Friday, July 14, 2017

AYA ZA SHETANI NDANI YA QURAN, SEHEMU YA TATU

Image may contain: text


Pingamizi la 8 la Waislam wa madhehebu ya Suni: Shaykh al-Albani, kwenye vitabu vyake vinavyohusu mtiririko wa waenezaji wa tamaduni, alisema ushahidi wa aya za Shetani una mlolongo mbaya wa ueneaji (isnad).
Itikio: http://answering-islam.org/Responses/ Saifullah/sverses.htm inasema, "Kuhusu al-Albani, nimefahamishwa kuwa siku hizi al-Albani ameelezwa vibaya sana kwa kutokuwa sahihi kuhusu isnads, hata anaandika kwenye kitabu kimoja kuwa mtu fulani ni mkweli lakini kwenye kingine anasema kwamba jambo hilo si sahihi! Kitabu kiitwacho Al-Albani Unveiled kilichoandikwa na Sayf ad-Din Ahmed Ibn Muhammad Amirul Islam kinatoa mifano mingi sana. Upande wa nyuma unasema: Kitabu hiki ni uchunguzi mchanganifu wa mmoja wa mashehe muhimu zaidi wa Hadithi(Muhammad Nasiruddeen al-Albani) wa harakati ya kisasa ya kiislam inayojulikana kama ‘Salafiya’. Mtunzi ameeleza wazi kabisa kupingana kwa Al-Albani kwa kutumia msaada wa kazi iliyoandikwa kwanza kwa Kiarabu (Tanaqadat al-Albani al-Wadihat), na mwanazuoni wa wa Hadithi wa Kijordani anayejulikana sana - Shakh Hasan ibn Ali al-Saqqaf."
Pingamizi la 9 la Waislam: Watu wasio Waislam wanampinga Muhammad na uislam.
Itikio: Tukio hili halikuundwa na watu wasiokuwa Waislam, bali liliandikwa na Waislam wenyewe. Waislam hawa wasahilina walikuwa na vyanzo vya zamani zaidi kuliko Waislam wa sasa. Kulifumbia macho jambo linalokosoa mtazamo wako kwa sababu tu linakosoa maoni yako, hakuendani na kuufuata ukweli. Kwa kuwa Wakristo wanadai kufundisha ukweli, tunao wajibu wa kumtaja nabii wa uongo. Hatufanyi hivi kwa sababu ya chuki au matakwa binafsi, bali kwa sababu ya upendo na haja ya kuwaona Waislam wanaepukana na mafundisho ya uongo, na kumgeukia Yesu wa kweli na kuwa nasi mbinguni pamoja na Mungu wa kweli.
Unakwenda wapi kutoka hapa?
Waislam wenyewe hawajakubaliana endapo maneno ya Shetani yalikuwemo kwenye Kurani mwanzoni.
Chaguo la 1: Itakuwa vipi endapo Muhammad aliongea kama nabii kuhusu maombezi ya mabinti wa Allah? Jambo hili litamfanya Muhammad kuwa nabii wa uongo kwa kipindi fulani.
Chaguo la 2: Itakuwa vipi endapo Muhammad hakuwahi kusema aya za Shetani? Waandishi wote wanne wa maisha ya Muhammad watakuwa wamekubaliana kukosea kuwa Muhammad alikuwa nabii wa uongo. Baadhi ya watu watachagua, kwa hiari yao wenyewe, kufuata kitu hata kama wanaamini kuwa kiongozi wao aliongea mambo ya Shetani. Hata kama jambo hili ni kweli, utafanya nini na aya za Kurani zinazohusu minong’ono ya Shetani ambayo Muhammad aliipata?
Kwa vyovyote vile, uislam unafundisha kuwa Allah anaruhusu maneno yake yabadilishwe kiasi kikubwa sana, na Allah anaruhusu wafuasi wake wazuri wajifunze njia za uongo kama njia ya ukweli. Hii ni kwa sababu Kurani kwenye Sura 43:44-45, inaonyesha kuwa manabii wote waliotangulia walikuwa na ujumbe mmoja. Sura 41:43 inasema kwamba hakuna kitu kilichotumwa kwa Muhammad ambacho hakikuwahi kutumwa kwa manabii waliomtangulia pia. Kwa hiyo kwa Waislam, ama
a) Allah aliruhusu ujumbe wake uliopotoshwa hapo awali,
b) Au, Kurani ndio ujumbe uliopotoka.
Kwa vyovyote vile, uislam unasema, Allah hawezi kutumainiwa kulitunza neno lake dhidi ya mabadiliko makubwa ya mafundisho.
Mwamini Mungu
Mungu Mwenye nguvu anao uwezo wa kuutunza ujumbe wake. Watu wanatakiwa kumwamini Mungu zaidi.
Mwamini Mungu kuwa amelitunza neno lake. Sura 5:46-48 inasema kwamba Yesu aliithibitisha Torati (kwa wakati wake), Mungu alituma Maandiko kwa Wayahudi na Wakristo, na hata wakati wa uhai wa Muhammad wangeweza kuupima ukweli kwa kuyatumia [Maandiko]. Sura 3:48 na 5:110-111 zinamwonyesha Yesu kuwa alikuwa na Torati na Injili. Wanafunzi wa Yesu pia walikuwa wamevuviwa. Kwenye Biblia, Isaya 59:21; 40:8; Zab. 119:89 zinaonyesha kuwa neno la Mungu hudumu milele. Neno lake halikuwa na kosa lolote hapo awali, na limetunzwa bila makosa (bila makosa makubwa) hadi leo hii. (Isa. 55:11; 1 Petro 1:23-25; Zaburi 119:89, 91, 144, 160).
Tumaini kuwa Mungu anataka uufuate ukweli na uje kwake. Mungu hataki mtu yoyote aangamie (Ezekiel 18:23, 32; 2 Petro 3:9). Watu wote wanatakiwa kuiamini Injili ya Yesu Kristo kwenye 2 Wathesalonike 1:8.
Usimtumaini mwanadamu ambaye maisha yake yana ukomo. Usiwatumaini watu wengine ambao wanakugeuzia mbali na Mungu. "Usiwe mwenye hekima machoni pako (Mithali 3:7). Badala yake, "Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe; katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako" (Mithali 3:5-6). Je unaamini kuwa Mungu anaweza kunyoosha njia zako kama ukimkiri?
Mtumaini Yesu; Yeye ametoka kwa Mungu na ujumbe wa Mungu umetunzwa. Yesu si mwizi wala mnyang’anyi (Yohana 10:8-10). Amini kuwa Yesu alitoa uhai wake kama fidia ya ukombozi (Mathayo 20:28), ili iwe sadaka ya dhambi (Warumi 8:3), kwa njia ya damu yake aliyoimwaga msalabani (Waeb. 10:19).
Mwamini Bwana Yesu nawe utaokolewa (Matendo 16:31). "… ‘Kila amwaminiye hatatahayarika’" (Warumi 10:11). Kwa hiyo mtumaini Mungu, na amini kuwa anaongoza kwa uaminifu. Hakuacha neno lake lipotoshwe, kwa hiyo Biblia inaaminika. Mpe Yesu maisha yako, na atakupa amani na furaha.
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo

No comments:

FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE

  **URGENT UPDATE**   **FORMER MUSLIM EVANGELIST MUSA BELLO ARRESTED BY NIGERIAN POLICE** Shimba TV, New York has received distressing news ...

TRENDING NOW