Sunday, April 23, 2017

MAMLAKA ULIYONAYO UNAPOLITUMIA JINA LA YESU KRISTO!

Image may contain: text
Hebu tuyatafakari maneno yafuatayo aliyoyasema Kristo juu ya mamlaka yaliyomo katika Jina lake.
Biblia inasema, “Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu
-watatoa pepo;
-watasema kwa lugha mpya;
-watashika nyoka;
-hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa;
-wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya”. (Marko 16:17-18).
Hebu na tuangalie kwa undani zaidi baadhi ya ishara alizosema zitatokea tukilitumia Jina la Yesu Kristo.
“Kwa Jina Langu watatoa pepo”
Yesu Kristo alitaka sisi tumwaminio tujue ya kuwa kwa jina lake tuna mamlaka juu ya mapepo. Ni vizuri ufahamu ya kuwa kwa kuwa umemwamini Kristo rohoni mwako kama Bwana na mwokozi wako, basi, una mamlaka yakuwatoa pepo mahali walipo! Ukijua pepo yuko mahali Fulani, una uwezo nanmamlaka ya kumtoa mahali hapo kwa jina la Yesu Kristo, naye atatii!!
Jina la Yesu Kristo libarikiwe sana maana ni ngome imara – walio na shida hulikimbilia na kupata pumziko na msaada!!
Barikiwa sana katika Jina la Yesu Kristo.
Shalom,
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW