Tuesday, April 18, 2017

JE, MELKIZEDEKI NA YESU NI MTU MMOJA? (SEHEMU YA PILI)


Kitabu cha Mwanzo mara kwa mara kinatutambulisha kwa kirefu maisha ya mwanzo wa jamii na sifa zetu ambazo kitabu kinatuonyesha. Bali Melkizedeki anatokea bila kutamkwa, bila taarifa za wazazi wake, na kupotea kwenye maelezo bila ya kutazamiwa.
Sasa ngoja nianze kuwafananisha na au linganisha Melkizedeki na Yesu:
JERUSALEM:
1. Melkizedeki alikuwa mfalme wa Salem (Yerusalemu). Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. (Mwanzo 14:14 - 18).
2. Yesu yeye ni mfalme wa Yerusalem mpya. Ufunuo 21: 1 Kisha nikaona mbingu mpya na dunia mpya; maana mbingu ya kwanza na dunia ya kwanza zilikwisha kutoweka na bahari haikuwapo tena. 2 Ndipo nikaona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi harusi aliyepambwa kwa bwana wake.
KUHANI MKUU:
1. Melkizedeki, ambaye jina lake linamaanisha "mfalme wa haki," alikuwa mfalme wa Salemu (Yerusalemu) na KUHANI MKUU zaidi wa Mungu (Mwanzo 14: 18-20; Zaburi 110: 4, Waebrania 5: 6-11, 6: 20-7: 28).
2. Yesu ni kuhani mkuu milele. Waebrania 6:20 inasema, "alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa KUHANI MKUU hata milele kwa mfano wa Melkizedeki."
MFALME WA AMANI:
1. Melkizedeki ni mfalme wa Salem (Amani). Waebrania 6:20....alikuwa mfalme wa Salemu (Yerusalemu)
2. Yesu nayeye ni mfalme wa Amani. Mfalme wa Amani (Isaya 9: 6)
HANA MWANZO WALA MWISHO:
1: Melkizedeki hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake; bali amefananishwa na mwana wa Mungu" (Ebrania 7: 1,3)
2. Yesu Kristo alikuwepo milele yote“...Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, Mimi niko.” (Yohana 8:58). “Na sasa, Baba, unitukuze Mimi pamoja Nawe, kwa utukufu ule Mimi niliokuwa nao pamoja Nawe kabla ya ulimwengu kuwako.” (Yohana 17:5)
SIFA YA UKUHUNI YA MELKIZEDEKI NA YESU ZINAFANANA. WOTE HAWAKUTOKA KATIKA KABILA LA LAWI.
Wayahudi wanahoji:'Ninyi Wakristo tuambieni kama huyu Yesu sasa anaweza kuwa kuhani wetu mkuu, mwenye kutoa maombi yetu na matendo yetu kwa Mungu. Lakini kuhani inampasa ukoo wake ujulikane, akithibitishwa katoka kabila ya Lawi. Na kwa vyovyote, ninyi wenyewe mnakiri Yesu alitoka kabila ya Yuda (Ebrania 7: 14). Tunasikitika, kwetu sisi Ibrahimu ndiye Kiongozi wetu mkuu na mfano (wa kuufuata) (Yohana 8: 33, 39), hatutamheshimu huyu Yesu'.
Kwa hiyo Paulo anajibu:
‘Lakini mkumbukeni Melkizedeki. Taarifa ya kitabu cha Mwanzo imetengenezwa ili kuonyesha kwamba kuhani huyu mkuu hakuwa na ukoo wa babu yeyote; naye Masihi kwa pande zote mbili anakuwa mfalme na kuhani, ambaye ukuhani wake ni wa kufuata mfano mzuri wa Melkizedeki (Ebrania 5: 6; Zaburi 110: 4).
MWANA WA MUNGU.
Yesu alikuwa na Baba (Mungu)-MWANA WA MUNGU (tazama Mathayo 1, Luka 3 na Yohana7: 27).
Melkizedeki katika Waebrania 7 aya ya 3 "alifananishwa na Mwana wa Mungu"; Waebrania 7:3 ....., bali kama alivyo Mwana wa Mungu, yeye adumu kuwa kuhani milele.
"Ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki", Yesu (Ebrania 7: 15) naye amefanywa kuhani mkuu' kwa mfano wa Melkizedeki"(Ebrania 5: 5,6).
Lugha ya Waebrania kumhusu Melkizedeki haiwezi kuchukuliwa tu kwa maneno jinsi yalivyo. Ikiwa Melkizedeki kwa maneno halisi hakuwa na Baba wala mama, basi mtu pekee anaweza kuwa ni Mungu mwenyewe; ni mtu wa pekee asiye na mwanzo (1 Timotheo 6: 16; Zaburi 90: 2). Lakini taarifa hii haikubaliani na Ebrania 7: 4:"Angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu" na vile vile kwa ukweli wa kwamba watu walimuona Melkizedeki (ambapo Mungu hawezi kuonwa) na alimtolea dhabihu Mungu. Ikiwa ameitwa mtu huyo, basi huyo ilimpasa kuwa na wazazi halisi. Yeye kuwa,"hana Baba, wala Mama, na wazazi" kwa hiyo inabidi kutaja ukweli kwamba ukoo wa babu na wazazi wake taarifa zao hazikuandikwa. Taarifa za wazazi wa Malikia Esta hazikuandikwa, kwa hiyo maisha yake ya nyuma yameelezewa kwa namna hii. Mordekai"alimlea …..Esta, binti wa mjomba wake: kwa kuwa hana Baba wala Mama …… nao walipokufa Baba na Mama yake, yule Mordeklai alimtwaa kuwa binti yake yeye"(Esta 2: 7).
Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki (Zaburi 110:4)
Je, Melkizedeki na Yesu ni mtu mmoja? Hoja inaweza kufanywa kwa njia yoyote. Kwa uchache sana, Melkizedeki ni aina ya Kristo, anayeonyesha huduma ya Bwana kabla yake.
Ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki", Yesu (Ebrania 7: 15) naye amefanywa kuhani mkuu'kwa mfano wa Melkizedeki"(Ebrania 5: 5,6).
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW