Friday, July 14, 2017

WEWE NI ROHO, UNA NAFSI NA UNAISHI NDANI YA MWILI

Image may contain: text




Mwanadamu ni Roho, ana Nafsi na anakaa ndani Ya Mwili.

Ukisoma 1Wathesalonike 5:23 Inatusaidia kuona maeneo yote matatu Ya UTU Wa MTU;
"Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi NAFSI ZENU na ROHO ZENU na MIILI YENU Mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo"
Hapa Unaona Nafsi, Roho Na Mwili Vimetajwa.
ROHO YAKO
Hii ndio sehemu ya uhai wako ulipo. Hii ndiyo iliyo chanzo cha Uhai Wako. Hii ndiyo wewe halisi. Ikitoka kwenye mwili wanakuita MAREHEMU..."MWILI WA MAREHEMU FULANI" Hii Ni kwa sababu "ROHO NDIYO ITIAYO UZIMA NA WEWE NI ROHO" Soma Ayubu 32:8, Ayubu 33:4, Mithali 20:27
NAFSI YAKO
Hii nayo imebeba sehemu Kuu Tatu; NIA/ AKILI (Mind), HISIA (Emotions And Feelings) Na UTASHI (Will). Soma Mathayo 11:28-29, Zaburi 103:1-2, Mithali 23:7a
MWILI WAKO
Ni nyumba yako inayohifadhi Roho Na Nafsi Yako.
Soma Mwanzo 2:7, Mwanzo 3:19b, Wagalatia 5:17-21, 24, 1Thesalonike 4:4.
Utendaji wako kama mtu unategemea na "UZIMA ULIONAO ROHONI"
Aliyekombolewa kwa Damu Ya Yesu [ALIYEOKOKA] Na Kujaa Neno La Mungu; Huwa anaanza kufanya chochote toka ROHONI- NAFSINI- MWILINI.
Lakini yule ambaye "AMEKUFA ROHONI" Kwa Sababu Ya Dhambi na kutokuwa na Ushirika Na Mungu; Anaishi kinyume chake. Anaishi toka MWILINI- NAFSINI- Na Roho haina kazi maana imekufa "KIUTENDAJI" Imebakiza tu "UHAI WA KUWA NDANI YA MWILI" Lakini haina uwezo wa KUSHIRIKI MICHAKATO YA KIMAAMUZI NA UTENDAJI!
Mtu ambaye HAJAOKOKA "ALIYEKUFA KIROHO" anaweza "KUZINI NA KAHABA" Huku "ANAJUA KABISA NI MWATHIRIKA WA VVU", Hajali maana "ANAENDESHWA TOKA MWILINI" na kwenye NAFSI anachukua tu uamuzi wa Kutenda Hiyo Dhambi.
Mtu ambaye "AMEKUFA KIROHO" anaweza kwenda kumchukua Mme/ Mke wa rafiki yake uu hata ndugu yake wa Damu, japo anajua HAIPENDEZI KWA WANADAMU NA NI DHAMBI KWA MUNGU lakini kwakuwa "ROHO YAKE HAIFANYI KAZI" Bado anajikuta ametenda ingawa anajua ubaya na madhara ya hilo.
Haishangazi kwa Mtu ambaye "ROHO YAKE IMEKUFA" Kufanya dhambi yoyote na wala haoni tatizo... Atavuta Sigara ilhali yeye ni DAKTARI MSOMI NA ANAJUA ATHARI ZAKE... Atakunywa Pombe ilhali anaelewa ATHARI ZAKE... Atatembea [Atazini] na Wanafunzi ambao ni kama wajukumuu zake kwa Umri; Wala haoni tatizo lolote, maana "ROHO YAKE IMEKUFA NA HAINA MAAMUZI KATIKA UTENDAJI" anatumia MWILI TU NA NAFSI YAKE BASI!
Barikiwa sana.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW