Friday, April 7, 2017

UNAWAFAHAMU MALAIKA WAKUU SABA WA MUNGU "ARCHANGELS OF GOD? (SEHEMU YA SITA)

Image may contain: 1 person, indoor


Malaika katika Agano Jipya:
Tunaona ya kwamba Malaika walimhudumia Yesu wakati alipokuwa katika nchi (duniani) (Mt. 4:11, Lk. 22:43). Malaika alimtokea Yusufu na kumwarifu habari za kuzaliwa kwake Yesu (Mt. 1:20, Lk 1:26-38). Malaika walikuwepo katika ufufuo wa Yesu (Mt 28:2-8; Yn. 20:12). Na walizungumzia wakati wa kupaa kwakeYesu Kristo (Mdo 1:9-11). Malaika wanatoa huduma za Kiroho kwa watu wa Mungu (Ebr. 1:14; Mt. 18:10; Mdo 5:19; 8:26; 10:3; 12:7; 27:23). Malaika hufurahi mwenye dhambi anapotubu (Lk. 15:10).
Katika Agano Jipya, Kristo kama mwanadamu bado alitenda kama mtu aliye mdhihirisha na kumfunua Mungu. Na alitenda kwa ukamilifu akifuata asili ya Mungu na tabia ya Mungu. Kama Mpatanishi kati ya Mungu na Wanadamu, kumwona Yesu ni sawa na kumwona Mungu, na kusikia na kumtii Yesu ni kumsikia na kutii Mungu. Maneno aliyozungumza hayakuwa maneno yake mwenyewe bali maneno ya Mungu yaliyotoka kwa Mungu. (Yn. 14:8-10)
Vyeo mbalimbali vya Jeshi la Mbinguni
Malaika wana vyeo, uwezo na nguvu zinazotofautiana katika utendaji wa kazi mbalimbali. (Zek. 1:7-11; Dan.10:13; 12:1; 1The. 4:16; Yuda 1:9; Efe. 1:22; Kol 1:16).
Enzi Utawala, Nguvu, Mamlaka,
MASERAFI NI NANI?
Kuna Maserafi na wana mabawa sita (angalia Isa. 6:2,6). Wana nguvu uwezo wa kuondoa makosa yaletayo dhambi na kuwandaa manabii kwa kuwatakasa (Isa. 6:7). Kuwa na mabawa sita inadhihirisha ukuu na uwezo wao katika katika utendaji wao wa kazi mbalimbali.
NENO MASERAFI MAANA YAKE NINI?
Neno Maserafi ni neno la wingi wa neno saraph (SHD 8314) likiwa na maana ya mwenye kuchoma kwa moto. Kwa sababu ya nyoka katika Hesabu 21:6,8 walikuwa na sumu inayochoma kama moto wakati wanapouma, kwa hiyo wakaitwa maserafi. Kwa hiyo hawa maserafi ni “moto wa mbinguni” (linganisha pia Kum. 8:15; Isa. 14:29; 30:6). Mungu aliwatuma ili waweze kuwadhibu watu waliotenda dhambi. Maumbile yao walionekana kuwa kama wandamu kwa vile walikuwa na nyuso, mikono na miguu juu ya umbile lao la kuwa na mabawa. Wanawakilishwa kama wenye “kusimama wakati wote” juu ya wote. Mfalme anaposimamisha enzi yake, tayari kwa kumhudumia.
Hawa ndiyo Malaika Wakuu na wana nafasi muhimu sana katika Jeshi la mbinguni. Ni Malaika wakuu ndiyo mara nyingi hutumwa katika nchi kuleta ujumbe wa Mungu na maonyo kwa wanadamu na kwa manabii.
Katika kitabu cha Henoko kinataja majina ya Malaika wakuu:
Mikaeli, Gabriel, Urieli Malaika Mkuu wa dunia na watu wakali) na Raphaeli, Ragueli (ambaye analipiza kisasi juu ya dunia na mwangaza) na Saragaeli.
Kitabu cha Henoko, sura ya 20, R.H Charles, 2002).
Malaika hawa pia wanaitwa Malaika Walinzi.
Malaika Mkuu Gabriel:
• Alitafsiri maono ya Danieli (Dan. 8:16, 26; 9:20-27)
• Alitangaza juu ya kuzaliwa kwa Yohana Mbatizaji (Lk. 1:11-20)
• Alitangaza kuzaliwa kwa Yesu (Lk. 1:26-38).
Malaika Mkuu Mikaeli:
Mikaeli Mwana mkuu wa Mfalme, ametajwa mara nyingi katika Agano la Kale.
• Katika Daniel 10:13 ametajwa “Jemedari mkuu aliyekuja kunisaidia.” Angalia pia Daniel 12:1
• Yuda 1:9 Mikaeli Malaika Mkuu, anagombana na Shetani kuhusiana na Mwili wa Musa.
• Ufunuo 12:7-8 Mikaeli pamoja na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake.
Hawa maserafi wanatambulikana kama makerubi wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu kama tunavyoona sasa.

MAKERUBI NI NANI?:
Kiti cha Enzi cha Mungu kinazungukwa na wanyama wanne wenye vichwa tofauti. Hawa ni Simba, Ndama, Tai na Mwanadamu, wanatambulikana kama Makerubi (umoja Kerubi) wako wanne katika jumla ya hesabu yao na wana mabawa sita wanakizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu (Ufunuo 4:6-9). Maelezo ya makerubi yanaelezewa katika Ezekiel 1:5-14; 10:20; na Ufunuo 4:6-9. Ambapo wameumbika katika viungo mchanganyiko katika Ezekieli wakiwa walinzi wa Yehova wa Israeli na wanaonekana wenye mabawa manne katika viwiliwii vyao vya juu. Hapa hawajatajwa kuwa na mabawa mawili katika miguu yao kama wale Makerubi wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu, au wale wa moto katika Agano la Kale. Idadi ya hao Makerubi kuwa wanne inatokana na Uumbaji. Wakati makerubi hawa wanapotumwa katika nchi, kwa ajili ya Yehova wa Israeli, na kutenda kwa pamoja huwa na mabawa manne na wanatembea pamoja katika gari daima wakiangalia sehemu moja. Makerubi wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu wana mabawa sita kama maserufi.
Mfano wa vichwa vya viumbe wanaokizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu wanatabulikana kama makerubi katika Ezekieli 1:1-28.
Vichwa vya wanyama vinaashiria vita vya Wana wa Israeli na mgawanyiko wa makabila katika idadi ya 10 na 11.
Tangu mwanzo kulikuwa na Makerubi wanne, makerubi wawili wanakizunguka na makerubi wawili wakisimama nyuma ya Kiti cha Enzi cha Mungu. Ezekieli 1:4-14 anaelezea juu ya makerubi wane; na hii ndiyo idadi ya “viumbe wane wenye uhai” wanaotajwa katika Ufunuo 4:6
Makerubi wanatajwa katika kitabu cha Mwanzo 3:24 ambapo tunasoma ya kwamba Mungu alimfukuza mwanadamu kutoka katika Bustani ya Edeni na kuweka Makerubi, na upanga uwakao moto katika sehemu ya Mashariki ya Bustani ya Edeni, kumzuia mwanadamu asirudi na kula tunda la mti wa uzima.
Katika 2 Samweli 22:11; Zaburi 18:10 na Ezekiel sura 1,9 na 10 inaonekana ya kwamba uzima wa milele umesimama juu ya Makerubi wanne.
Tunaona mifano ya Makerubi inavyotumika, katika Hema ya kukutania pamoja na kwenye Hekalu. Wale waliyo katika Sanduku la Agano wanaitwa “Makerubi wa Utukufu” (Ebrania 9:5), kutoka kwa hao Makerubi Utukufu wa Mungu unaoonekana hukaa kwao.
Makerubi wawili walitengenezwa kwa dhahabu, na wakiangaliana na mabawa yao yakiwa yameinuliwa, huwekwa juu ya sanduku la Agano (Kutoka 25:17-20). Mungu (kwa kupitia katika malaika wake aliahidi kuzungumza na Musa “kutoka kati ya Makerubi” (Kutoka 25:22). Mifano ya Makerubi iliwekwa katika mapazia ya Hema ya kukutania (Kutoka 26:1,31).
Mfalme Sulemani alikukuwa na Makerubi wawili waliotengenezwa kutokana na mbao za Mzeituni, na kuwekwa Hekaluni. Makerubi pia waliwekwa milangoni na kwenye sehemu za ukutani katika Hekalu, na mifano ya makerubi iliweza kushonewa katika nguo zilizotumika Hekaluni (1 Falme 6:23-35; 2 Nyakati Sura ya 3).
Ingawaje Biblia inatwambia ya kwamba tusijifanyie sanamu ya kitu chochote cha mbinguni au cha duniani (Kutoka 20:4; Kumbukumbu 4:16), Wana wa Israeli waliamriwa kufanya picha za Makerubi katika kuta za hema ya kukutania. Hizi zilikuwa ni mifano tu na hazikuwa za kuwabudiwa. Hema ya kukutania ambayo Musa alijenga na Hekalu alilojenga Sulemani ilikuwa mifano halisi inayowakilisha mambo ya mbinguni.
USIKOSE SEHEMU YA SABA. MALAIKA MIKAELI NA KAZI ZAKE.......
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW