Neno la Msingi:
Zaburi 101:3
“Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.”
“Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.”
Watu wengi wameanguka katika mtego huu wa Ibilisi na kujikuta wakifanya mambo ya "AIBU" wanapokuwa sehemu zao za Siri iwe ni chumbani au bafuni. Wanaume wamejikuta wakipiga punyeto (Mastubation) na Wanawake wakijisaga ( wanatumia mikono yao na viungo vyao vingine kama njia ya kujikidhi hali zao za tamaa mbaya waliloziamsha wao wenyewe). Haipaswi kamwe kuwa hivyo. Biblia inasema tusiyachochee wala kuyaamsha "mapenzi" mpaka yatakavyoona yenyewe (Wimbo ulio bora 2:7, 3:5).
Naomba tufuatane pamoja kwenye somo hili muhimu sana ambalo litakuweka huru mbali na "utumwa wa fikra za kingono"
1. MAANA YA PICHA ZA NGONO
Neno PICHA ni kivuli cha mtu, watu, kitu n.k. PICHA si kitu halisi bali ni kivuli chake. Unaweza ukapewa PICHA ya mtu lakini usifahamu urefu wake au ni mfupi kiasi gani lakini sura yake ukawa umeiweka katika kumbukumbu yako. NGONO ni kitendo cha mtu, watu kufanya kitendo cha kujamiana (Tendo la Ndoa) na pia ni ile hali ya kuwa uchi wa mnyama. Kuangalia picha za ngono ni kitendo cha kuangalia watu wakifanya Matendo ya kujamiana iwe kwa njia ya asili, kinyume na maumbile au kufanya na wanayama. Kitendo hicho huleta kuchochea tamaa ya miili kiasi ambacho watu wengine hufanya mambo ya "AIBU" katika nyumba zao (Warumi 1:24-28). PICHA za NGONO zimeenea kila mahali kwa sasa, kwenye simu yako unaweza ukakutana na "uchafu" wa namna hiyo. Wahindi wao picha za ngono huziita "kachumbali" na unaweza ukamkuta Mhindi amekaa na familia yake anaangalia "kachumbali" wanadai inanogesha utamu wanapofika kitandani. Huko ni kujidanganya Mungu hakumletea Adamu PICHA ya NGONO bali alimletea mke ambaye watashirikiana naye kwenye Tendo Takatifu (Mwanzo 2:18, 21-25). Wakati mmoja Mfalme Daudi wakati watu wake wa vita wamekwenda vitani yeye akawa yuko ghorofani anaangalia "PICHA LIVE" ya NGONO mwanamke alikuwa akioga matokeo yake yakawa ni kufanya kitendo chenyewe na kuamua kumuua mume wa Bathsheba (2Samweli 11:2-27).
“Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho. Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?”………..
Kile kitendo cha Daudi "kuona" lilikuwa kosa kubwa la kiufundi katika akili yake likamchanganya. Ndivyo ilivyo kwa PICHA ZA NGONO lazima ukiangalia upate "UKICHAA" wa muda ukajikuta umeng'ang'ania sabuni au ndizi ukiwa unapiga punyeto. Ni aibu sana sana mtu mwenye heshima zako kama wewe labda wewe ni meneja, mkurugenzi, mtu mwenye Elimu yako ya maana unakutwa unaangaika sabuni, godoro au toy la jinsia ya kiume.
USIKOSE SEHEMU YA PILI
Shalom
No comments:
Post a Comment