Friday, July 14, 2017

KWANINI TUNAOMBA KATIKA JINA LA YESU? SEHEMU YA PILI

Image may contain: cloud, sky, text and outdoor


Mbona uombe katika jina la Yesu?
Mbona si Budha, au Allah, au mwalimu mwingine shupavu wa dini, au nabii au Muhammad?
Kuomba katika jina la Yesu ni kukubali malipo ya dhambi zetu ambazo Kristo alilipa pale msalabani ili tuweze kuifikia uwepo wa Mungu. Kama vile Wayahudi hawangeingia Patakatifu bila gharama ya damu (kwa Yom Kippur), ndivyo mwenye dhambi hawezi kuingia katika uwepo wa Mungu bila damu iliyomwagika ya Yesu Kristo. Ni kupitia kwa kifo chake, kuzikwa kwake, kufufuka kwake, na kupaa kwake mbinguni ndipo tunaweza kuwa na uhusiano wa Baba-Mwana pamoja na Roho Mtakatifu. Mwenye dhambi asiyekuwa na mwokozi hana tumaini la msamaha wa dhambi.
“… Vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo…kwa sababu Kristo hakuingia patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali
aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu” (Waebrania 9:22,24), na “Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu” (Waebrania
10:19).
Hiyo ndio sababu tunasogelea kiti cha enzi cha Mungu katika jina la Yesu. Tunaomba kwa kuwa yeye ni mwadilifu. Ni kama kumwambia Mungu, “Mungu, siombi kwa sababu ya jinsi nilivyo ama kwa ajili ya uzuri wangu. Naomba kwa sababu Yesu alisema nije kwako na kukuambia amenituma. Alisema utajibu
maombi yangu kwa ajili yake, wala si kwa ajili yangu.”
Ghala La Baba:
Ukienda sokoni na kununua vyakula vyote unavyohitaji nyumbani mwako, na mahitaji mengine. Ukaenda kulipa ukiwa na vikapu kumi vilivyojaa vyakula, na vitu vingine ulivyonunua. Muuzaji akahesabu gharama ya vitu vyote ulivyonunua.
Unagundua kwamba vimegharimu pesa kiasi kikubwa. Muuzaji anakuangalia kwa mshangao na kukosa kukuamini. Tuseme labda kiasi cha pesa unazohitajika kulipa ni $5000. Kisha
unamwambia huyu muuzaji, “Hebu nipe cheti hicho niweke sahihi.” Anapigwa butwaa na kukuuliza, “Uweke sahihi? Kwani unafikiri wewe ni nani, mwenye soko?” Alafu unamjibu, “La hasha, kwa hakika mimi si mwenyewe, lakini baba yangu ndiye mwenye soko. Mimi ni mwanawe wa pekee. Nitaurithi mali
yake yote.”
Yesu alimaanisha hivyo alipotuambia tuombe kwa jina lake. Yote ya Mungu Baba pia ni ya Mwanawe wa pekee. Yesu ndiye mwenye soko, akiwa pamoja na Baba yake. Amemwambia Baba yake kwamba tunaweza kuweka sahihi cheti katika jina lake. Baba anaheshimika kujibu maombi yako katika jina la Yesu, kama vile Kristo mwenyewe angeweza kuomba. Muumini ameshikamanishwa na Kristo kiasi cha kwamba kuomba kwetu ni kuomba kupitia kwa Roho wake aliye ndani yetu. Huu ni ukweli wa ajabu!

Kutumia Fimbo Ya Mungu:
Tumetazama Mwanzo 17, na “fimbo ya Musa ya Mungu.” Tumeona kwamba fimbo yetu ni imani katika jina la Yesu. Katika Marko 16:17, Yesu ametuambia tutumie jina lake hata kwa kuwatorosha mapepo.
Inasisimua kuona wanafunzi wa Yesu wakitenda yale Yesu alihubiri.
Baada ya Pentekote, Petero na Yohana walienda hekaluni kuomba. Yesu amerudi kwa Baba, lakini Roho Wake sasa anakaa ndani yao. Wakiwa nje ya hekalu, Petero na Yohana walikutana na kilema ambaye alikuwa akiomba pesa kutoka kwa wale waliokuwa wakienda hekaluni kusali. Petero aliwaza akiwa
ameshurutishwa na Roho wa Yesu aliyekuwa ndani yake:
“Petero, tumia fimbo yako. Tumia jina langu. Mwombe Baba. Ona muujiza.” Petero, kwa msukumo, akamwambia yule kilema, “Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, simama uende.”
(Tazama Matendo 3:1)
Kwa hivyo, kwa mara ya kwanza mmoja wa wanafunzi kumi na wawili wa Yesu alifanya kitu. Waliamini maneno ya Yesu na kutumia jina lake. Walisogelea eneo la miujiza. Baadaye Petero na Yohana walipoulizwa na viongozi wa Wayahudi jinsi huyu kilema alivyoponywa, kwa furaha walijibu, “na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote” (Matendo 3:16). Iweke imani yako katika jina la Yesu na Mungu ataweka jina lake, na nguvu zake, katika imani hiyo.
Barikiwa sana
Ni mimi Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW