Sunday, September 10, 2017

JE WEWE UNAISHI KWA NEEMA YA YESU KRISTO AU SHERIA ZA MUSA NA SABATO?

Image may contain: text


SABATO SI SIKU
Upo ushahidi wa kutosha katika Biblia unaoonyesha kwamba sabato si siku katika juma. Bwana anapoongelea kuhusu safari ya wana wa Israeli anasema:
Kwa hiyo nalichukizwa na kizazi hiki, nikasema, Siku zote ni watu waliopotoka mioyo hawa ... hawataingia rahani mwangu. (Ebr. 3:10-11).
Pia imeandikwa: Maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; na hapa napo, Hawataingia rahani mwangu. (Ebr. 4:4-5).
Katika maandiko haya Mungu anasema kwamba, kutokana na kukasirishwa na uasi wa wana wa Israeli kule jangwani, alimua kwambahawataingia kwenye raha aliyokuwa amewaandalia. Neno rahani hapa, au kwa Kiingereza rest, ndilo hilohilo sabato. Ndiyo maana hapo juu katika Waebrania 4:4-5, anahusisha siku ya saba na kuingia rahani.
Lakini hebu tujiulize maswali yafuatayo ili tuweze kupiga hatua zaidi.
• Je, Israeli walipokuwa jangwani kwani hawakuwa wakitunza Sabato kama siku? Jibu ni ndiyo, waliitunza. Biblia inasema:Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu mara dufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa. Akawaambia, Ndilo neno alilonena BWANA, Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa BWANA ... (Kutoka 16:22-23).
• Kama basi waliitunza sabato, iweje tena Mungu aseme, ‘Hawataingia rahani mwangu’? Kama ingekuwa ni kumwuliza Mungu, mtu ungesema, “Bwana, unasemaje hawataingia rahani mwako wakati kila siku ya saba wanapumzika?” Hii ni ishara ya wazi kwamba sabato hasa si kupumzika au kutofanya kazi kimwili katika siku ya saba. Sabato ni jambo jingine tofauti na siku ya saba. Iko sabato halisi ambayo siku ya saba na kupumzika kwake vilikuwa ni kivuli chake tu.
• Jambo jingine la kujiuliza ni kwamba, japo ni kweli kwamba wale ambao Mungu alisema hawataingia rahani mwake walifia wote jangwani, lakini walikuwapo wengine wengi walioingia, yaani watoto wao. Sasa je, hao walioingia waliipata hiyo raha (Sabato)?
Mtu anaweza kujibu, Ndiyo, maana sote tunajua kuwa hata wakati alipokuja Bwana Yesu, alikuwa akifundisha mara nyingi kwenye masinagogi 'siku ya Sabato'. Kwa hiyo, mtu anaweza kusema, ‘Ndiyo, waliingia kwenye raha au kwenye sabato.’
Hebu sasa tumsome Mtume Paulo:
Kwa hiyo mtume Paulo anafundisha kuwa ni jambo la udanganyifu kuwafundisha watu washike siku ya Sabato. Kwa sababu ya wokovu wetu ndani ya Kristo (Wakolosai 2:11-15) Paulo anasema, “Basi, MTU ASIWAHUKUMU ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.” (mstari wa 16).
Paulo anaanzisha mstari huo na neno hili, “Basi.” Kwa nini? Kwa sababu ya mistari 14 na15, “(Yesu) akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani; akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.”
Walikuwepo watu wa dini – kama tunavyojua kwa kusoma hasa Matendo na Wagalatia – waliotaka wakristo waishi chini ya sheria, yaani, kushika mambo ya nje ya torati; kwa mfano watahiriwe au washike ‘siku’ ya torati. Paulo anafundisha hapo kama mtu akisema, “Lazima ushike sabato ili kumpendeza Mungu au kuokoka ‘kweli’, usimruhusu akuvute chini ya sheria hiyo na humjali kama anakuhukumu! Tunasoma kwenye Matendo 15 na Wagalaia juu ya watu waliojaribu kupotosha njia ya Ukweli kwa kuwalazimisha waumini wayarejee mambo ya torati ya Musa. Ni vivyo hivyo siku hizi. Wasabato wanawahukumu wakristo kwa sababu hawashiki siku ya sabato! Paulo aliwaonya wakristo juu ya watu wa dini kama hao hao!
Hayo ni mafundisho ya Agano Jipya. Hatuwezi kusema au kufundisha kwamba ni lazima tukusanyike siku ya Sabato (jumamosi). Kama fulani akifundisha hivyo anawadanganya watu, sawasawa na maneno ya Paulo. Au je, tunataka kusema Paulo alifundisha uongo? Au tunataka kutumia mstari mmoja dhidi ya mstari mwingine kana kwamba Biblia siyo neno la Mungu? Mistari yote ina muktadha (mazingira) yake! Nani aliyekupa wewe ruhusa na mamlaka kupendelea mstari mmoja na kuudharau mstari mwingine au kutokujali kabisa? Hakika hiyo haitokani na Mungu.
Ndugu msomaji, ningependa ufahamu kuwa wokovu wetu sisi Wakristo upo ndani ya Yesu Kristo, siyo kwa kushika Torati ya Musa kama ambavyo WASABATO “SDA" wanavyo amini, SIKU HAINA UWEZO WOWOTE ULE KATIKA MAISHA YAKO, LAKINI YESU NDIE MUWEZA WA KILA KITU NA YEYE NDIE ALIYEIUMBA HIYO SIKU YA SABA YA JUMA.
Wasabato hutumia hii aya kumhukumu Mtume Paulo kuwa alifundisha uongo Kwa mfano wananukuu, ‘Imeandikwa katika Kutoka 20:8-11 lazima tushiike sabato!’ Sasa, inamaana Mtume Paulo alikuwa anafundisha uongo alipo sema tuna haki ya kumtukuza na kumwabudu Mungu siku yeyote ile?
Mtume Paulo anatueleza kiuwazi kuwa, ni vigumu sana kumfuata Yesu kwa asilimia 100 na wakati huo huo unafuata sheria za Musa. Hebu tusome jinsi Mtume Paulo alivyo ianza baruka yake kwa Wagalatia “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeukia injili ya namna nyingine. Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya kristo. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe.”
Hapa ni wazi kuwa Mtume Paulo alikuwa anaongea juu ya waumini ambao walikuwa wanataka kufuata sheria ya Musa. Ndio maana tunamsoma Mtume Paulo akitumia lugha au maneno makali kwa Wagalatia.
Hii tabia ya watu kupenda kushika sheria za Musa tunaiona kwa kanisa la SDA ambalo wanafuata sheria za Musa na kusahau kuishi kwa Imani kama jinsi ambayo Biblia inatufundisha katika Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Paulo alihuzunishwa sana, kwa sababu anasema wazi hivi “…..sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini KUYAREJEA TENA MAFUNDISHO YA KWANZA yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena? MNASHIKA SIKU, na miezi, na nyakati, na miaka.”(Wagalatia 4:9,10).
“Maana yale YASIYOWEZEKANA kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa DHAIFU kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma “YESU KRISTO” Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ILI HAKI YA TORATI YATIMIZWE NDANI YETU sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.” (Warumi 8:3,4).
Kwa hiyo, mtume Paulo anasisitiza, “Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au SABATO.”
Ningependa ufahamu kuwa kiwango cha haki ya Injili ya Yesu Kristo KIPO JUU ZAIDI ya kiwango cha Torati ya Musa. Imeandikwa, “torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.” Yohana 1:17:
SWALI KWAKO MSOMAJI, wewe unaishi kwa uongozi wa NEEMA YA YESU KRISTO AU UONGOZI WA TORATI YA MUSA?
Kumbuka kuwa sheria ambayo ipo nje yako haiwezi kuishinda neema ya Yesu ambayo inaishi ndani yako.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo Mungu Mkuu na mwokozi wetu.

1 comment:

Unknown said...

Nimeipenda hiyo ,,,,,mwalimu wa masomo haya naomba uendelee kufundisha kupitia hiyo blog yako

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW