Sunday, September 10, 2017

WAKRISTO WA KWANZA WALIKUTANA JUMAPILI NA SIO SABATO DHAIFU

No automatic alt text available.
Ni siku gani ya Sabato, Jumamosi au Jumapili? Je, Wakristo wastahili kuitunza hii siku?
Sabato (kwa Kiebrania: שבת, shabbāt, yaani pumziko kwa Kiswahili) ni siku ya pumziko ya kila juma katika Uyahudi kwa ujumla na hasa katika nchi ya Israeli.
Kumekuwa na maswali mengi sana kutoka imani tofauti kuhusu hii siku ya Jumamosi. Wafuasi wa dini na imani zote wanao fuata Torati wanajiuliza kuhusu Sabato, je, Mwenyezi Mungu anaikubali Jumamosi tu kama siku ya ibada? Katika Agano Jipya, tunajifunza kuwa siku ya Jumapili inaitwa siku ya kwanza ya juma na walio amini walikusanyika katika siku hii ya Jumapili. Matendo 20: 7 Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.
Siku ya kwanza ya juma ni Jumapili na hii ni siku ambayo walio mwamini Yesu walikusanyika na kuabudu. Huu ni ushaidi wa kuonekana kwa macho ambao Wakristo wanaabudu Jumapili tokea Karne ya kwanza.
“Hata sabato ilipokwisha, kupambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi.” (Mathayo 28:1). “Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma…”. (Marko 16:9).
Bwana Yesu alifufuka kutoka wafu katika siku ya kwanza ya Juma. Zaidi ya hapo, tumesoma nyaraka za Mtume Paulo zikionyesha kuwa kuwa Wakristo wa kwanza walikuwa walikusanyika siku ya kwanza ya Juma, yaani Jumapili. “Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kuumega mkate, Paulo akawahutubu…” (Matendo 20:7). “Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja…” (1 Wakor.16:2).
Zaidi ya hapo, hatusomi na wala hakuna amrisho ndani ya Agano Jipya kuhusu wauminia yaani Wakristo ni lazima wakutane kwenye hii siku ya kwanza ya Juma, “Jumapili”, lakini tunao mfano wa siku ambayo Wakristo wa kwanza “Kanisa la Kwanza wakati wa Pentekoste”, na utamaduni huo wa kuabudu Jumapili unaendelea mpaka sasa. Zaidi ya hapo, ukisoma Agano Jipya kwa umakini utaona kuwa WAKRISTO WA KWANZA HAWAKUKUSANYIKA SIKU YA SABATO, nikimaanisha kuwa, hakuna aya ambayo inasema moja kwa moja kuwa Wakristo walikusanyika siku ya Sabato au kulikuwa na utamaduni au desturi au mila au sheria inayo walazimisha kukutana siku ya Sabato.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

1 comment:

Unknown said...

Thanks. Be blessed for the brief explanation on worshipping on Sunday. Bt it too short, can expose it in detail?

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW