Friday, July 14, 2017

JE! WAJUA KWANINI NENO USIOGOPE LIMETAJWA MARA 365 KATIKA BIBLIA TAKATIFU?

Image may contain: 1 person, text and outdoor


Ipo sababu kubwa tunapo sema kuwa, Biblia ni Neno la Mungu, na huwa hatubahatishi. Biblia imekamilika na haina shaka ndani yake bali ni mwongozo thabiti kwa wanao taka kwenda kuishi na Mungu Mkuu, yaani Yesu Kristo.
Mwaka una siku 365 na katika kila siku, Yesu Mungu Mkuu (Tito 2:13) anakwambia usiogope, maana yupo pamoja nawe.
Isaya Mlango 43: 1 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, USIOGOPE, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
Yesu Mungu Mkuu yupo mahali pote na kwa wakati wote "omnipresent" na hii sifa ni ya Mungu pekee na si ya kibinadamu. ( Mathayo 18:20 ) “Kwa kuwa walipo wawili watatu, wamekusanyika kwa jina langu, mimi nipo papo hapo katikati yao”. Mwenye uwezo wa kukaa mahali pote ni Mungu.
Zaburi Mlango 23: 4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.
Mathayo : Mlango 10: 28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.
Leo nawakumbusha tu kuwa, "USIOGOPE YESU MUNGU MKUU YUPO PAMOJA NAWE"
Pokea ulinzi wa Yesu na USIOGOPE TENA MAANA YESU YUPO PAMOJA NAWE.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW