisha yetu. Tunabadilishwa tunapoelewa upendo wake. Tuna kuwa na uwezo wa kupenda mara tunapopokea upendo wake. Mungu mwenye upendo hutuandaa kuwapenda wengine, hata adui zetu.
Vipengele vingine vya tunda la Roho Mtakatifu sharti vizingirwe na upendo wa Mungu ili vilete mantiki.
FURAHA:
Je; ni nini sababu ya furaha aletayo Roho?
Kuuelewa na kuukubali upendo wa Mungu kwetu, Kafara yake, Rehema yake, Msamaha wake, Ahadi na baraka zake. Hicho huleta furaha idumuyo, haidhuru hali zetu.
Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.” (Warumi 14:17)
AMANI:
Je; Amani aletayo Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa namna gani?
Amani hiyo ni matokeo ya kuwekwa huru dhidi ya dhambi zetu kwa imani katika Yesu kristo.
Amani hiyo hutufanya tuwe wenye amani na kutusukuma Zaidi kuwa na amani na kila mtu (Warumi 12:18).
“Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.” (Warumi 5:1)
UVUMILIVU:
Je; uvumilivu pamoja ukiwa na tunda la Roho mtakatifu hutofautianaje na uvumilivu bila tunda la Roho Mtakatifu?
“Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.” (14:12)
WEMA:
Je; tunawezaje kuuonja wema wa Bwana?
Neno wema limetumika mara 10 katika Biblia. Mara 8 kati ya hizo huzungumza namna mungu anavyotutendea (2 Samuel 22:36; Zaburi 18:35; War. 2:4; War. 11:22; Efeso 2:7; Kolosai 3:12; Tito 3:4; 1P. 2:3) na mara zingine 2 huzungumza kuhusu tunda la Roho ndani yetu (2 Korintho 6:6; Wagalatia 5:22).
Namna njema ambayo kwayo Roho hutuongoza kuwatendea wengine huakisi namna ambavyo Mungu ametutendea sisi kwa kuonesha wema wake.
“ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.” (1 Petro 2:3)
FADHILI:
Je; unawezaje kueleza maana ya fadhili?
Fadhili ni upendo katika vitendo.
Tunaonyesha fadhili tunapopenda tunafanya kazi kwa faida ya wengine. Fadhili ni “kufanya kilicho sahihi, liwalo na liwe.”
Hii ni sehemu ya vitendo ya tunda la Roho.
“Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.” (Luka 6:35)
UAMINIFU:
Kwa nini uaminifu ni muhimu katika Maisha ya ukristo?
Mungu ni mwaminifu kwa asili. Hawezi kuvunja ahadi zake (2 Timotheo 2:13).
Yesu ni “shahidi aliye mwaminifu” (Ufunuo 1:5). Tunaakisi tabia ya Yesu kama tukiwa waaminifu kwa agano letu na Mungu na waaminifu katika mahusiano yetu na wengine kwa kazi ya Roho.
Mkristo wa kweli daima ni mwaminifu.
“Umtumaini Bwana ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.” (Zaburi 37:3)
UPOLE:
Je; Kuna tofauti gani kati ya upole na uoga au soni?
Muoga au mwenye aibu aweza kuonekana kama mpole, lakini anaweza kuwa mwenye kujivuna au jeuri.
Kiburi si sehemu ya upole. Yesu alituambia: “mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo” (Mathayo 11:29).
Kuiamini nguvu ya Roho wa Mungu ambayo hutenda kazi ndani yetu hutufanya tuwe wapole, wanyenyekevu na wavumilivu.
KUWA NA KIASI:
Je; ni katika maeneo gani ya Maisha napaswa kuboresha kiwango changu cha kiasi?
Kiasi ni kuwa na uwezo kamilifu wa kujizuia dhidi ya mambo mabaya na kutumia mambo mazuri kwa uzania sahihi.
Kiasi huhusisha si tu vyakula na vinywaji. Lazima iguse kila Nyanja ya Maisha yetu.
Hilo ni tunda la Roho. Kwa nguvu zake, tunaweza kulionyesha tunda lake kila mahali, katika kila nyanja ya Maisha yetu : upendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili, uaminifu, kiasi.
“Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.” (Mithali 16:32)
Maisha ya Kikristo ni vita vya mwili ulio wa dhambi dhidi ya asili mpya iliotolewa na Kristo (2 Wakorintho 5:17). Kama binadamu viumbe tulioanguka, sisi bado tumenazwa katika mwili wa dhambi na kwamba tunathami mambo ya dhambi (Warumi 7:14-25). Kama Wakristo, tuna Roho Mtakatifu kuzalisha matunda yake ndani yetu na nguvu za Roho Mtakatifu zinapatikana kwa kushinda matendo ya mwili (2 Wakorintho 5:17; Wafilipi 4:13).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW