Thursday, April 20, 2017

AONAVYO MTU NAFSINI MWAKE NDIVYO ALIVYO


KUMBUKA KUWA MAWAZO NI MBEGU NA JARIBU KUZINGATIA UNACHOKIPANGA KWENYE NAFSI YAKO.
Mithali 23:7 "AONAVYO MTU NAFSINI MWAKE NDIVYO ALIVYO" Je wewe unaona nini? unaona kushinda au kushindwa? unaona umasikini au utajiri?
Fikiri kabla hujanena na kuonyesha kutokujua kwako. Imeandikwa, Mithali 15:28 "Moyo wa mwenye haki hufikiri atakavyojibu bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya."
Lazima tuwe na nidhamu katika mafikara yetu na kufikiri mambo mema kwani hapo ndipo chanzo cha mambo yote. Imeandikwa, Marko 7:21-22 "Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya na uasherati. wivu, uuaji, uzinzi, tama mbaya ukorofi, hila, ufisadi, kijicho matukano, kiburi, upumbavu." Mithali 23:7 sayema "Maana aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo. akauambia, haya, kula, kunywa, lakini moyo wake hauwi pamoja nawe."
Lazima tufikiri mambo mema ndipo maneno yetu na matendo yetu yawe ya busara na yenye kusaidia. Imeandikwa, Wafilipi 4:8 "Hatimaye ndugu zangu mambo yo yote yaliyo ya kweli yo yote yaliyo staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema, ukiwapowema wo wote ikiwapo sifa nzuri yo yote, ya tafakarini hayo."
Tuwe na mafikara kama ya Kristo. Imeandikwa Wafilipi 2:5 "Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu."
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

WAS MUHAMMAD PROPHESIED IN THE BIBLE?

SURAH 61:6 Muslims believe that the coming of Muhammad was foretold in the Bible. For centuries, Muslims have tried to find predictions of t...

TRENDING NOW