Friday, July 14, 2017

JINSI YA KUOMBA KWA IMANI, SEHEMU YA TATU

Image may contain: one or more people, sky and text


Kuna vikundi viwili vya watu ambao wana imani aina mbili tofauti. Kikundi cha kwanza ni cha “kuona ni kuamini.” Katika Yohana 20:25 Tomaso alisema, “Mimi nisipoziona…mimi sisadiki.” Ilimlazimu kuona Bwana aliyefufuka kabla kusadiki kwamba Bwana alifufuka. Tomaso alikuwa na imani iliyojengwa kwa hisia. Tunasema, “Bwana nipe ushindi, nami nitasadiki kuwa ninayo ushindi huo.” HIYO SI IMANI! Hiyo ilimsababisha Yesu kusema sadiki kwamba tayari umepokea, ndipo utapata.
Yesu hakusema Tomaso alifanya vizuri. Alisema, “wa heri wale wasioona, na hawahitajiki kuona -wakasadiki” (Yohana 20:29, maneno ya mwandishi). Hiyo ni imani iliyo sambamba na maandiko.
Tunahitaji kuondoka katika eneo la hisia, na kuingia katika eneo la Bibilia. Hapa ndipo tunagundua kwamba “imani ni kuona yale ninayotumaini.” Nikiwa na hakika kwamba nimepokea yale nimeahidiwa na Mungu, basi NITAONA ninayoyatumaini! Nasema tena, hii ni imani inayookoa. Hukumwona Yesu akifa
na kufufuka siku ya tatu; uliamini neno tu. Hiyo ndio hakikisho uliyohitaji. Uliliamini neno, alafu ukamwona Yesu na kupata msamaha wake. Imani ni kufanya kama kwamba imetimika, wakati ambapo haijatimika bado, nayo itatimika!
Imani ya Mwenye Ukoma
Katika Luka 17, tunaona wenye ukoma 10 waliomwendea Yesu wakipaaza sauti kwa kusema, “Ee Yesu, Bwana Mkubwa uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.” Mwenye ukoma aliyetakasika ni lazima ajionyeshe kwa kuhani ili
ithibitike kwamba ameponywa kweli. Yesu aliwaambia waende kwa kuhani kabla kuponywa kwao. Je, kama wangalisema, “Bwana, hatuwezi kwenda kwa kuhani, kwani hatujaponywa bado”? Yesu, kwa kweli alisema, “fanya kama kwamba imetimika, ijapokuwa haijatimika bado, nayo itatimika.” Waliamini na kuelekea hekaluni, na “walipokuwa wakienda, walitakasika”…Kisha akawaambia, “imani yako imekuponya.”
Ushindi Na Imani
Waraka wa Kwanza wa Yohana 5:4 inafananisha ushindi katika maisha na imani kwa Mungu. “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.” Kwa hivyo, ushindi umepatikana tayari! Unao ushindi kwa kuamini kwamba
Yesu tayari ameshinda (1Yohana 5:5).
Labda utasema, “Je, unamaanisha kwamba nina ushindi dhidi ya kila shida kwa kuamini tu kwamba ninao ushindi?” Hiyo ni kweli! Ni kweli kabisa! Unasema, “Siamini hayo!” La, nawe hutapata ushindi kamwe!
Amini hayo, nawe utapata ushindi! Imani ni ushindi! Yesu Kristo tayari ameshinda adui wote: yaani ulimwengu, mwili, na shetani (Waebrania 2:14; Wakolosae 2:14,15; 1 Yohana 3:8,4:4). Huna vita vingine vya kushinda. Yesu alishinda vyote miaka 2000 iliyopita. Ukiyaamini hayo, kuyasimamia imara, na kuyadai, basi ushindi wake utakuwa wako!
Imani hii ya “Mungu ameshashinda vita” hutupa wokovu. Ni lazima uamini kwamba Mungu ameshatupatia wokovu ndani ya, na kupitia kwa Yesu Kristo. Aliyepotea dhambini lazima amjie Mungu na kupokea yale Mungu ametenda kwa kutubu dhambi, na kusema “Ahsante Yesu, ishatendeka.” Jinsi ulivyopata wokovu ndivyo utakavyopata ushindi na mwongozo wa kila siku. Ukiwa na imani, basi una bayana. Kwa hitaji lolote, amini kwamba ni yako, nawe utapata.
Mungu akuzidishie katika maombi na kuamini kwako.
“Bwana, tufundishe kuomba kwa imani, tukidai yaliyo yetu katika Kristo.”
Michango
1. Tazama Luka 11:9-13
2. Sura ya 4, “Can a Christian Lose His Salvation?” inaongea kuhusua kuwa na hatia na msamaha kwa kinaganaga.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW